Wimbo wa Aje wa Alikiba umepata shavu kwenye mtandao wa simu wa MTN wa nchini Nigeria.
Aje umekuwa miongoni kati ya nyimbo zinazopatikana kwenye mtandao huo
ambao wananchi wanaweza kuuchagua wimbo huo kuwa kama muito kwenye simu
zao.
Hatua hiyo itamwezesha staa huyo kuendelea kuingiza mkwanja kulingana
na mikataba yake aliyosaini ikiwemo ule wa Sony Music aliosaini mwezi
Mei mwaka huu.