Header Ads Widget

RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 47 & 48


Mwandishi: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA       
Akaminya honi zake kwa nguvu ili mtu uyo kuweza kupisha njiani, na mbaya zaidi dokta Maliki aligundua amasimama katikati ya daraja la Sarenda. Kwa haraka akilini mwake akahisi ni majini ambao mara kwa mara inasadikika yanaonekana kwenye daraja hilo. Akawasha gari yake ila haikuwaka akajaribu kuliwasha gari lake ila halikuwaka kabisa. Mtu aliye simama mbele ya gari lake taratibu akaanza kugeuka huku sura yake akiwa ameiinamisha chini. Alipo inyanyua sura yake, macho ya Dokta Maliki yakamuona vizuri Samson akiwa amsimama mbele yake, huku akiwa tumbo wazi, mikononi mwake akiwa amshika bastola mbili zilizo elekea chini.
   
ENDELEA
Samson hakuhitaji kumuacha hai dokta Maliki, akafyatua risasi zipatazo ishirini, zilizo vunja kioo cha gari ya dokta Maliki, na nyingi zikatua kifuani kwake na huo ndio ukawa mwisho wa maisha ya dokta Maliki. Samson akapiga hatua hadi kwenye gari la Dokta Maliki, akafungua mlango wa gari hilo ili kuhakikisha kwamba adui yake amesha poteza maisha. Alipo hakikisha dokta Maliki tayari amekuifa, akarudi kwenye gari walipo raisi Praygod pamoja na Rahab. 
 
“Tayari Madam Rahab”
“Kazi nzuri”
Wakaondoka katika eneo la daraja ili kuto kuweza kuingia mikononi mwa askari ambao hawakujilikana watafika muda gani kwenye eneo hilo, kwani ni tayari askari wa nchi nzima walipewa jukumu la kuimarisha ulinzi masaa ishirini na nne, kwani usalama wa nchi bado ni hali tete.
                                                                                              ***
Agnes akiwa katika wazo la kufikiria kutoka nje ya treni hiyo inayo kwenda kwa kasi, binti huyo akavunja kioo kimoja kwa kutumia kishikizo cha jambia lake. Upepo mwingi ukaanza kuingia ndani ya treni hiyo
 
“Tunatoka sasa”
Binti huyo alizungumzakwa sauti ya juu kutokana na upepo huo mwingi. Binti huyo akachungulia nje, alipo ona kuna usalana, hakuhitaji kupoteza muda akapanda kwenye dirisha hilo huku akiwa ameshikilia vizuri kwa ndani. Kabla ya kupanda juu, akamtazama Agnes ambaye anaonekana kuhofia kitendo hicho.
“Hei jikaze, unahitaji kukamatwa?”
Binti huyo alizungumza huku akimtazma Agnes. Hapakuwa na jinsi yoyote ya kuweza kufanya, binti huyo akatoka ndani ya behewa hilo na kwautaalamu mkubwa alio nao akapanda juu ya behewa hilo. Agnes akashusha pumzi kuuondoa woga, akafanya kama alivyo fanya binti huyo, chakushukuru Mungu akafanikiwa kupanda juu ya behewa hilo alipo mwenzake.
 
“Tunafanyaje sasa?”
Agnes aliuliza kwani hakuelewa ni kitu gani ambacho kinakwenda kutokea kwa wakati huo, na jinsi akitazama mwendo kasi wa treni hilo akajikuta akizidi kuchanganyikiwa.
“Tunaruka”
“TUNARUKAAA…..!!”
“Ndioo”
“Ahaaa siwezi kufanya hivyo, nitakufaaa”
“Tunafanyaa jiamini, pale mbele kuna daraja chini kuna mto mkubwa”
“Ndio turuke………?”
Wakiwa katika kujadiliana ni nini cha kufanya, kwa mbali wakaiona helcoptar ikija kwa kasi ikitokea nyuma, kwao treni inapo tokea. Katika kuitazama vizuri binti huyo akagundua kwamba ni helcoptar ya jeshi la Marekani.
 
