Chadema kimetoa salaam za pole kwa wananchi wote walioathirika na tetemeko la ardhi katika maeneo ya mikoa ya Kagera, Mwanza, Tabora na kwingine, tukio ambalo limesababisha vifo vya watu 16, majeruhi na uharibifu mkubwa wa mali. 

Kupitia taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Idara ya Habari ya Chama hicho, Tumaini Makene, chama hicho kimetoa wito kwa Watanzania wote katika maeneo yaliyopatwa na tetemeko hilo na wengine kutoka nje ya sehemu hizo, kuguswa na tukio hilo na kuwiwa kuwasaidia waathirika wa tukio hilo katika wakati huu mgumu wa kukabiliana na athari zilizotokana na janga hilo. 

Imesema viongozi wa chama katika ngazi mbalimbali, wabunge, madiwani na wanachama wote wa Chadema wataungana na kusaidiana kwa kila hali na wote walioathirika na tukio hilo.