Header Ads Widget

Serikali kufuta utitiri wa kodi kwenye viwanda

Makamu wa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema serikali inajipanga kuondoa utitiri wa kodi mbalimbali zinatozwa kwenye viwanda kama hatua ya kuviwezesha viwanda vingi nchini  kuongeza uzalishaji na kutoa ajira nyingi kwa watanzania.

Samia ametoa kauli hiyo jana Jijini Arusha baada ya kutembelea kiwanda cha kutengeneza mafuta ya kupikia cha Mount Meru Millers ili kujua changamoto zinazokikabili kiwanda hicho ili Serikali iweze kuzifanyia kazi katika kuleta unafuu kwenye uzalishaji wa mafuta ya kupikia nchini.

Alisema mlolongo wa kodi zinazotozwa kwa wamiliki wa viwanda hazina uratibu mzuri hivyo mkakati ya Serikali wa awamu ya Tano inataka kuweka utaratibu mzuri wa ulipaji wa kodi hizo ikiwemo kuondoa kodi ambazo ni kero kwenye viwanda.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Mount Meru Millers Atul Mittal alisema kama Serikali itafuta au kuondoa utitiri wa kodi wanazotozwa kwenye viwanda hivyo watakuwa na uwezo wa kuongeza maradufu uzalishaji na kutoa ajira nyingi kwa Watanzania.

Alisema kwa sasa Kampuni hiyo inafanya kazi kwenye nchi 10 barani Afrika na kwa Tanzania pekee imeajiri wafanyakazi zaidi ya 1000 ambao wanafanyakazi katika maeneo mbalimbali nchini.

Post a Comment

0 Comments