Na jinsi ninavyo ogelea kwenda mbele ndivyo jinsi papa aliyozidi kunikaribia na safari hii akajitokeza vizuri na kuhakikisha kweli ni papa samaki mwenye meno makali ya kumrarua binadamu anaye ingia kwenye kumi na nane zake ndio anaye nifwata kwa mwendo wa kasi na kujikuta nikipiga picha ya jinsi atakavyo nirarua pamoja na huyu msichana mdogo
Endelea...
....Gafla nikasikia milio mingi ya risasi iliyoanza kunichanganya hata mfumo wa kuogelea ukabadilika nikatamani maji ya bahari yabadilike na kuwa mchanga ili miguu yangu ipate uwezo wa kukimbia ila hikuwa hivyo zaidi ya milio kuzidi kuongezeka kwa kasi ya ajabu na kwakiweza sikujua hata ni wapi inapo tokea,maji yakabadilika na kuanza kuwa na rangi nyekundu nikageuka nyuma na kukutana na boti iliyo wabeba watu wapatao wanne wenye bunduki na pembeni nikamuona papa aliyekuwa akinifwata akielea elea juu ya maji akiwa amekufa.
Jamaa wenye boti yao wakaisogeza hadi pembeni na kunitazama kwa muda kisha wakanipa mkono na kunivuta kwa nguvu huku buinti mdogo akuwa mgongoni,wakanipa kitaulo cha kujifunga na kunza kumfwata mama ambaye tayari alisha fika mbali kutoka sehemu ambayo nilikuwepo mimi.Jamaa mmoja alizungumza na simu na sikuielewa luga yake kutokana anazungumza kikabila kisha akakata simu.Wakaisogeza boti yao hadi alipo mama na wakamvutia ndani ya maji.Nikawaona jamaa wakinong’onezana na kisha wakagongeana mikono ikatubidi mimi na mama tutazamane.
“asanteni ka masaada wenu”
Mama alizungumza huku akiwatazama usoni
“musijali kwa hilo”
Jamaa wakaonekana kutawaliwa na furaha ambayo hadi wakati huu sikujua ni ya nini
“mbona munafurahi?”
“tunafurahi kwa maana tumesha kuwa ni matajiri”
“matajiri wa nini?”
“kuna tangazo lilikuwa linatolewa kwa mtu atakaye fanikisha kukupata wewe atapewa dola milioni mbili za kimarekani na baba yako na sasa ni mwezi wa tatu ndio sisi tumekupata”
Nikatabasamu ila ikawa ni tofauti kwa mama ambaye nahisi kuwa anajua ni mume wake mzee godwin
“eddy waambie wanipige risasi ili nife sipi tayari kurudi tena mikononi mwa baba yako”
“mama sio baba wa tanzania?”
“unataka kusema wewe baba yako yupi huyo mwenye roho ya kibinadamu atakaye toa pesa yake ili amzawadie mtu?”
“mama sio baba unaye mjua wewe…tambua kuwa ukweli wote ninauju na ninamshukuru mungu kuwa nimempata baba yangu ambaye yeye ndio damu yeke japo amepitia yaliyo mengi ila ninamshukuru mungu yupo hai”
Mama akabaki kimya huku macho yake yakiwa chini akimtazama mtoto tuliye mlaza chini,tukaona boti nyingine kubwa ikija na kusimama karibu na sehemu ilipo boti hii ndogo,wakatuwekea kingazi na tukaanza kupanda na kuingia kwenye boti kubwa iliyo kuja na jamaa watatu wakingia na kumuacha mwezao mmoja kwenye boti ndogo.Ndani ya boti wakatupa makoti makubwa kwa ajili ya kuzui baridi kali iliyo kuwa ikitukung’uta.
Wakampa msichana mdogo huduma ya kwanza na sisi wakatupatia vyakula na chai ya moto kutoa njaaa tumboni.Mimi wakanihudumia kwenye sehemu niliyo jeruhiwa na jiwe kisha wakanipa suruali mpaya,nikavua kitaulo nilicho pewa na kuivaa suruali hii.Boti ikazidi kusonga mbele huku moyoni mwangu nikijawa na amani tele ya kuweza kumpata mama yangu na kilicho salia ni kuwaunganisha baba mzazi na mama.
