Story zilianza kuvuma mitandaoni zikimuhusisha chipukizi ambaye alikuwa chini ya lebo ya muziki ya The Industry (Selline) na uongozi wa lebo hiyo kuwa uongozi huo umemtema mwanadada huyo katika lebo hiyo.
Kuondoa utata wa mambo DJADAM64 imemtafuta C.E.O wa lebo hiyo Nahreel na kupiga nae story kuhusiana na suala hilo, Nahreel amefunguka juu ya hilo na kuthibitisha kuwa habari hizo zina ukweli na wamefanya hivyo kutokana na utovu wa nidhamu wa msanii huyo.
“Yes, tumemsimamisha msanii wetu mmoja ambaye anaitwa Selline, na ni kwasababu tu ya utovu wa Nidhamu na kushindwa kufanya kazi chini ya uongozi. Mambo mengi ni ngumu kuelezea kwenye media lakini kiufupi ni hivyo tu. Kwahiyo sasa hivi kazi yoyote inayomuhusu msanii huyo sisi hatuhusiki nayo.”Alisema Nahreel.
Unaweza kumsikiliza Nahreel akibonga juu ya hilo kwa kuplay hii video hapa chini.
0 Comments
on