Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva jana alimtembelea Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Job Ndugai nyumbani kwake  Jijini Dar es Salam na kumjulia hali baada ya kurejea kutoka nchini India alikokwenda kwa ajili ya matibabu.

Akiwa nyumbani  kwa  spika Jaji Lubuva pia alimkabishi  Mh. Ndugai ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa Rais Wabunge na Madiwani  ya Mwaka 2015 na kumueleza kuwa kukamilika kwa ripoti hiyo ndio hitimisho la Uchaguzi Mkuu na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu ujao. 
 
Kwa upande wake Mheshimiwa Ndugai aliipongeza hatua ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya kuweka mikakati ya kushiriki katika maonyesho mbalimbali yakiwemo yale ya biashara SabaSaba na Nanenane katika kutoa elimu kwa wananchi.
 
Jaji Mstaafu Lubuva alikwenda kumjulia hali Ndugai ambaye kipindi  cha Bunge la Bajeti lililomalizika hivi karibuni, alikuwa nchini India kwa matibabu  na hivi sasa afya yake imezidi kuimarika. 
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (kushoto) akizungumza na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Job Ndugai alipokwenda kumtembelea nyumbani kwake Salasala Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (kushoto) akimkabidhi  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Job Ndugai ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2015 wakati alipokwenda kumtembelea nyumbani kwake Salasala Jijini Dar es Salaam.