“samahani kaka nyinyi ni kina nani?”
“sisi ni wavuvi wa samaki wakubwa sasa yule papa tuliye muua tulikuwa tunamkimbiza alitusumbua sana na pale tumemuacha yule mwezetu akilinda sisi tutamrudia kumchukua na boti nyingine”
“sawa”
Tukafika ufukweni na jamaa wakatupeleka kwenye moja ya hotel isiyo mbali sana na bahari na kutuchukulia chumba,wakamchukua daktari maalumu na kuja kutuhudumia.Tukakaa hotelini kwa wiki moja tukijitahidi kuirudisha miili yetu katika afya zake za kawaida kwani kwa muonekano tulio nao ninaweza kujifananisha na misukule.Mudu wa wiki moja kukatika afya yangu ikarejea kama awali japo sio sana ila kidogo niliweza kusimama mbele ya mtu au watu na kujiona ni mtu.
Gharama zote zikalipwa na mama kutokana na kuwa na akaunti yake ya siri iliyopo huku afrika kusini na kwakipindi chote hatukuwasiliana na mtu yoyote zaidi ya jamaa walio tuokoa ambao nao mama aliwakanya wasizungumze ummbea wa aina yoyote kwa mtu yoyote ili waweze kupata donge lao nono wanalo lisubiria kwa hamu kubwa kutoka kwa baba yangu mzazi
Msichana mdogo alilazwa kwenye moja ya hospitali na madaktari wanaendelea na juhudi za kuweza kumtibu kama ataweza kuzungumza tena ili awe miongoni mwa mashaidi wa kumuhukumu baba mzee godwin katika kesi ya kuwatumikisha watu kikatili na kuwakatili katika kuzungumza nao.
“mama unampango gani na baba?”
”nitahakikisha ninamfunga hadi magereza yanabomoka”
“sawa mama je baba yangu mzazi naye una mpango gani naye?”
“mmmm sijui hata ni wapi nitaanzia kwa maana kwa niliyo mfanyia baba yako kidogo yananipa hata ugumu wa kusema ninaanzi wapi”
“ninafurahi kusikia hivyo mama ila kwa hilo ninaomba uniachie mimi kwa maana baba ananipenda sana”
“ila eddy roho yangu imejawa na dukuduku kubwa ambalo sielewi siku ninamkamata godwin nitamfanya kitu gani?”
“hilo mama wala lisikutie mawazo sana cha msingi ni kuweza kumuomba msamaha baba yangu ili kama ni maisha yaweze kuendelea kwa amani”
“sawa mwanangu nitafanya hivyo”
“je umewasiliana na serikali ya tanzania?”
“mmmm siwezi kufanya hivyo kwanza kutokana huwezi jua baba yako ana mtandao mkubwa kiasi gani ila nitarudi kimya kimya”
“hapo umesema ila yule daktari wako ni mnoko sana na kama unaweza awe miongoni mwa watu wa kushuhulikiwa”
“kwa nini?”
“ana vitu vingi sana ambavyo wewe ukimuambia humuambia baba,kwa mfano swala la kuwa mimi sio mwanaye wewe siku ulipokuwa unamwambia pale sebleni kama sisi.Yeye kaenda kuyang’aza kwa lile jijambazi ndio maana likatumia uwezo wake wa kijeshi kufanya mambo ya ajabu kama haya”
“kumbee hapa ndio ninaanza kupata picha kwa maana siku ambayo waliniteka hospitali baba yako akawa analalamika kuwa nimemdhalilisha na lazima na mimi anidhalilishe”
“ndio hivyo mama je ile siku walikupeleka wapi?”
“walinipeleka sehemu moja hivi wala sikujua ni wapi ila nikaja kukutana na binti mmoja aliniambia anaitwa nani vileee…..”
“nani…..?”
