Yemi
Alade alishinda tuzo ya msanii bora wa kike, na Tekno akachukua ya
msanii bora aliyechipukia kwenye tuzo za MTV MAMA 2016 – hawa wawili
hawakwepeki na hakuna ubishi ni miongoni mwa wasanii wa moto zaidi
Afrika kwa sasa.
Wapopo hao wametajwa kutumbuiza kwenye kilele cha tamasha la Fiesta,
litakalofanyika jijini Dar kwenye viwanja vya Leaders, November 5.
Hiyo sio mara ya kwanza wawili hao kuja Dar. Supastaa na nguli wa muziki
wa Uganda, Jose Chameleone naye atatumbuiza kwenye show hiyo.
Wasanii wengine watakaopanda jukwaani siku hiyo ni pamoja na Alikiba,
Raymond, Mr Blue, Belle 9 ba wengine. Bado haijajulikana ni msanii yupi
kutoka Marekani atakayetumbuiza mwaka huu.


0 Comments
on