Moja ya habari iliyoandikwa kwenye magazeti ya October 5, 2016 ni hii kutoka gazeti la Mwananchi yenye kichwa cha habari ‘Muziki tiba ya kukosa usingizi’Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>Djadam64.com Tayari nimezikusanya na waweza kuzipata huko.
Muziki ni tiba ya usingizi wakati wa usiku? Hilo ndilo swali ambalo wataalamu wengi huhangaika kupata majibu. Hata hivyo wakati juhudi za kutafuta tiba kwa wanaokosa usingizi usiku zikiendelea kupitia tafiti mbalimbali, Leo nakusogezea ushahidi wa kisayansi kuwa, Muziki husaidia kupunguza tatizo hilo.
Kwa mujibu wa utafiti, mtu asiyepata usingizi baada ya kupima afya yake na kuonekana hana tatizo lolote la kiafya, anashauriwa kutumia muda mwingi usiku kusikiliza muziki laini ili mishipa ya fahamu ifanye kazi vizuri.
Utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha Tubigeng cha Ujerumani, umeonesha kuwa muziki wa taratibu ni msaada wa kuongeza uwezekano wa mtu kuoata usingizi. Imeelezwa kuwa muziki husaidia kumfanya mtu anayetaka kulala kuimarisha kumbukumbu zake.
Kiongozi wa utafiti huo Dr. Jan Born anasema mtu anayesikiliza muziki wa aina hiyo hupata usingizi kwa urahisi tofauti na msikilizaji wa miziki mingine, hasa ile ya Hip Hop. Mtaalamu huyo anasema muziki huo huingia taratibu katika mishipa myembamba ya ubongo ambayo husaidia kufanya mwili wa binadamu na kupumzika kwa urahisi, hivyo kumrahisisha kulala.
Dr. Jan Born ameeleza kuwa Ubongo wa binadamu una mishipa isiyohitaji kelele ambayo hufurahi pale inaposikia sauti nyembamba au laini. Mishipa hiyo ndiyo huratibu mfumo mzima wa utulivu wa fahamu na wakati huo huo kurahisisha mawasiliano kati ya sehemu moja na nyingine ndani ya mwili katika mzaingira na hali ya utulivu, ili kuvifanya viungo muhimu vipumzike.
Ripoti ya Mtaalamu wa Saikolojia ambaye pia mkurugenzi wa taasisi ya Timamu Counseling, Anania Maulid anasema watanzania wengi wana tatizo la kukosa usingizi linalosababishwa na changamoto za kila siku za maisha.
Anania anasema hali iliyopo nchini haitofautiani na nchinnyingine zinazoendelea ambazo wananchi wake hufanya kazi katika viwanda vyenye mashine chakavu zinazotoa milio mikubwa ambayo huathiri mfumo wa usingizi kwa binadamu. Inaelezwa kuwa mtu anapofanya kazi katika mazingira yenye kelele, usingizi wake huwa wana kushtuka shtuka ambao huleta madhara.
Moja kati ya magonjwa yaliyotajwa kumpata mtu anafanya kazi kwenye makelele na kutopata usingizi ni pamoja na ugonjwa wa Moyo pamoja na Kiharusi ambacho huchangiwa na mtu kutopata usingizi mzuri, tatizo lililotajwa kukua kwa kasi zaidi nchini Tanzania.
Mtaalamu huyo wa masuala ya Saikolojia amesisitiza kuwa kuna ugumu katika kupata tiba ya moja kwa moja ya usingizi iwapo muhusika hana maradhi mengine yanayoambatana na suala hilo huku akiitaja Tanzania kuwa na waathirika wengi zaidi kuliko inavyodhaniwa.
0 Comments
on