“jina lake limenitoka mara moja alisema na yeye anatokea tanzania na anakufahamua sana wewe na mumeshirikiana sana kwenye mambo mengi”
“sheila”
“eheee huyo huyo….Yule binti alinisaidia sana kipindi nipo matesoni kweni baba yako alinipeleka kwenye jijumba chakavu msituni huko wakanifungia…cha kushukuru mungu yule binti alikuwa akiniletea chakula kila siku usiku kwani wao walikuwa wakinipa vyakula vibaya?”
“kina nani?”
“si hilo jibaba lako na watu wake”
“ahaaa ila sio baba yangu”
“basi siku kama mbili zilipita sikumuona sheila sasa sikujua ni wapi walimpeleka binti wa watu sijui walimuua au”
“hawakumuua….Nilikutana naye hapa kipindi cha katikati akiwa amelishwa makaa ya mawe hawezi kuzungumza”
“weeee ndio maana baba yako akaamua kunipeleka kwenye lile jipango na kuniambia kuwa nitalisha keki za moto”
“ndio”
“basi nakumbuka kipindi ninaingizwa mule sikubahatika kulishwa hayo makaa na walinipiga na kuninyanyasa sana hadi ikafikia kipindi wakanitenga na wezanu na kunifungia kwenye kile kijichumba”
“unajua siku ya mwisho unapigwa mimi ndio niliye kusadia kuuziba mwili wako ili nipigwe mimi badala yako”
Mama akabaki akiwa mdomo wazi na taratibu chozi likamtoka na akanivuta na kunikumbatia kwa uchungu na machozi yakaendelea kumtoka hadi akalowanisha bega langu alilo pitishia bega
Niambembeleza mama hadi akanyamaza na akaniaga na kuingia chumbani kwake kulala na mimi nikabaki nikitazama tv na nikapitiwa na usingizi kwenye sofa nililo kaa.Asubuhi kama ilivyo kawaida daktari maalumu anayetuhudumia akaja kututembelea na kutupa maelezo ya nini tuweze kufanya ili afya zetu ziweze kuhimarika.Nikwasiliana na jamaa walio tuokoa kili waje kutuchukua na watupeleke nyumbani kwa baba.
Baada ya nusu saa jamaa wakawa wamefika na sisi tukawa tayari kwa safri,njia nzima ndani ya gari mama akawa amenishika mkono huku akiwa na futaha sana.Tukafika kwenye jumba la baba na nikamuona mama akitazama tazama kila sehemu
“mama mbona unashangaa?”
“hili jumba lote ni la kwake?”
“ndio”
“amejitahidi”
“mama mbona unashangaa?”
“hili jumba lote ni la kwake?”
“ndio”
“amejitahidi”
Walinzi wakazungumza na dereva anaye endesha gari letu na baada ya kuniona mimi wakaturuhusu.Nikawa mtu wa kwanza kushuka na nikamuomba mama kusubiri ndani ya gari hadi nitakapo kuja kumuita wenyewe wazungu wanasema kumfanyia suprize baba.Nikafungua mlango ndani huku nikiwa na shuuku kubwa sanaya kumuona baba,
“nimesema sitaki kumona huyo kinyago wako humu ndani”
“lazima…….”
Nilizisikia kelele za baba na mke wake wakibishana ila sentesi ya baba haikumalizika na kwakasi kubwa nikashuhudia akinguka kutoka juu gorofani alipo sukumwa na mke wake na akatua kwenye meza ya kioo na kutulia kimya....
*****sory madam*****(40)
......Nikabaki nikiwa nimesimama kama sekunde kadhaa huku macho yangu nikimtizama baba kisha ninayahamishia kwa mke wa baba ambaye hakuzungumza kitu cha aina yoyote,akaondoka na kukimbilia ndani kwa haraka nikamsogelea baba na kumuwekea mkono kifuani na sikuyasikia mapigo yake ya moyo yakifanya kazi,nikapiga kelele za kuomba msaada na walinzi wa baba wakaingia akiwemo mama na akaonekana kustuka baada ya kumkuta baba katika hali kama hii
“eddy amefanya nini?”
