Shaa aliwahi kusema kuwa ni sawa ukawa shabiki wa wote Diamond na Alikiba. Mrembo aliyetumika kwenye video ya Nagharamia, Zahara Zaire, naye ni kama Shaa – anapenda muziki wa mafahari hao bila kubagua.

Na cha kufurahisha zaidi, mrembo huyo amechambua tofauti zao katika kuimba.

“I love both of them,” mrembo huyo wa Kenya, aliiambia Bongo5. “Nafikiri Diamond is naturally an entertainer, on stage ako na hiyo power. “Alikiba is very lyrical, very sensual, miziki yake, I love his songs, they are two different individuals, lakini wote wawili wako poa.”Zahara na rafiki yake Tracey Love aliyekiri pia kuwapenda wote, walikuwa Dar mwishoni mwa wiki, kutembea na kikazi.