Mahakama ya Hakimu mkazi Arusha imemsomea mashtaka mawili Mwenyekiti wa umoja wa vijana (UVCCM) Lengai Ole Sabaya ambaye pia ni diwani wa kata ya Sambasha Wilaya ya Arusha vijijini .
Miongoni mwa makosa hayo aliyosomewa mahakamani hapo kosa la kwanza alituhumiwa kujifanya Afisa mtumishi wa serekali (TISS)huku kosa la pili ikiwa kugushi moja ya nyaraka za serekali(kitambulisho ).
Akisoma mashtaka hayo mahakamani hapo Wakili wa serekali Lilian Mmasi alisema kuwa Mnamo May 18 katika hotel ya Skyway iliopo makao mapya jijini Arusha Mshitakiwa alijitambulisha kama Afisa utumishi wa idara ya usalama wa taifa na kufanya Utapeli .
Wakili Mmasi alitaja kosa la pili ambalo Mshitakiwa Lengai Ole Sabaya alisomewa kuwa ni kugushi kitambulisho cha idara ya usalama wa Taifa kilichokuwa kikisomeka jamuhuri ya muungano wa Tanzania idara ya usalama wa Taifa (TISS) Lengai Ole Sabaya kikosi maalumu Agent (undercover)chenye code no MT 86117 huku akitambua kuwa ni kinyume cha kisheria .
Hata hivyo mara baada ya kusomewa mashtaka hayo mahakamani hapo mtuhumiwa alikana mashtaka ndipo Hakimu Mkazi aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo Gwantwa Mwamkuga Alisema dhamana ipo wazi iwapo wathamini watakithi vigezo vinavyotakiwa na mahakama hiyo.
Hata hivyo Mshitakiwa alipata dhamana baada ya kukithi vigezo vilivyowekwa na mahakama ambapo ilikuwa ni wadhamini wawili wenye sifa ambapo kwanza awe mtumishi wa serikali pili awe na mali isiyohamishika yenye thamani ya shilingi milioni tatu kwa kila mmoja.
Kesi imeaihishwa na hakimu mkazi hadi itakapotajwa tena October 5 ambapo uchunguzi unatarajiwa kukamilika na kesi hiyo kuanza kusikilizwa.
Mara baada ya kupata dhamana mahakamani hapo wakili wa mtuhumiwa Yoyo Asubui alisema kuwa mshtakiwa amesomewa mashtaka yote mawili na kukana mashtaka ambapo wanatarajia uchunguzi ukikamilika kesi itaanza kusikilizwa mapema na haki kutendeka ,huku akimtaka mteja wake kuendelea na majukumu ya mandeleo kwa wananchi wa kata ya Sambasha.
“kwakweli kesi hii sio ya kweli na naweza kusema ipo kisiasa na nashukuru jeshi la polisi kwa kunishikilia na kukaa na mimi vyema hadi kunileta mahakamani ambapo naamini haki itatendeka na ukweli utabainika “Alisema Sabaya mara baada ya kupata dhamana
Alisema kuwa hili limetokea mara baada ya kuwatoa wabadhilifu wa mali za umoja wa vijana (UVCCM) ambapo kwa muda mrefu wamekuw a mali za umoja huo kujinufaisha wenyewe na vijana kukosa maendeleo kupitia miradi ya umoja huo.