Malkia wa filamu Kajala Masanja amefunguka kwa kusema kuwa anatamani kupata mtoto wa pili wa kiume huku akiweka wazi aina ya mwanaume ambaye atazaa naye.

Mwigizaji huyo ambaye ana mtoto mmoja wa kike aitwaye Paula aliyezaa na prodyuza maarufu Bongo, Paul Matthysse ‘P Funk’, amesema anahitaji Paula apate kaka yake.

“Najua mtoto ni mtoto lakini kwa sasa natamani kuwa na mtoto wa kiume ili Paula naye ajivunie kuwa na kaka. Siku zote nilitamani nipate watoto wenye jinsia tofauti na sasa tayari ninaye wa kike ni zamu ya kumpata mwingine wa kiume,” Kajala aliliambia gazeti la Mtanzania.

Aliongeza, “Natamani kuzaa na mwanaume yeyote aliye tayari na anayejitambua na kuwa tayari kuitwa baba na kugharamia matumizi ya watoto wangu na kuipa familia matunzo bora.”

Kwa upande mwingine, Kajala ameweka wazi kuwa anatamani kuvuka nje ya nchi kimafanikio, jambo ambalo tayari kwa sasa limeanza kuonesha dalili kwa kiasi kikubwa.