Sikumjibu mama zaidi ya kunyanyuka na kuanza kupandisha ngazi za kuelekea gorofani na nikakutana uso kwa uso na mke wa baba akiwa ameshika begi la kuburuza huku mkono wake mmoja akiwa na bastola,akiwa anababaika kuikoki bastola kwa haraka nikamrukia na kusukuma na akaanguka chini na bastola yeka ikaangulia pembeni.
Nikamuwahi kumshika kifuani kwenye shati alilo livaa na nikamnyanyua hadi akasimama na nikumvuta karibu yangu na ngumi mbili za haraka zikatua usoni mwake,akainama huku akiwa ameizima pua yake kwa mikono yake miwili na damu nyingi zikaanza kumtoka,sikuhitaji kumuonea huruma zaidi ya kuiacha mikono yangu kufanya kazi ya kuzichomoa ngumi zenye kasi kubwa na kutua katika mwili wa mke wa baba ambaye aliendelea kulia kama mtoto mdogo
Mke wa baba akaanguka chini na kunipa fursa nzuri ya kuanza kumpiga mateke ya tumbo yaliyo mfanya ajikunje kama samaki mbichi huku damu zikiwa zinamwagika puani na mdomoni.Nikaikota bastola yake na kuikagua kwa haraka na kugundua kuwa ina risasi za kutosha na nikaielekeza kwake kwa hasira
“eddy......Eddy”
Nikaisikia sauti ya mama ikiniita kwa nyuma
“eddy mwangu ninakuomba usifanye hivyo baba yangu nakuomba tena sana mwanangu mpendwa usifanye hilo mwanangu”
“mama huyu mwanamke ndio chanzo cha baba kuanguka kutoka juu na kufa,na hana haki ya kuishi duniani kwahiyo niache nifanye ninacho kitaka kukifanya”
Nilizungumza kwa sauti nzito na nne iliyo jaa uchungu na hasira na machozi yakiwa yametapakaa kwenye sura yangu kiasi kwamba hata mimi mwenyewe nikajishangaa ni wapi hii sauti imetokea
“eddy nakujua mwangu....Nakuomba utulize hasira zako nakuomba mwanangu tafadhali”
Mama alizungumza huku akinisogelea taratibu huku walinzi watutu wa baba wakiwa nyuma yake,nikamtazama mke wa baba jinsi anavyo hema kwa tabu nikayakaza meno yangu kwa kuyang’ata na kwa hasira nikaipiga risasi moja chini karibu na eneo alilo lala na bastola yake nikaitupa pembeni na mama kwa haraka akanikumbatia na kuanza kunibembeleza huku akinipiga piga mgongoni
“shiii....Nyamaza baba yangu usilie baba hajafa tumemuwahisha hospitalini”
Milio miwili ya risasi ilinistua na nikatizama nyuma yangu na kumshuhudia mlinzi wa baba aliyekuwa na mahusiano na mke wa baba akianguka chini na damu nyingi zikiwa zimetapakaa kifuani mwake huku bastola ya yule mama ikiwa mkononi.Mlinzi aliye mfyatulia risasi mwenzake ni yule ambaye alinipeleka bank
“aitaka kuwaua”
Jamaa alizungumza huku akiusogelea mwili wa mwezake na kuuchunguza kama kweli amefariki dunia,mke wa baba akazidisha kulia baada ya kumuona mpenzi wake akiwa amelala chini.Mama akanishika mkono na kuniondoa katika eneo la tukio na kunitoa nje huku akiendelea kunituliza hasira hadi nikarudi katika hali yangu ya kawaida
“baba anaendeleaje?”
“wamemuwahisha hospitalini”
“nani amempeleka?”
“amepelekwa na wafanyakazi wake pamoja na wale vijana walio tusaidia,tuwasubiri warudi ndio tutajua ni hospitali gani ambayo wamempeleka”
“ahaa sawa”
“yule uliye kuwa unampiga ni nani?”
“si ni mke wa baba”
“ahaa na yule mwengine aliye pigwa risasi?”