“Shitii…..”
Akamkumbatia Agnes, kisha kwakutumia nguvu, akajirusha naye kuelekea kwenye mto mkubwa unao pitisha maji mengi. Agnes akawa na kazi ya kupiga makelele kwani hakujua watakapo fika chini watakuwa hai au laa. Kila mwanajeshi aliye kuwa kwenye helcoptar hiyo, walio pata habari juu ya uvamizi wa mabinti hao, alijikuta akishangaa kitendi hicho, kwani kuruka kutoka juu ya treni hadi kwenye mto huu kuna urefu mkubwa sana, ambao kama mtu akiruka ni lazima atakutana na mauti yake ndani ya mtu huo.
Wakawashuhudia mabinti hao wakidumbukia ndani ya maji hayo mengi yanayo kwenda kwa kasi sana.
“Sir tunafanyaje?”
Mwanajeshi mmoja alimuuliza mkuu wao wa kikosi waliye kuwa naye ndani ya helcoptar hiyo.
“Peleka helcoptar karibu na mtu huo”
“Sawa mkuu”
Rubani huyo akafanya kama alivyo agizwa na mkuu wake, kutokana na uwezo wa helcoptar hiyo aliweza kuishusha karibu sana na mtu huo kuangalia kama mabinti hao wapo hai au wamesha kufa. Hawakufanikiwa kuwaona wasichana hao ambao hakuna aliye weza kujua kama wamechukuliwa na maji au kufia ndani ya mto huo.
 
“Wasiliana na kikosi cha maji waje kutoa msaada”
Mkuu huyo alimuagiza msaidizi wake, akafanya kama alivyo agizwa, kwani hawakuhitaji kuweza kuwapoteza wasichana hao, haswa Agnes aliye weza kufanya mauaji ya kiongozi wao, jambo lililo zua simanzi kubwa sana kwa wamarekani wengi, ukiachilia simanzi iliyo wakumba pia ni aibu kubwa sana kwa nchi kubwa iliyo endelea kama hiyo, kiongozi wao mapoja na askari walio aminika kumlinda kiongozi wao nao pia waliuawa kikatili
“Hawa malaya nilazima tuwakamate”
Mkuu huyo wakikosi alizungumza huku akiwa amekunja ngumi ya mkono wake wa kulia akiwa na hasira kali, kwani masaa ishirini na nne waliyo pewa na raisi wao ya kumkamata binti huyo yanazidi kuteketea pasipo mafanikio ya aina yoyote.
Baada ya muda mchache, wanajeshi wa majini wakafika katika sehemu walipo ingia mabinti wanao watafuta, kazi ya kuwasaka ikaanzia hapo, huku  kila mmoja akijitahidi kufanya anacho weza kuwatia nguvuni wasichana hao.
                                                                                                 ***
“Muheshimiwa kuna barua ujumbe wako”
Msemaji  wa ikulu alimfwata raisi Praygod Makuya, mara baada ya kufuki ikulu wakiwa wameongozana na mke wake pamoja na Samson.
“Umetoka wapi?”
“Whait House Marekani”
Raisi Praygod hakuwa na wasiwasi mkubwa, kwani Tanzania inaushirika mzuri sana na nchi hiyo kubwa duniani na alicho weza kukiamini, ujumbe huo utakuwa ni wapole kwa yale yaliyo weza kujitokeza.
 
