Mkurugenzi wa Kituo cha Mkubwa na Wanawe, Mheshimiwa Diwani, Bwana Saidi Fella ameonyesha bidhaa maalum za mavazi ya bendi hiyo ambayo yataingizwa sokoni kwa ajili ya biashara kwa nchi nzima ambapo wadau wameombwa kujitokeza kwa wingi kuwaunga mkono.
Bidhaa hizo amezizindua rasmi Septemba 2.2016 ni nguo aina mbalimbali zenye nembo ya Yamoto Band huku wakitoa tahadhari kwa wananchi kutoingilia nenmbo hizo kwani tayari wamesha zisajili kwenye mamlaka husika ikiwemo Brela na COSOTA.
Bidhaa zenye nembo ya kundi ama msanii husika ni miongoni mwa njia ya kujiingizia kipato hivyo kwa hatua hii bendi hiyo mbali na muziki itaweza kusonga mbele na kupiga hatua katika shughuli zao.Mkurugenzi wa Kituo cha Mkubwa na Wanawe Saidi Fella akionyesha baadhi ya bidhaa zenye nembo ya Yamoto Band zitakazopatikana nchi
0 Comments
on