“ni mshenzi mwenzake ambaye walikuwa wakitembea pamoja na kumzunguka baba”
Tukiwa katika mzungumza ya kawaida tukazishuhudia gari mbili za polisi pamoja na gari moja za wagonjwa zikiingia kwenye geti kuu la jumba la baba na kusimama sehemu ya magari ya kusimama,wakaingia ndani na baada ya muda madaktari wakatoka wakiwa na kitanda cha matairi na juu yake wakiwa wamemlaza mke wa baba na kumuingiza kwenye gari lao na wakaondoka huku wakiwa wanapiga ving’ora.Askari wawili wakatufwata sehemu tuliyo simama na mama na kutusalimia kwa utaratibu.
“tunaimani na nyinyi ni miongoni mwa wahusika kwenye hii nyumba?”
Askari mmoja alizungumza huku akituangalia usoni na mama akanitizama kisha akajibu
“ndio labda tuwasaidie nini?”
“kwa jina ninaitwa afande lawnrance ninawaomba kuwafanyia mahojiano ya nini kilicho tokea muda mfupi uliopita”
“mimi ninaitwa afande martin
Kitu ambacho nimekigundua kuwa askari huyu anaukarimu mkubwa na nitofauti na baadhi ya askari wa tanzania ambaye kwenye tukio kama hili atataka kukutingisha tingisha ilimradi iwe ni shida,mama akashusha pumzi na kumtazama askari lawnrence
“kilicho tokea kwa ufupini kwamba yule mama aliye wahishwa hospitalini alimsukuma baba wa huyu kijana kutoka gorofani hadi chini ninaimani mumeona meza ya kioo iliyo pasuka?”
“ndio nimeiona”
“yaa hilo ndio kubwa ambalo limetokea na mengine mukawahoji wale wafanyakazi wa humu ndani”
“asante mama je kijana una lolote la kuzugumza”
Kwa haraka mama akaniminya mguu pasipo askari kuono tukio hilo
“hapana sina la kuzungumza”
“haya asanteni kwa maelezo yenu”
Wakatupa mikono na wakaondoka na kuniacha nikiwa na wasiwasi mwingi juu ya tukio hili na sheria za hapa afrika kusini hata kama una pesa kiasi gani ila kama umefanya kosa lazima ustakiwe
“mama si watanikama wakiujua ukweli?”
“ndio..Ila cha kufanya sasa hivi nikupeleke kwenye ubalozi wa tanzania uliopo hapa na urudi tanzania na mimi uniache nishuhulikie hili swala”
“mama wewe ubaki.....!?”
“ndio nahitaji kulishuhulikia kwanza hili swala la baba yako la sivyo wataanza usumbufu tena wa kukupeleka mahakamani na ikiwa hivyo ujue ni ishu nyingine tena ya kukuweka mmatatani”
“sasa mama....”
“hakuna cha sasa tena ngoja nizungumze na vijana wa hapa kazi hiyo ifanyike sasa hivi”
Mama akamuita mmoja wa walinzi wa baba na kuwaomba atupeleke ulipo ubalozi wa tanzania
“si unapajua?”
“ndio mama ila mimi sihusiki na maswala ya usafiri na funguo zote za magari zipo ndani”
“eddy si unajua sehemu zinapokaa funguo za magari?”
“ngoja nikatazame ndani kwa baba”
Nikaingia ndani na kuwakuta askari wakipiga picha sehemu za matukio yalipo tokea,moja kwa moja nikaingia chumbani kwa baba na kuanza kufungua kabati moja baada ya jengine na sikufanikiwa kuona funguo hata moja.Nikafungua droo ya kitanda na kukuta funguo mbili za gari pamoja na saa mbili za dhahabu.Nikaziingiza mfukoni saa na kuzichukua funguo na kutoka nje,nikiwa ninashuka ngazi askari mmoja akanifwata na kunizuia.
“angalia usikanyange hiyo kwenye hilo sehemu lililo chorwa”
Alinielekeza nisipite kwenye sehemu ambayo wameichora kama ushaidi,nikapita pembeni na kutoka nje na kuwakuta mama na mlinzi wakitusubiria.Tukafika sehemu yenye magari ya baba na kuitoa funguo moja na kuminya kitufe kilichopo kwenye gari kikiwa na matumizi ya kulifungua gari husila la funguo hiyo.Gari moja likatoa mlio na sote tukajua ndio gari husika la funguo hii.Nikamkabidhi mlizi funguo na sote tukaingia ndani ya gari na kuondoka.
