Header Ads Widget

Picha: Vijana 30 kutoka nchi 5 waingia kwenye kijiji cha Maisha Plus

Vijana 30 kutoka nchi tano za Afrika Mashariki, Jumapili hii waliingia rasmi kwenye kijiji cha shindano la Maisha Plus.16Kuwasili kwa vijana hao katika kijiji hicho ambacho hakijulikani kilipo, kulikuwa kukirushwa live kupitia kituo cha runinga cha Azam Two. Wakiwa na mabegi yao mkononi, washiriki hao walipokelewa na mwanzilishi wa kipindi hicho, Masoud Kipanya huku wakiwa wamefunikiwa vitambaa vyeusi machoni.
Masound Kipanya akitoa maelekezo kwa washiriki
Masound Kipanya akitoa maelekezo kwa washiriki

Mshindi wa shindano hilo atajinyakulia kitita cha shilingi milioni 30. Washiriki wote watapewa shilingi 7,000 kwa wiki ili kujikimu wakiwa kwenye kijiji hicho kilichopo katikati ya msitu. Lengo la kupewa shilingi 1,000 kila siku ni kuwafunza maisha ya waafrika wengi ambao huishi chini ya dola moja kwa siku.
Hakuna nyumba kwenye kijiji hicho na hivyo watatakiwa kujenga nyumba zao wenyewe za kuishi.
Tazama picha zaidi hapo chini.
Masoud na Babu wa Kijijini wakiteta jambo
Masoud na Babu wa Kijijini wakiteta jambo

Babu akikagua himaya yake
Babu akikagua himaya yake
1387891112131518192022232425262728293031323435363738401127

Post a Comment

0 Comments