“Baby muangalie mtu wako”
“Sawa”
Raisi Praygod akaondoka na kumuacha Rahab na Samson wakipelekwa kwenye chumba kingine kwa kuweza kuzungumza. Raisi Praygod alicho weza kukifanya ni kuweza kuivua sura ya bandia aliyo weza kuivaa, moja kwa moja akaongozana na msemaji wa ikulu, hadi ndani ya ofisi maalumu ya mawasiliano. Tv kubwa zote zilizomo ndani ya chumba hicho zikawashwa, ili kuweza kufanya mawasiliano na kiongozi mwenzake wa nchi hiyo kubwa. Kutokana na urafiki wao wakaribu, wakasalimiana kwa furaha, huku raisi wa Marekani akimpa pole raisi Praygod kwa yale yaliyo weza kujitokeza.
“Ila ninatatizo kubwa kuliko hata hilo lakwako”
Raisi wa Marekani alizungumza, huku wakitazama Raisi Pragod Makuya kwa kupitia Tv hizo kubwa
 
“Tatizo gani ndugu yangu?”
“Waziri wa mambo ya nje bwana Paul Henry Jr ameuawa”
“Weee Paul amefariki…….!!?”
“Ndio tena ameuawa na kijana kutoka nchini kwako?”
“Nchini kwangu!!?”
“Ndio, tena ni msichana mdogo tu mwenye umri kama miaka ishirini na nne au tano”
Raisi Praygod akajikuta akichoka kwa taarifa hizo, kwani Mtanzania huyo hakujua anauwezo gani wa kuweza kufanya mauaji makubwa ya kiongozi anaye lindwa sana
“Praygod, kwa hili nimeamua kulishikilia mimi mwenyewe, ila kutokana wewe ni mtu wakaribu ninakuomba kitu kimoja. Nitakapo mkamata huyu msichana, nimuue”
 
Raisi wa Marekani alizungumza maneno yaliyo mfanya Raisi Praygod Makuya kukaa kimya huku akimtazama kiongozi mwenzake.
“Hembu naomba hiyo picha niiione yahuyo muuaji”
Picha hiyo ikatumwa kwa njia ya emali, msemaji wa raisi akaitoa picha hiyo na kumkabidhi raisi Praygod, aliye jikuta akiitumbulia macho picha ya msichana huyo kwani kati ya wasichana wanne walio isumbua nchi ya Tanzania katika swala la ujambazi huyu ni miongoni mwao.
“Je unaniruhusu kumuondoa duniani huyu muadiani?”
“Utakapo mkamata, nitakuomba kama rafiki yangu tuweze kukutana kulizungumze hili”
“Sawa ni kutokana ni wewe, laiti angekuwa anatokea nchi nyingine nisinge omba hata kibali cha kuweza kumuua, kwani ameua vijana wangu kama ishirini”
 
“Ishirini…..?”
“Ndio ishirini wale wote walio kuwa wakimlinda Paul, kwani wote walikuwa Russia kwenye ziara ya kikazi”
“Sawa tutashirikiana kwani mimi pia ninawatafuta hao mabinti waliniulia wanajeshi wangu wengi”
“Basi mimi na wewe ni kitu kimoja, tuendele kuwasaka”
“Sawa”
“Basi tunaendelea kufahamishana kila linalo endelea”
“Sawa”
Mawasiliano yakaishia hapo, Raisi Praygod akaitazama vizuri picha ya Agnes
“Hawa mabinti kumbe bado wapo?”
“Hata mimi nimeshangaa muheshimiwa”
“Ngoja nikapumzike, kesho nitahitaji viongozi wote wa usalama wa taifa wafikie ofisini kwangu”
“Saa ngapi?”
“Saa moja asubu wawe hapa, fanya nao mawasiliano”
“Sawa muheshimiwa”
Raisi Pragod akaondoka na kuelekea kwenye chumba walipo Samson na Rahab, akawakuta wakiendelea na mazungumzo.
 