Tukafika kwenye ofisi za ubalozi wa tanzania na mama akashuka na kuniomba nibaki ndani ya gari na baada ya muda akatoka na kuniita kwa ishara na sote tukangozana hadi ndani ambapo akaanza kunitambulisha kwa balozi wa tanzania afrika kusini bwana marki msuya na baadi ya wafanyakazi wa ofisi hii.
“tena mumekuja muda mzuri kwa maana leo ndio siku ya wale vijana wa tanzania walio zamia huku na kukamata ndio wanarudishwa”
“wanatumia usafiri gani?”
“serikali ya hapa imetupa ndege tuwarudishe vijana wetu wapo kama 248 hivi”
“si kijana wangu anaweza kupata nafasi kwa maana mimi ninahitaji kubaki huku kuna ishu nitaishuhulikika kabla ya kurudi nchini”
“ndio nafasi zipo.....Za masiku dada yangu kwa maana ninayo taarifa kuwa umetekwa na al shabab?”
“ahaa tutazaungumza baadaye kaka yangu ila kikubwa kwanza tumshuhulikie huyu kijana wangu”
Mipango ya mimi kurudi tanzania ikaanza kushuhulikiwa na jina langu likawa ni miongoni mwa majinina ya vijana wanao rudishwa tanzania kwa kuingia nchini afrika kusini pasipo kuwa na kibali maalumu.Mida ya saa nane mchana tukafika uwanja wa ndege wa o.R. Tambo international uliopo johannesburg na nikajumuishwa na baadhi ya vijana nilio wakuta katika sehemu za kusubiria ndege muda wa kuondoka huku wakiwa chini ya ulinzi mkali wa askari.Mama akanikumbatia kwa ishara ya kuniaga.
“ukirudi hakikisha humuambii mtu yoyote ni wapi nilipo na hakikisha kuwa unafwatilia nyendo zima za baba yako na utakuwa unawasiliana na mimi”
“nitawasilia vipi na wewe kwa maana sina simu?”
Mama akamuita balozi wa tanzania na akamuoma namba yake ya simu ambayo akaiindika kwenye kikaratasi na kunikabidhi mimi
“hiyo utaitumia kuwasiliana na mimi kwa maana mama atakuwa kwangu”
“sawa”
Muda wa kuondoka ukawadia na tukaongozwa hadi kwenye ndege ambayo ndi maalu kwa sisi kuondoka na tukaanza kuingia kwa majina na mimi nikawa mtu wa mwisho kwenye orodha ya majina na kuingia ndani ya ndege na kukuta wezangu wote wamekaa kwenye siti zao.Nikaanza kutafuta siti niliyoa ambiwa na muhudumu nikae.Kila abiria akawa ananitazama na macho yangu yakagongana na macho ya sheila akiwa amejifunga kitambaa kichwani na pembeni yake amekaa jamaa mwengine
“sheila?”
“bee”
Nikampa mkono nikataka kuanzisha mazungumzo ya kujua ni nini kimempata ila muhudumu akaniomba nikakae kwenye siti yangu iliyopo nyuma kabisa kwani ndege imebakisha dakika chache kabla ya kuondoka.
Nikakaa kwenye siti yangu na kujufunga mkanda na nisita ambayo pembeni hapakuwa namtu yoyote na mashine za ndege zikawashwa taratibu,kwa kupitia kwenye kioo nikazishuhudia gari sita za polisi zikija katika eneo ilipo ndege na kuizuia isiondoke na katika kuchungulia vizuri nikamuona askari lawrance akizungumza na waongozaji wa ndege wa chini akiwaomba ndege isiondoke na wakihitaji kumshusha mmoja wa abairia wa ndege hii na kwa haraka nikajua ni mimi ndio wamenifwata na kuyafanya mapigo yangu ya moyo kuanza kwenda kasi na amani ikanitoweka moyoni mwangu
Itaendelea......
0 Comments
on