Majagina wa muziki wa Afrika Mashariki na washindi wa tuzo kibao, Sauti Sol (Kenya) wameachia video ya wimbo wao unaofanya vizuri, KULIKO JANA, uliopo kwenye santuri yao ya tatu: Live and Die in Afrika.

Bien wa Sauti Sol anaelezea maana ya wimbo huo, “Unamaanisha kuwa uaminifu wa Mungu haukomi kamwe. Huruma yake haiishi – kila uchao ni vipya.” Wakimshirikisha Redfourth Chorus (Upper Hill School), wimbo huo mtamu lakini wenye ujumbe mzito, umezikwea chati na kuwagusa mashabiki barani Afrika na zaidi.
Video maarufu ya Sauti Sol wakiimba akapela ya wimbo huo wakiwa na Redfourth Chorus, ulivutia masikio ya watu mashuhuri duniani na kwenye vyombo vya habari hadi kumfanya Amber Riley, nyota wa kipindi kilichoshinda tuzo za Emmy, Glee, kuandika kwenye Instagram, “Sielewi wanachokisema lakini najua ni kizuri. Inasikika kimalaika, kuna yeyote anayejua kama kuna video?” Mastaa wengine waliowahi kuiweka video hiyo kwenye mitandao ya kijamii ni pamoja Master P, Anthony Hamilton, Jb Smoove na WorldstarHipHop, miongoni mwa tovuti zingine za habari za kimataifa.
Katika video mpya iliyotoka yenye rangi nyeusi na nyeupe ya KULIKO JANA, Sauti Sol wameungana na chipukizi lakini mweye kipawa cha hali ya juu, Redfourth Chorus kwa maajabu ya kimuziki. Sauti Sol wamesema kwenye taarifa yao, “KULIKO JANA ni wimbo maalum sana kwetu. Ulihamasishwa na safari yetu na rehema zisizoisha, mapenzi na baraka ambazo Mungu ametuonesha muda wote licha ya udhaifu wetu.”
Video ya KULIKO JANA imetayarishwa na Fulfillment Limited, na kufanyika Kenya na waongozaji wakiwa Tim Mwaura na Joash Omondi. Wimbo umeandikwa na kutayarishwa na Sauti Sol. Kipande cha akapela kilipangwa na Philip Tuju na Redfourth