“Mumefikia wapi?”
Raisi Pragod alizungumza mara baada ya kukaa kwenye moja ya kiti kilicho pembeni mwa meza hiyo.
“Ni mengi ambayo tumeyazungumza, labda wewe useme unahitaji kuyasikia yapi?”
Rahab alizungumza huku akimtama mume wake
“Ahaaa mwaka huu nitachanganyikiwa”
“Kwa nini?”
“Kuna kiongozi wa Marekani ameuawa”
“Kisa?”
“Hata sifahamu, ila muuaji ni huyu hapa”
Raisi Praygod akampa picha mke wake. Rahab akashtuka mara baada ya kukuta ni Agnes rafiki yake wakaribu sana.
“Agnes…….!!”
Samson baada ya kusikia jina la Agnes, akaichukua picha ya aliyo ishika Rahab kwa haraka na kutazama ni Agnes anaye mfahamu au laa. Hakuwa ni mwengine bali ni Agnes kati ya mabinti alio kuwa akishirikiana nao.
“MUNGU WANGU………!!”
Samson alizungumza huku akitetemeka mwili mwimza hadi Rahab na Raisi Praygod Makuya wakalistukia hilo.
 
“Vipi unamfahamu?”
Rahab aliuliza
“Ndio nimefanya nao kazi, na kwasasa wapo chini ya gaidi la kimataifa bwana Rusev”
“Rusev, Rusev ndio nani?”
“Ni mmoja ya magaidi wanao taka kuipindua nchi ya Rusia na kama kuna uwezekana kuishikilia dunia kwa ujumla”
“Mmmm kuishikilia dunia!!?”
Raisi Pragod aliuliza kwa mshangao mkubwa sana kwani kinacho weza kuzungumza na Samson ni kitu cha kustaajabisha sana.
“Ndio, kuna maraisi Kumi na tano wanatakiwa kufa”
Samson alizungumza huku akimtazama raisi Praygod Makuya.
“Kati ya hao kumi na tano, wewe pia ni mmoja wapo”
Raisi Praygod akajikuta akijichokea, kwa mbali machozi yakaanza kumlenga lenga, kwani kama kiongozi huyo wa Marekani ameuawa, na muuaji hakuweza kukamata kiurahisi, basi hata yeye anaweza kuuwa muda ni siku  yoyote
                                                                                     
                                   SHE IS MY WIFE(48)

“Usijali sana mume wangu nitakulinda”
Rahab alimfariji mume wake baada ya kuona amefadhaishwa na taarifa alizo weza kuzitoa Samson.
“Twende tukapumzike”
Raisi Praygod alizungumza huku akiondoka ndani ya chumba, huku sura yake dhahiri ikioshesha hana furaha hata kidogo.
                                                                                                 ***
Kwa uwezo mkubwa aliokuwa nao binti aliye weza kumsaidia Agnes, aliweza kuendelea kupambana na maji mengi yanayo kwenda kwa kasi huku akiendelea kumshikilia Agnes vilivyo. Ili kuto kuweza kumpoteza Agnes ambaye kwake ni muhimu sana kwa lile ambalo anahitaji kwenda kulifanya na binti huyo.
 
Kwa bahati nzuri maji hayo yakawapeleka hadi kwenye moja ya mto mkubwa uliotulia na unao katika katika msitu mmoja mkubwa. Akamtoa Agnes nje ya maji, ambaye hali yake ni mbaya kiasi, hii ni kutokana na kushindwa kuweza kuhimili msukomo wa maji hayo ambayo yalikuwa yakiwapeleka kwa kasi. Akampa huduma ya kwanza Agnes, huku akiendela kuuchunguza mwili wa Agnes.
“Shit….”
Msichana huyo alizungumza huku akichomoa kisu chake kidogo kwenye mguu wake wa kushoto, akaushika vizuri mkono wa kulia wa Agnes na taratibu akakipitisha kisu chake kwenye maeneo ya bega la Agnes na kumfanya akurupuke
“Unataka kufanya ni……..?”
“Tulia”
Msichana huyo, akatoa kipande kigogo ya mawasiliano alicho kuwa ameingiziwa Agnes kwenye bega lake na bwana Rusev ili kila anapo kwenda aweze kuonekana.
                                                                                                ***
Kila aliye kuwa kwenye chumba cha wamaasilano alijikuta akitumbilia macho computer kubwa iliyomo ndani ya chumba hicho, kwani ni mawasiliano yao na Agnes yaliweza kukatika gafla
“Ni nini kumetokea?”
Bwana Rusev aliwauliza watu wake wa mawasiliano kwa kufoka
“Ku….kuu…kuu kuna tatizo”
Mmoja alijibu kwa kubabaika
“Nini wewe, tumempotezajee”
Bwana Rusev aliendelea kubabaika kwa kufoka sana, kila mmoja akaendelea kuhangaikia jinsi wanavyo weza kumpata Agnes kwenye mitambo yao kwani maandishi makubwa yasomekayo  NO SIGNAL, yalijitokeza.
Swala la Agnes kutoweka, likazidi kuwachanganya Fetty, Halina na Anna. Kila mmoja wasiwasi  mwingi ulimjaa dhidi ya rafiki yao huyo, hawakuhitaji kupungua zaidi ya hapo walipo fikia, kwani rafiki yao kifpenzi Rahab hadi leo hawafahamu yupo wapi.
 
