Header Ads Widget

VANESSA MDEE AINGIA STUDIO NA PRODUCER WA NYIMBO 6 ZA BEYONCE, SEAN GARRETT, NA NYOTA WA THE VOICE 3, AVERY WILSON

Vanessa Mdee yupo nchini Marekani kufanya mambo makubwa. Ameingia studio kurekodi wimbo na producer na mwandishi maarufu wa nyimbo nchini Marekani, Sean Garrett.


Vanessa Mdee akiwa studio na Sean Garrett (kushoto) pamoja na Avery Wilson

Pia wameungana na aliyewahi kuwa mshiriki wa shindano la The Voice msimu wa tatu, Avery Wilson. Wote kupitia akaunti zao za Instagram wamepost picha wakiwa studio kwaajili ya kazi hiyo.
“Musical Exchange with my brothers @averywilson and @seangarrettthepen,” ameandika Vanessa.
Naye Sean ameandika: The World ðŸŒŽ is one!!!Peace and love Africa!Salute u @vanessamdee and My brother @averywilson.”
Kwa upande wake Avery amesema: In The Studio Tonight With @vanessamdee – She’s Lit In Africa.”
Wafahamu zaidi wakali hao:
Sean Garrett

Pengine Sean alifahamika zaidi Tanzania baada ya kushirikishwa na Nicki Minaj – kwenye wimbo wake wa mwaka 2010, Massive Attack. Lakini Garrett amehusika kwenye kuandika na kutayarisha nyimbo kubwa ukiwemo wa Usher, Yeah!
Nyimbo zingine alizoandika ni pamoja na Goodies ya Ciara, Make Her Feel Good wa Teairra Mari, Break Up wa Mario, Buttons wa Pussycat Dolls na Toy Soldier wa Britney Spears.
Hushirikiana katika kutengeneza muziki na Swizz Beatz na pamoja walitengeneza nyimbo kadhaa za Beyoncé Knowles zikiwemo “Ring the Alarm”, “Get Me Bodied”, “Upgrade U”, “Check on It”, “Diva”na “Video Phone”.
Avery Wilson

Ni muimbaji, mwandishi wa nyimbo na dancer, ambaye mwaka 2012 alishiriki kwenye shindano la The Voice msimu wa 3. Baadaye alikuja kusainishwa na Clive Davis na RCA Records.
Mwaka 2015 alirejea kwenye The Voice Season 8 na kuimba wimbo If I Have To

Post a Comment

0 Comments