Header Ads Widget

RIWAYA: MEMORY CARD. SEHEMU YA KWANZA

.
Baada ya miangaiko ya siku nzima,
Jackson James Mtei alikuwa
nyumbani kwake akijipata chakula
cha usiku.
Nyumba hiyo kubwa yenye hadhi na
mandhari ya kuitwa nyumba ya
kisasa, kijana Jackson alikuwa amekaa
mezani na kijana mwingine aitwae
Sangu ambae alikuwa ni mfanyakazi
wake wa ndani,
"chakula cha leo sio kabisa, nakula
sababu nina njaa tu",Jack
alimwambia Sangu,
"nimezidisha manjonjo bosi, si
unajua lazima nijaribu jaribu kuweka
hiki na kile ila ladha ibadilike",Sang
u aliongea huku akichekacheka,
"usiwe unajaribu jaribu kufanya
mambo yako katika chakula
ninachokula mimi, hayo majaribio
fanya katika chakula chako",Jack
aliongea huku akijifuta mikono na
karatasi maalum ya kujisafishie
mikono,
"umeshiba lakini, au umezila
kula?",Sangu aliuliza huku
akitabasamu kama kawaida yake,
"sijashiba bwana, nitaenda kula
hotelini wakati naenda club
baadae",Jack alijibu huku akibonyeza
simu yake,
"vipi na leo utanitosa tena kwenda
mziki?",Sangu aliuliza huku akiweka
pande la nyama mdomoni,
"sasa tukienda wote nani atabaki na
nyumba?",Jack aliuliza huku akiamia
sebuleni,
"sasa boss walinzi kule nje wana kazi
gani?",Sangu nae aliuliza,
"wale wanalinda nje, wewe unalinda
ndani. Kuna habari gani mpya
leo?",Jack aliamua kubadili mada,
"bora umenikumbusha, Clara alikuja
mchana hapa, alikuwa anakuulizia"
"kwanini hakunipigia simu?",
"anadai ulikuwa hupatikani",
"ukamwambia nimeenda wapi?",
"si uliniambia nimwambie
umesafiri?",Sangu alimuuliza,
"basi poa, mimi simtaki yule demu,
ananing'ang'ania mpaka najuta
kwanini nilimtokea",Jack aliongea
kwa majuto,
"ila mbona yuko poa sana
bosi",Sangu alimsifia Clara,
"kama yupo poa mchukue wewe",Jack
alimuambia Sangu,
"aah acha zako bwana, yule matawi
yenu bwana, kapuku kama mimi
nitampeleka wapi?",Sangu alijibu
huku akijishusha,
"maji si yanatoka?",Jack alimuuliza
Sangu,
"yanatoka, tena yana presha
mbaya",Sangu alijibu huku akiondoa
vyombo mezani,
"maji ya moto ya kuoga naweza
kupata?",Jack aliuliza,
"nakwambiaga kila siku maji ya moto
yanazeesha wewe",Sangu aliongea
huku akitabasamu na kufanya pengo
lake lionekane vizuri,
"we mbona kijana alafu una
mapengo kama mzee?",Jack alimtania
Sangu alafu wote wakaishia kucheka.
Jack baada ya kuoga na kuvaa vizuri,
alitoka chumbani kwake na kumuaga
Sangu,
"kurudi saa ngapi, au unalala huko
huko?",Sangu aliuliza,
"nitarudi saa kumi alfajiri",Jack
alijibu huku akivaa miwani yake
ambayo haikua maalum kwa
wagonjwa wa macho ila ni ya urembo
tu,
"poa, nitaegesha tu mlango wa
mbele",Sangu aliongea huku macho
yake yakiwa ktk TV,
"funga kabisa, wazee wa kazi wasije
kuvamia bure",Jack aliongea,
"watavamia vipi wakati kuna security
guard nje?",Sangu aliuliza,
"hawaaminiki hao. Baadae
jamaa",Jack aliaga na kuondoka zake.
****
Jackson James ni muigizaji maarufu
nchini. Ni mtoto wa mwisho kati ya
watoto wanne katika familia ya mzee
James Joel Mtei.
Hana mke, hana mtoto.
Anaishi na msaidizi wake aitwae
Sangumbwi Amosi ktk nyumba yake
ya kifahari maeneo ya Upanga jijini
Dar es salaam.
*****
Usiku huo wa mwisho wa wiki, mji
ulikuwa umechangamka kutokana na
kumbi mbalimbali za starehe kuwa
wazi, Jack alienda moja kwa moja
katika sehemu ambaya haikua na
kelele sana na kuagiza kinywaji huku
akionekana kumsubiri mtu. Baada ya
dakika 5 akaingia mwanaume mnene
na kuelekea upande alipokaa Jack,
"karibu Mr Mapesa",Jack aliongea
kwa bashasha huku akicheka,
"asante, inaelekea umefika muda
mrefu ee?",Mapesa aliuliza huku
akikaa katika kiti,
"nimeingia sasa hivi, twende kwenye
topic moja kwa moja, maana najisikia
kuumwa",Jack alimharakisha bwana
mapesa,
"hamna jipya, ni yale yale, kesho
twende moro kuangalia eneo la
kuchukulia picha za video",Mapesa
aliongea hayo, kisha wakaongea
mengine mengi kuhusu kazi yao hiyo
na mwisho wakaagana.
*****
Kesho yake mapema, Jack alimuaga
Sangu, kisha akamfuata Mr Mapesa
ambae ni meneja wake na wakaanza
safari ya Morogoro, iliwachukua
mwendo wa masaa matatu kufika ktk
msitu ambao walitakiwa kuchukulia
picha za video, waliongozana na
mwenyeji wa msitu huo ili wasipate
tabu kuujua,
"huku hakuna wanyama wakali
kweli?",Mapesa alimuuliza kijana
walieongozana nae,
"uwa wanaonekana siku moja moja,
wanafuataga swala na digidigi",Yule
kijana alijibu,
"kwa hiyo wawindaji wapo sana
maeneo haya?",Jack aliuliza,
"hawaruhusiwi kuwinda huku,
majangiri ndo wapo wengi",Yule
kijana alijibu, mara wakamuona mtu
anakuja upande wao mbio mbio
huku mwili wake ukiwa umejaa
damu, wakataka kukimbia ila yule
mtu akawapa ishara ya kutaka
msaada, wakamuwahi, walipomfikia,
akaingiza mkono mfukoni akatoa
memory card na kumpa Jack,
"Edward Sambo ana..",Yule mtu
alitamka huku akishindwa kuendelea
kutamka maneno mengine kisha
ukasikika mlio wa risasi na yule mtu
kupoteza uhai, Jack na wenzake
wakakurupuka baada ya kuona vijana
wanne wenye bunduki wakielekea
upande wao..
****ITAENDELEA****