“Bosi tunaomba kazi ya kwenda kumtafuta Agnes”
Fetty alizungumza kwa kujiamini, akiwa amesimama wima na mikono yake akiwa ameirudisha nyuma. Bwana Rusev akaka kimya pasipo kujibu kitu chochote, akili yake haikuwa na kitu chohote cha kuwaza zaidi ya kumfikiria Agnes, binti aliye tokea kumpenda na kumuamini kati ya mabinti wote wanao mtumikia.
“Mutampatia wapi?”
“Inabidi kuweza kutambua mto huo upo eneo gani?”
“Nyinyio tafuteni eneo la mto lilipo”
Bwana Rusev aliwaamrisha mafundi mitambo wake ndani ya chumba hicho cha mawasiliano.
“Sir mto huo unaitwa AMUR, ni sawa na kilometer 260 kutoka hapa tulipo”
“Toeni ramani ya mto huoo”
Ramani ikatolewa kama alivyo agiza bwana Rusev, akawakabidhi Fetty na wezake wawili, walio ipita kwa muda, kisha wakaelekea kwenye vyumba vyao kwenda kujiandaa na kazi hiyo ambayo kila mmoja aliamimi itakuwa ni ngumu kwake.
 
“Tuhakikishe tunarudi wote salama salimini sawa”
Fetty alizungumza huku akifunga kamba za buti yake ndefu aina ya travota
“Sawa, je situchukue vijana wawili watusaidie katika hili?”
“Anna sisi tunatosha kuikamilisha hii kazi”
“Ila Fetty alicho kisema Anna kina maana si kila kitu sisi tunaweza kukifanya kumbuka kwamba hii si Tanzania ambayo tumeizoea, tupo ugenini huku”
Maneno aliyo yazungumza Halima yakamfanya Fetty kuwa muelewa, kwani ukitazama leo ndio siku yao ya kwanza kutoka nje tangu walipo ingia kwenye ngome hii, iliyopo kwenye miamba mikubwa chini ya bahari. Kila mmoja alipo hakikisha kwamba amebeba silaha yake, aliyo ona inafaa kwenye zoezi zima la kwenda kumtafuta Agnes, wakatoka ndani cha chumba na kurudi chumba cha mawasiliano na  kumkuta bwana Rusev akiendelea kuweweseka kwa wasiwasi mkubwa, kwani mtu aliye mchukua Agnes hadi sasa hivi hawatambui ni nani.
 
