Umoja
 wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wanatarajia kufanya maandamano
 ya Amani nchi nzima Agosti 31 kwa ajili ya kueleza utendaji kazi wa 
Rais Dk.John Pombe Magufuli kwa Watanzania.
Akizungumza
 na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,Kaimu Katibu Mkuu wa 
Umoja huo, Shaka Hamdu Shaka amesema kuwa wameshamwandikia barua mkuu wa
 jeshi la Polisi kwa ajili ya kupata ulinzi siku hiyo
Amesema
 kuwa wasipopata ulinzi watafanya kwa kujilinda wenyewe ikiwa ni lengo 
la kufikisha ujumbe kwa wananchi juu ya utendaji kazi wa Rais Dk. John 
Pombe Magufuli.
Shaka
 amesema kuwa Rais Dk.John Pombe Magufuli amefanya watendaji kuwa na 
utii pamoja na maadili katika utoaji wa huduma kwa wananchi.
Aidha
 amesema kuwa katika maandamano hayo wanaawalika na vijana wa vyama 
vingine kushiriki kwa lengo moja tuu,la kuunga mkono utendaji wa Rais 
Dkt.John Pombe Magufuli.


0 Comments
on