Pale unaponunua simu mpya, kinachofuata ni kuhamisha vitu vyako vyote kutoka katika simu ya zamani kama vile contacts, picha, video, baadhi ya apps na vitu vingine vingi. Lakini kuhamishi vitu vyote hivi huwa inachukua muda mwingi sana kama hutotumia njia sahihi za kufanya hivyo.
Hebu leo tuangalie baadhi ya njia sahihi na za haraka za kuhamisha vitu kutoka katika simu moja kwenda nyingine.
1. Kuhamisha Contacts
Contacts zako ni moja ya vitu muhimu zaidi katika simu yako. Zile enzi za kunakili contact zako zote pembeni na kuzisave upya katika simu zimepitwa na wakati.
A. Hamisha kwa kutumia SD Card
Funga sehemu ya Menu => Manage Contacts => import/export contacts. Hapa utaweza kuhamisha contacts kutoka katika simu yako ya zamani. Kuzisave katika simu yako mpya fuata step kama za hapo juu ila kwenye kuexport/import utachagua uzisave kwenye simu. Njia hii ni kwa wale wenye simu zenye sehemu ya kuweka slots za memory cards.
B. Hamisha kwa kutumia Account yako ya Google (Gmail)
Gmail wamerasisha zaidi zoezi la kuhamisha contacts kwa kuweka chaguo maalumu la contacts synchronization kwa vifaa vyote vinavyotumia account moja ya gmail.
Ili kuweza kutumia huduma hii inakupasa kutumia email account moja ya google katika vifaa vyako vyote. Kufanya hivyo nenda kwenyesettings=>Accounts=>Google=>Add new Account kama haipo kisha katika sehemu ya synchronization weka on ili kuruhusu simu yako kushare contacts zake na simu nyingine zenye account kama hiyo.
C. Kuhamisha kwa kutumia laini ya SIM (SIM Card)
Hii ni njia ya kizamani japo inaendelea kusaidia watu. Faida kubwa ya njia hii ni uwezo wa kuchagua contacts zipi uhame nazo na zipi uziache. Unachotakiwa kufanya ni kuwa na SIM Card isiyokuwa na majina kabisa na kucopy majina yote kutoka katika simu yako ya zamani na kuyahamishia katika simu yako mpya.
Tatizo kubwa la njia hii ni uwezo wake mdogo wa kuhamisha contacts 200 tu kwa pamoja.
2. Jinsi ya kuhamisha SMS zako
Kama bado unazipenda baadhi ya sms zako kama za malipo ya bili mbalimbali, usitie shaka unaweza ukahama nazo pia kwa msaada wa app inayoitwa SMS Backup and Restore ambayo inafanya kile ulichokitarajia. App hii ni ya bure kabisa na unaweza ukaipakua kutoka Playstore.
3. Jinsi ya kuhamisha picha, video na miziki
Hapa kuna njia nyingi kama vile kutumia SD Card yenye uwezo mkubwa kucopy na kuhamishia kwenye simu mpya au kutumia baadhi ya apps za cloud storage kama Google Drive, Google Photos au DropBox kuhamisha vitu vyako. Tatizo la njia hizo zinahitaji kiasi kikubwa cha data.
Hivyo kwa urahisi tumia kompyuta yako kuhamisha mafaili kwa kuyacopy kwenye kompyuta kwanza alafu kuyahamishia kwenye simu mpya.
4. Jinsi ya kuhamisha Applications na data zake
Hapa utahitajika uwe umeiroot simu yako. Sikushauri kufanya hivyo kwa simu yako mpya kwa sababu unaweza ukaharibu warranty ya simu yako. Baada ya kuiroot tumia application ya Titanium Backup, app hii itakuwezesha kubackup kila kitu katika simu yako.
Haya sasa kazi ni kwako wewe na simu zako tuu.
0 Comments
on