“Tupo tayari”
Fetty alimuambia bwana Rusev, akawatazama jinsi wasichana hao wanavyo jiamini kisha akashusha pumzi nyingi akitafakari cha kuzungumza.
“Ahaa…ahaa hakikisheni munarudi wote”
“Sawa mkuu”
“Ila mutaidi muwe na vifaa maalumu tuwe tunawasiliana”
Kila mmoja akafungwa kifaa cha mawasiliano, kila mmoja alipo kamilika wakatoka na bwana Rusev kwenda kwenye eneo lenye maegesho ya helcoptar zakijeshi. Wakakuta vijana wengine wanne walio jiandaa tayari wakiwasubiri.
“Mutaongozana na hawa vijana”
“Sawa mkuu”
“Nawatakia  kila laheri katika kazi yenu”
“Asante mueheshimiwa”
Wote wakaingia kwenye helcoptar hiyo, kwa kutumia mitambo mikubwa, sehemu ya juu ya eneo hilo ikafunguka na taratibu helcoptar hiyo ikatoka na kuanza safari ya kuelekea kwenye mto Amur.
                                                                                          ***
“Tuondoke hili eneo”
Binti huyo alimuamrisha Agnes, baada ya kukifunga  kwa kitambaa sehemu alipo mchana na kiu na kutoa kifaa malumu kilicho mfanya kuweza kuonekana kila anapo kwenda kw akutumia mitambo ya Satelaite.
“Tunakwenda wapi?”
“Utafahamu ni wapi tunapo elekea”
“Ila samahni, nahitaji kujua wewe ni nani?”
“Utanijua hapo baadaye, ila kwa sasa tunahitaji kusonga mbele, kumbuka kwamba unatafutwa na jinsi tunavyo endelea kukaa hapa ndivyo jinsi tutakavyo jikuta tunakamatwa”
 
Agnes hakuwa na pingamizi zaidi ya kuongozana na binti mwenzake kuingia kwenye msitu huo wenye miti mirefu sana kwenda juu. Masaa na majira yakazidi kukatika hadi kigiza kikaanza kutawala anga, wakazidi kutembea kusonga mbele pasipo kuchoka, hadi wakafanikiwa kufia kwenye moja ya kijiji, ambacho binti huyo aliweza kuongoza na Agnes mpaka kwenye moja ya nyumba, iliyo tengenezwa kwa mbao na wote wakaingia. Wakamkuta mmzee mmoja mwenye nywele ndefu, na sutra ya kichina akiwa amekaa chini na kukunja miguu yake pamoja na mikono akionekana kama yupo kwenye ibada.
Wakasimama nyuma yak kumsubiria mzee huyo kuweza kumaliza anacho Sali, baada ya muda mzee huyo akawageukia na kuwatazama.
“Monk nimerudi”
Binti huyo alizungumza kwa lugha ya kijapani na kumfanya Agnes asiweze kuelewa kitu cha aina yoyote.
“Kazi nzuri, muandalie sehemu mzuri ya kulala”
“Sawa Monk”
Binti huyo akatoa heshima kama alivyo zoea ufanya kwa watu kama hao ambao ni wacha Mungu, ila pia ni watu hatari sana kwenye maswala ya kupigana. Akamuandalia Agnes chumba ambacho angeweza kujipumzisha kisha akarudi sehemu alipo waacha yeye na Monk. 
 
“Tayari Monk”
“Je ameiona sura yako?”
“Hapana”
“Unaweza kumuonyesha”
Msichana huyo, taratibu akaivua kitambaa kilicho funika kichwa chake pamoja na sura yake, Agnes akabaki akiwa amemtumbulia mimacho kwani ni binti mwenye asili ya kiafrika, isitoshe ana kifahamu kiswahili vilivyo.
“Naitwa JACKLINE”
Binti huyo alijitambulisha mbele ya Agnes huku akimpa mkono wa salama, Agnes taratibu naye akaopokea mkono huo na kusalimiana naye.
“Mimi ni mtazania kama ilivyo kuwa wewe, ila ninakufahamu ndio mana nikaamua kukuleta sehemu kama hii”
Jackline alizungumza maneno yaliyo muacha Agnes mdomo wazi kwani hakujua ni jinsi gani Jackline aliweza kumfahamu yeye pamoja na mipano yake yote aliyo kuwa akiifanya.
 
