Wananchi
katika jimbo la Chalinze mkoani Pwani, wamekiri kuona mwanga kwa jinsi
viongozi wanavyotatua matatizo yao, kufuatia kuongezeka kwa
ushirikishwaji wa wananchi katika kutoa kero zao mbele za viongozi na
kujadiliana utatuzi wake kwa pamoja.
Kauli hiyo imetolewa wakati wa mkutano kati ya wananchi wa kitongoji cha Visakazi kata ya Ubena Chalinze na Mbunge wa Chalinze RIDHIWANI KIKWETE, ambapo sehemu kubwa ya wananchi waliohojiwa wameonyesha kukubali kwamba mikutano ya majadiliano mara kwa mara kati ya viongozi na wananchi huongeza ufanisi katika utendaji.
Naye
Mbunge wa Chalinze kwa upande wake amebainisha kuwa mikutano hiyo ni
sehemu ya utaratibu wa kiuongozi ambao amejiwekea katika kuhakikisha
anatatua kero za wananchi wake kwa wakati muafaka na kwa kiwango
kinachotakiwa.
Wakati
wa mkutano huo, wananchi hao wameshukuru kwa kazi kubwa ambazo tayari
zimefanyika katika jimbo hilo ikiwemo uimarishaji wa huduma za afya,
elimu na pamoja na mambo mengine ya kijamii.
“Mbunge
huyu amekuja na staili kama ya wakati wa mzee wake wananchi tunapewa
nafasi tunasema hata yetu binafsi naamini hii itasaidia sana na utakuwa
karibu na wananchi wako", alisema Bi Semeni Masound,
Aidha wameelezea kuridhishwa na juhudi zinazoendelea kuchukuliwa katika kutatua migogoro kati ya wakulima na wafugaji.
Katika
hatua nyingine Mbunge Ridhiwani ameshiriki katika mazishi ya Mama mzazi
wa Diwani wa zamani Kata ya Bwilingu Ndg.Rashidi Shomari Lugazo.
Mbunge huyo ataendelea na ziara ya kutembelea wananchi tarehe 5 novemba.
Mwenyekiti
wa Chama cha CCM Tawi la Visakazi akieleza baadhi ya malalamiko ya
wananchi mbele ya Mbunge wao Ridhiwani Kikwete hayupo pichani kwenye
ofisi ya chama hicho katika mkutano.
Mbunge
Ridhiwani Kikwete wa pili upande kushoto akishiriki katika mazishi
Mama mzazi wa Diwani wa zamani Kata ya Bwilingu Ndg.Rashidi Shomari
Lugazo na wa kwanza upande wa kulia ni Sheikh Hussein wa Bwilingu akitoa
neno la Mawaidha katika msiba
0 Comments
on