Hivi karibuni kwenye siku yake ya kuzaliwa akiwa anafikisha miaka 30 rapa Drake ametoa nyimbo nne na moja wapo ya nyimbo hizo ina maneno makali kwa wasanii wawili ambao ni Push T na Kid Cudi. Nyimbo hizi zipo kwenye orodha ya nyimbo zake za kazi mpya ya More Life.
Kwenye wimbo huu Drake amemuita producer Pusha T ‘Muuza dawa za kulevya akiwa studio’ na kusema matatizo anayopitia Kid Cudi ni Phase tu.
Haya ndio mashairi ya wimbo huu wa “Two Birds, One Stone”.
“My numbers are out of the world, no wonder they got me feeling so alienated, You were the man on the moon, now you go through your phases, Life of the angry and famous“
Na Mistari ya Push T “But really it’s you with all the drug dealer stories that’s gotta stop though,You made a couple chops and now you think you Chapo,If you ask me though you ain’t lining in the trunk with kilo’s“
Mashabiki wa hiphop wamechukizwa na mistari hii kwa Kid Cudi ambaye kwa sasa yupo chini ya uangalizi kutokana na msongo wa mawazo na matatizo mengine ya kibinafsi yanayoweza msababishia kujidhuru mwenyewe.
0 Comments
on