Mtunzi: EDDAZARIA G.MSULWA
....Nikabaki nimesimama huku sielewi ni kitu gani nifanye nikageuka kiunyonge na kukutana na daktari tuliyemkuta jana usiku akiwa anatembea mwendo wa kasi sikujua ni wapi anapoelekea ikanibidi nimsimamishe.
“Daktari vipi”
“Salama mdogo wangu nakomba tuzungumze baadaye mimi ngoja niondoke hali imeshakuwa mbaya”
“Sijakuelewa dokta?”
“Kuna waziri wa afya amekuja hapa tayari dokta mkuu ameshapigwa chini wewe nakuomba tuondoke kama vipi njoo tuzungumze nyuma huku”
Nikatoka huku nikicheka kimoyo moyo na kusema laiti angejua huyo mtu anaye mkimbia ni mama yangu wala asingezungumza na mimi.
“Ehee kijana shida yako ni nini?”
“Dokta jana nilileta mgojwa hapa mida wa usiku alipatwa na….”
“Ohooo nimekumbuka huyo mgonjwa wako tumemsafirisha kuelekea katika hospitali ya K.C.M.C”
“Hali yake ikoje?”
“Si nzuri sanaa na kama tungembakisha hapa angetufia bure…..Kijana hebu nakuomba uniache niende kwani huyo mama namuona anakuja huku”
Dokta alizungumza huku akichungulia chungulia kupitia mlango tulio tokea nje huku akianza kupiga hatua za haraka kuelekea kwenye njia ya kichochoro iliyopo karibu na Zahanati hiyo.Nikarudi ndani huku nikiwa nawaza ni nini nifanye ili mama aweze kunielewa kama ni kuenda shule niende siku hiyo hiyo.Mama akamaliza kuzungumza na madaktari pamoja na manesi aliowakuta.
“Ehee wee huyo mgonjwa wako yupo wapi?”
“Wamesema wamemuamisha hospitali”
“Nani kasema?”
“Waulize hao madokta hapo”
“Eti kuna mgonjwa aliletwa jana amepata ajali?”
“Ndio muheshimiwa”
“Ahaa bahati yako haya jamani tekelezeni yale niliyo waambia ni bora mupoteze kazi nyingi kuliko kupoteza nguvu kazi ya taifa kwa vifo vinavyosababishwa na uzembe wenu na kuanzia sasa hivi Kiongozi mkuu atakuwa huyo hapo bwana nani vile?”
“Bwana John Henry”
“Ok bwana John ndio atakuwa kiongozi wenu kwa muda hadi pale wizara itakapo leta mtu daktari mwengine sawa jamani.”Madaktari na Manesi wakamuitikia mama kisha akaagana nao pamoja na wananchi kisha tukaingia ndani ya gari na safari ya kurudi nyumbani ikaanza.Tukafika nyumbani mida ya saa saa nane mchana.Wakanishusha getini kisha mama akaelekea kwenye mishuhuliko yake.Mida ya jioni mama akarudi huku akionekana amechoka nikamsalimia na moja kwa moja akaenda chumbani kwake na kulala.Nikakaa nyumbani kwa siku mbili na bila ya kuzungumza na mama kuhusiana na swala la kurudi shule.
“Eddy shule unakwenda lini?”
Mama aliniuliza baada ya kupita mbele yake nikitokea nje huku yeye akiwa amekaa sebuleni akitazama taarifa ya habari ya saa mbili usiku
“Mama nakusikilizia wewe?”
“Unanisikilizia mimi hivi unaakili kweli mwanangu?”
“Sasa mama kuzungumza hivyo ndio mimi sina akili?”
“Nakuona bado unaakili za kitoto.Sasa anaye soma ni mimi au wewe?”
“Ila kumbuka mama wewe ndio uliye niruduisha nyumbani”
“Nilikurudisha ili akili yako ikae sawa.Na sijui hiyo PCB yako unaisoma vipi?”
“Mama mimi Genius”
“Mmmm genius uwe wewe,kesho shule na uondoke na gari ya kwanza uwahi kufaika shuleni?”
“Mama siwezi kusafiri ijumaa”
“Pumbavu wewe usiniletee ujinga nimekuambia kesho alfajiri nikitoka kwenda kazini ninakuacha ubungo sawa”
“Ila mama hizi safari zako za kushtukiza huwa sizipendi kama nini”
“Upende usipende kesho shule”
Kama alivyozungumza mama safari ya kurudi shule ikaanza na akaniacha stendi ya mabasi ya Ubungo mida ya saa kumi na moja asubuhi kisha yeye akaelekea ofisini kwake sikujua ni kwanini siku hiyo amewahi sana kwenda ofisini.Nlicho kifanya ni kutafuta nyumba ya wageni(gest house) iliyo karibu na stendi kwa bahati nzuri nikapata chumba nikaingia na kulala hadi mida ya saa tatu asubuhi kisha nikarudi stendi na safari ikaanza kwa kutumia basi Dar Express na katika siti niliyokaa nipembeni yangu kuna msichana amavalia baibui ninja na ni ngumu kuweza kuiona sura yake.
