Header Ads Widget

Riwaya: Mtoto Wa Shetani Shemu ya Nne Na Ally Ayubu Katalambula


RIWAYA: MTOTO WA SHETANI
MTUNZI: ALLY AYUBU KATALAMBULA
SEHEMU YA NNE
Ilipo ishia jana......
Gari lilifunga breki katika geti la gereza la Bangwe,mahabusu wote waliaamriwa kuteremka upesi, walitakiwa kuchuchumaa chini wakati milango mingine ikifunguliwa, taratibu walingia ndani chini ya ulinzi mkali,

Sasa endelea.....
Baada ya kuingia ndani mahabusu wote ambao hawakupata dhamana walitakiwa kurejesha vitu ambavyo awali pindi walipoingia gerezani waliviacha katika ofisi ndogo ya koplo Magreth,kabla ya kurudishiwa,siku ya kesi,ilikuwa ni utaratibu
Sophia alikuwa ni miongioni mwao,alitakiwa kurejesha saa ndogo ya mkononi, akiwa mnyonge alisimama nyuma kabisa ya wenziwe,alipo tupa jicho upande wa pembeni ya mlango aliona chupa ya cocacola,akili yake ilifunguka haraka,haraka aliona ni dhana pekee itakayo tumika kuondoa uhai wake.
Alijisogeza kwa mbele na kwa siri aliinama na kuikota ile chupa,aliivingilisha katika kanga na kujikausha kimya,alikabidhi saa yake, na kutoka nje ya ofisi upesi,
Hakutaka kupoteza muda,alidhamiria kujiua siku ile,ile, alitaka kesho ikuche akiwa maiti,akiwa akhera aliamini atakutana na Ally na wataishi maisha mazuri milele na milele,
Aliingia chooni na jiwe dogo la kupondea ile chupa,aliisaga saga, ile chupa vipande vidogo, kisha akavikusanya vyote na kuviweka katika kiganja chake,alichota maji katika guduria lilokuwa humo chooni na kwa ujasiri alibugia vipande vyote vya chupa akivisindikiza na maji machafu yaliyo katika guduria, aliamini itachukua muda mchache kabla ya kufa,alijifungia kwa ndani hakutaka kutoka nje akiwa hai,japo sakafu ya chooni ilikuwa chafu hakuona vibaya kuketi chini akiwa mwingi wa tabasamu kusubiri MAUTI..
Sophia alifurahi,alitegemea dakika chache zijazo atakuwa katika maisha mengine ya haki na usawa,aliona malaika mtoa roho anachelewa kufika,alichukua vipande vingine vya chupa akavibugia tena akavisindikiza na maji machafu,vilimchana, chana kooni lakini hakujali aliona sawa tu.ama kwa hakika akili ya Sophia ilikuwa imevurugwa.kama wasemavyo vijana wa kisasa!!.
Dakika sita,saba, nane,tisa…bado Sophia alijihisi kawaida kabisa, hakuhisi maumivu ya tumbo wala kichwa, “mbona sifi!.” Sophia alijiuliza moyoni hakuwa tayari kabisa kuiona siku ya kesho,nusu saa ilikatika Sophia akiwa chooni bado dalili za kifo hakuziona alilia mno,alimwomba mungu aitwae roho yake lakini wapi..ilikuwa ni miujiza ambayo hakuwahi kuisikia,
Kengele ya gereza iligongwa ilikuwa ni ishara wafungwa na mahabusu wote kujitayarisha kwa ajili ya kulala, wakati huo ilikuwa imetimu saa kumi kamili jioni,bado dalili ya kifo kwa Sophia ilikuwa kitendawili,hakuwa tayari kutoka ndani ya choo akiwa hai,
Hesabu za mahabusu hazikuwa sawa uchunguzi ulifanyika ikabainika Sophia ndio pekee hayupo, “ hakikisheni anapatika kokote aliko na akamatwe mara moja” ilikuwa ni amri kutoka kwa mkuu wa jela,msako ulianza wa kumtafuta Sophia,haikuwa kazi ngumu kwa muda wa dakika tano askari walikwisha gundua alijifungia chooni,
Ndani ya chumba cha choo Sophia hakutaka kufungua mlango kabisa,hakuwa tayari kuishi katika huu ulimwengu,aliichukia dunia na viumbe vyake vyote, askari magereza walimuamuru afungue malango lakini Sophia aligoma, askari hawakuwa na chaguo jingine zaidi ya kuvunja mlango,
Baada ya kumtoa Sophia ndani ya choo askari magereza hawakuwa na jingine zaidi ya kumcharaza virungu kisawasawa,hawakujali kama wanae mpiga ni mwanamke walimkong'ta kwelikweli, Sophia alilia mno,maisha yake yaligeuka kuwa kilio kila siku,
Tofauti na watu wengine, Ndani ya gereza Sophia hakuwa na rafiki kabisa,hakutamani wala kuona faida ya jambo hilo,usiku wa siku hiyo pengine inaweza kuwa ndio usiku mbaya kuliko siku zote alizo wahi kuishi ndani ya gereza, kufa hakufa ila chamoto alikipata!.Sophia alilia mpaka macho yalimvimba,
Ugumu wa maisha ndio kipimo cha akili,hili lilijidhihirisha kwa Sophia, kuna jambo lilipenya katika ubongo wake,alitafuta utulivu wa muda,alikaa kimya kidogo kwikwi za kilio alizisitisha,alitafakari kwa nukta kadhaa kisha akatikisa kichwa kukubaliana na kile alicho kiwaza.kabla ya kufanya kile alicho kiwaza aliona ni vema asubiri kukaribie kupambazuka,ili mapango wake uendane na muda.
Swalaaaaa,swalaaaaa,swalaaaa,ilikuwa ni sauti ya muadhini, ,ilitimu saaa kumi na moja alfajiri,Sophia alikurupuka mahali alipokuwa amejikunyata,aliona muda wa mpango wake umewadia, alisogea karibu na debe linalo tumika kujisaidia haja kubwa,alifunua mfuniko, alipotupa jicho aliona ndani ya debe kuna kinyesi cha kutosha,
Aligeuza shingo yake kutazama wafungwa wenzake,wote walikuwa wakikoroma,aliingiza mikono miwili katika debe kisha kwa mikona miwili alichota kinyesi kisha akakibugia mdomoni kama mkate,SOPHIA ALIKULA KINYESI akakitafuna kisha akameza!!!!!!!......
Nia ya Sophia ilikuwa ni kujiua,chochote ambacho aliamini ni sumu alikitumia ilimradi ateketeze maisha yake, ajabu ilikuwa tofauti,zoezi la Sophia kubugia kinyesi cha haja kubwa aliendelea nalo, “jamani anakula maviiiii!!!.” ilisikika sauti kali ya mfungwa wa kike aliye mfuma Sophia akibugia kinyesi,
ITAENDELEA KESHO!!

Post a Comment

0 Comments