Mchekeshaji maarufu nchini, Emmanuel Mathias aka MC Pilipili amesema tayari ameshaanza mchakato wa kuandika kitabu kinachohusu maisha yake.
Akiongea na DJADAM Jumamosi hii, MC pilipili amesema ameona kuna umuhimu wa vijana wenzake kijifunza mambo mbalimbali aliyopitia katika maisha yake mpaka akafanikiwa.
“Mashabiki wangu wasubirie kitabu changu kipya cha historia ya maisha yangu, ni kitabu ambacho kimesheheni matukio yakusikitisha ambayo yatawaaminisha watu kwamba kila kitu kinawezekana kwenye maisha,” alisema MC pilipili. “Kwa hiyo kuna mtu nimempatia kazi ya kukiandika na tayari ameshaanza kufanya mahojiano na Mama yangu pamoja na wadogo zangu ili kupata baadhi ya stori kutoka upande wao,”
Pia alisema kitabu hicho kitauzwa sehemu mbalimbali ili kuwapa watu nafasi ya kukinunua na kujifunza baadhi ya mambo hasahasa suala la kutokata tamaa kwenye maisha.
0 Comments
on