Header Ads Widget

Diamond Platnumz adai soko la muziki wa kimataifa linamlazimisha kuimba vitu vya kipuuzi,fahamu zaidi hapa..

Msanii wa bongo fleva,Diamond Platnumz amefunguka na kusema kuwa soko la muziki wa kimataifa linamlazimisha kuimba vitu virahisi na wakati mwingine vya kipuuzi kutoakanana ukweli kwamba melody ndio zinauza kwenye soko la kimataifa kuliko ujumbe.
Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa,Diamond amedai mara kadhaa wasanii wa kimataifa wamekuwa wakipenda nyimbo zake ambazo yeye anaziona ni za kipuuzi kuliko zile zenye ujumbe mzuri kitu ambacho kimemfanya awe anafanya nyimbo kwa ajili ya soko la nyumbani na soko la kimataifa.
Soko langu mimi lina vitu viwili,kuna muziki wa nyumbani ambao naufanya miaka yote na muziki mwingine wa uongo uongo ili uweze kufika nchi zingine kwa sababu nchi nyingine zinasikiliza melody tu wanataka wacheze kwa sababu hawaelewi tunachoimba japo mimi sipendi kuandika upuuzi ndio maana natoa nyimbo mbili za kinyumbani na za  kimataifa.Unajua unaweza ukawa na wimbo wa nyumbani mkali lakini mtu wa nje ukimsikilizisha wimbo wa kipuuzi ndio anasema mkali.” alifunguka Diamond

Post a Comment

0 Comments