Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.January
Makamba ameendelea na ziara ya kikazi katika Mkoa wa Rukwa. Katika ziara
yake Waziri Makamba ameshuhudia uharibifumkubwa wa mazingira hususan
pembezoni mwa ziwa Rukwa.
Waziri
Makamba amewaambiwa wakazi wa Kijiji cha Nankanga kwamba mwaka 2000
kina cha maji katika ziwa Rukwa kilikuwa ni mita sita, na kwa mwaka 2016
chanzo hicho kimepungua hadi kufikia mita tatu.
“Tafiti
zinaonyesha kuwa kupungua kwa kina hicho pamoja na mambo mengine
kunasababishwa na kilimo cha milimani na kandokando ya ziwa, na
ulishajiwa mifugo katika Vyanzo vya maji,” Makamba alibainisha.
Katika
ziara yake baada ya kushuhudia uharibifu mkubwa kiasi hicho, Waziri
Makamba ameazimia kulitangaza eneo la Ziwa Rukwa kama eneo mahsusi kwa
mazingira na kanuni za matumizi ya maeneo hayo zitaandaliwa ilikunusuru
Ziwa Rukwa.
Pia,
wakurugenzi wote wa Halmashauri za Mkoa wa Rukwa wameagizwa kutenga
pesa zitokanazo na tozo mbalimbali ili waweze kugharamia uwekaji wa
alama maalumu ‘beacons’ ili kuainisha eneo tengefu na kuagiza kuwazoezi
hili lifanyike haraka.
Aidha,
Mhe. Makamba amesisitiza juu ya upandaji wa miti na ameonyesha
masikitiko yake kwa Mkoa wa Rukwa kuwa na upungufu wa miti ya asili na
ile ya kupanda kwa kiwango kikubwa. “nimetembea zaidi ya kilomita 200
sijaona miti iliyopandwa,” Makamba aliongezea.
Wakazi
wa Mkoa wa Rukwa wamefahamishwa na kusisitizwa kuwa kuanzia mwakani
itakuwa lazima kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kuripoti na
miti na kutakiwa kuitunza mpaka pale watakapomaliza shule. Waziri
Makamba ameahidi kuleta wataalamu na kutoa orodha ya miche inayostawi
katika kila kijiiji ili kurahisisha uoteshaji wa miti.
Katika
hatua nyingine, Waziri Makamba amekutana na viongozi mbalimbali wa dini
na wazee wa Mkoa wa Rukwa na kuwataka kuunda Kamati ya Amani,na kuahidi
kugharamia Mkutano wa kwanza wa kuundwa kwa baraza hilo nakusisitiza
agenda ya mazingira iwepo.
Mkoani
Rukwa Waziri Makamba ametembelea mwalo wa ziwa Rukwa na kuzungumza na
wananchi wa maeneo hayo na Mkutano wa Hadhara katika
Na Lulu Mussa, Sumbawanga
0 Comments
on