 ***
Giza kila lilivyo zidi kwenda ndivyo  jinsi Fetty na wezake walivyo zidi kuendelea kutafuta sehemu alipo Agnes, kila mmoja alijitahidi kuchunguza kwa umakini katika eneo la mto huo wenye maje mengi yaendayo kwa kasi.
 
Wakiwa katika msako, kwa mbali wakasikia milio ya mbwa wanaokuja katika eneo walipo.
“Kuweni makini”
Wote kwa pamoja wakaingia msituni na kujibanza kwenye miti kutazama ni kina nani wana kuja katika enoo hilo. Mianga ya tochi nyingi ikaanza kuonekana kwa mbali, ikitokea usawa wa mto huo.
“Ni wanajeshi”
Anna alizungumza huku bunduki yake akiwa ameishika vizuri na kuielekezea sehemu ambapo wanatokea wanajeshi hao, wanao endelea kuwatafuta wasichana wawili kwa udi na uvumba. Msako huo uliundwa na majeshi ya Marekana pamoja na majeshi ya Riussia. Kila watu walina maumivu kwa upande wao haswa Wamarekani.
 
Wakafanikiwa kufika kwenye sehemu walipo fika Agnes na Jackline. Wakasimama katika eneo hilo huku wakiendelea kuchunguza eneo hilo kwa umakini wa hali ya juu.
“Hapa ndipo walipo kuwa, inaoenekana wapo ndani ya huu msitu”
Mtaalamu mmoja wa kuchunguza mambo ya kitaalamu alizunungumza huku akishika udongo wa eneo walipo kuwa Jackline pamoja na Agnes.
“Wapo kumi na tano”
Fetty alizungumza kila mmoja akiwa na kifaa chake cha mawasiliano masikioni mwake, aliweza kuisiskia  sauti hiyo iliyo kuwa ikizungumzwa na kiongozi wao wa msafara.
“Tuwafanyaje mkuu?”
Jamaa mmoja aliuliza, huku bunduki yake ikiwa wameielekeza walipo wanajeshi hao
“Ngojeni kwanza, musifanye chocho”
“Ila sister, inaoenekana wameingia kwenye mission moja na sisi”
 
“Sawa, tuwaache ache kwanza, tunaweza kuwaona wapo wachachche kumbe kuna wengine”
“Ila Fetty siku hizi umekuwa mzito sana, tazama jisni wanavyo tizama tizama huku, wasije kutuona”
“Cheki wanavaa miwani za usiku tutakwisha”
Jamaa mmoja alizungumza, bila hata kusubiri amri ya Fetty, akaanza kufyatua risasi, zilizo anza kuwapeleka baadhi ya wanajeshi chini. Kitendo hicho kikawafanya baadhi ya wanajeshi kutawanyika na kujificha kwenye majabali, makubwa na kuanza kujibu mashambulizi hayo. Kazi ikawa ni moja tu, kuhakikisha wanawazidi wanajeshi hao, walio jipendekeza katika kazi yao.
“Tunahitaji msaada, narudia tena tunahitaji msaada”
Mwanajeshi mmoja alipiga simu makao makuu, kuomba msaada wa wanajeshi wengine kwani tayari wanajeshi wao kama saba wamesha iaga dunia.
 
“Tumekupata”
Alipokea jibu mmoja kutoka, makao makuu. Wakaendelea kujibu mashambulizi ya watu hao ambao wamewavamia na hawakujua niwatu wangapi. Hali katika eneo la mto ikazidi kuwa mbaya zaidi milio ya bunduki, ilizidi kurindima kila kona.
“Helcoptar…..!!!”
Anna alishangaa baada ya kuona helcoptar zipatazo sita za jeshi la marekani zikifika katika eneo hilo, huku wajeshi wengi wakishuka kwenye helcoptar hizo zilizopo hewani, kwa kutumia kamba ndefu hadi chini.
‘Tunakufa leo’
Halima alijisemea kimoyo moyo huku akiendelea kuftyatua risasi nyingi kuelekea walipo wanajeshi hao.

==> ITAENDELEA

Post a Comment

0 Comments