Mashabiki wa muziki jijini Kampala, Uganda, wamesikitishwa na taarifa kuwa show ya Wizkid iliyokuwa imepangwa kufanyika Jumamosi hii haitokuwepo tena licha ya maandalizi makubwa yaliyokuwa yamefanyika tayari.



Waandaji wa show iliyokuwa imepewa jina ‘6 Years of Startimes; Wizkid Live in Kampala’, wamedai kuwa staa huyo wa Nigeria alishindwa kusafiri na ndege kutoka Marekani usiku wa Alhamis hii kutokana na sababu ambazo zilikuwa juu ya uwezo wake.
15043399_639920036186278_1155985474146271232_n
Waandaji hao ambao ni Face TV, wamewaomba radhi mashabiki na wadhamini wa show hiyo kufuatia hatua hiyo. Show hiyo ilikuwa imepangwa kufanyika kwenye uwanja wa Lugogo Cricket.
cymn4gnwgaapm3k
Wamedai kuwa wanaendelea kuwasiliana na Wizkid ili kupanga tarehe mpya ya show hiyo.