Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimesema endapo vyama vya siasa vitaendelea kunyimwa fursa ya kuwa na uwanja mpana wa kuzungumzia siasa wananchi wasitegemee kunufaika na uwepo wa vyama vingi ikiwa ni pamoja na kuhimiza maendeleo kupitia sauti za wanasiasa.
Kauli hiyo imetolewa na Mjumbe wa kamati kuu wa chama cha maendeleo na demokrasia na waziri mkuu wa zamani, Fedrick Sumaye wakati akifungua mkutano wa ndani wa chama hicho katika wilaya ya Masasi mkoani Mtwara huku akisisitiza dhana ya vyama vingi sio uadui ni mapambano dhidi ya hoja na itikadi.
“Timu zinapocheza timu moja ukaiwekea mawe ili ijikwae hii nyingine kazi yake ni kufunga magoli, kwahiyo vyama vingi vya siasa vitakuwa havina maana kama vyama havipewi uwanja ulio sawa,” alisema.
“Kwa sasa hivi katika Tanzania hakuna uwanja ulio sawa, uwanja bado haujawa sawa na hivyo tunadai tunataka tupewe uwanja ulio sawa ili Simba na Yanga wacheze,” alisema Sumaye
0 Comments
on