Hatukusemeshana chochote kiasi kwamba safari nzima kila mtu akawa kimya,kwa bahati mbaya tukakuta ajali ya roli mbili zimegongana maeneo ya Wami kiasi kwamba ikatuchukua muda mrefu kukaa barabarani tukisubiria gari hizo kuja kuondolewa kutokana zimeifunga barabara na hapakuwa na uwezekano wa magari kupita.
“Aisee hii ajali inatuchelewesha”
Msichana niliye kaa naye alizungumza na kunifanya nimtazame kwa muda kisha nikamjibu.
“Wee acha tuu yaani nilisaa la tatu tumekaa hapa na hiyo foleni hapa hadi tuimalieze ni shughuli”
“Ndio tatizo la nchi yetu kukitokea jambo kama hili basi wahusika wataanza kujivuta vuta usishangae hapa tunakaa zaidi ya masaa kumi”
“Kweli na hapa mtu huwezi kusema utahairisha safari kwani nyuma yetu kuna foleni mbele huko ndio usiseme”
“Kuna biashara zangu nilitaka kuziwahi ila hapa nimesha chelewa itanilazimu kulala Arusha kitu nilichokuwa sijakipanga kabisa”
“Ulitaka urudi leoleo?”
“Ndio ila kwa hali hii nahisi hapa kuna kulala”
“Wewe ni mfanya biashata?”
“Ndio ninachukua mizigo ya nguo za wanawae na watoto kutoka Dar na kwenda kuuza Arusha”
“Ahaa hivi hiyo biashara inalipa?”
“Ina lipa pale mtu unapokuwa mchacharikaji ila ukiwa goigoi utaiacha kazi…..Vipi wewe uanashughulika na nini?”
“Mimi ni mwanafunzi nipo kidato cha tano”
“Ahaaa ila si hamjafunga bado?”
“Ndio ila mimi kuna matatizo kidogo yalinipata ndio nikarudi nyumbani ila sasa hivi kidgo nipo powa”
“Soma bwana sisi wengine tulikimbia shule na sasa hivi tunazunguka zunuka na dunia”
“Sawa ila hata wanao soma pia wanaangaika na dunia”
“Ni kweli ila huwa ninawashangaa sana wale wanaosoma na kutaka kuajiriwa.Wanashinda kutumia elimu walizonazo katika kubuni miradi itakayo waingizia pesa wanakazi ya kukaliaa kuhangaika na vijibahasha vyao kwenye maofisi ya watu na mbaya zaidi unakuta mshaara anaolipwa ni waajabu sana”
“Yaani wee acha tuu mdoi maana mimi katika maisha yangu sijapanga kuja kuajiriwa nahitai nijiajiri mimi mwenyewe”
“Ukiwa na nia na malengo utaweza hakuna kinacho shindikana chini ya jua”
Gafla tukasikia mlipuko mkubwa ukitokea katika magari ya mbele ya magari yetu na ikatulazimu tushuke kwenye gari haraka kwenda kuangalia ni nini.Tukakuta moshi mwingi mweusi ukisambaa angani na huku magari mawili ya mbele ikiwemo roli la mafuta lililopata ajali yakiteketea kwa moto mwingi.Watu waliopo kwenye magari ya karibu na magari hayo yanayowaka moto wakaanza kukimbia kurudi nyuma tulipo sisi na kusababisha msongamano mubwa wa watu wanao jaribu kuziokoa roho zao.
“Huu moto utakuja tuu huku”
Msichana alizungumza huku akiwa anafunua kitambaa kilicho iziba sura yake na kujikuta nikimeza fumba kubwa la mate na kubaki nikimtazama jinsi alivyojaliwa uzuri wa sura kiasi kwamba nikajikuta nashindwa kumjibu kitu
“Vipi mbona unanishangaa?”
“Ha…haaa pana”
Kabla sijajibu chochoye gari nyingine mbili zikashika moto na kuanza kuteketea na kwa mahesabu ya haraka haraka gari letu ni la nane kutoka katika gari nne zinazoteketea kwa moto.Polisi wa kikosi cha barabarani wakaanza kuwaomba watu kurudi nyuma kwani hali sio nzuri na muda wowote magari mengine yanaweza kufwata katika kuungua kwa moto.Nikaingia ndani ya basi na kuchukua begi langu la nguo pamoja na pochi kubwa ya msichana huyo kisha nikashuka na tukajumuika na watu wengine kurudi nyuma huku tukizipisha gari za zima moto kufanya kazi yao.
“Kaka unaitwa nani?”
“Ninaitwa Eddy wewe je?”
“Mimi ninaitwa Sheila”
“Una jina zuri”
“Hahaaaaa wapi mbona jina la kawaida”
“Ebwaane ehee hapa safari inaweza ikaahiriswa?”
0 Comments
on