Jana Rais Magufuli alitengua uteuzi wa Nape Nnauye na nafasi yake akapewa Dr. Mwakyembe.
Baadaye Nape Nnauye alitoa taarifa kuwa atazungumza na waandishi wa habari lakini Meneja wa Hotel ambayo mkutano ulitakiwa ufanyike alisema ameagizwa kuwaambia waandishi watawanyike na hakutakuwa na mkutano.
Nape alilazimika kuzungumza akiwa juu ya gari lake.Hata hivyo, polisi waliingilia kati
Leo asubuhi kupitia ukurasa wake wa twitter, ametoa ujumbe kwa wanahabari nchini ambapo ameandika: "Wanahabari mme GUSA sana moyo wangu!Sikujua kama mnanipenda na kunithamini kiasi KILE!Nawashukuru SANA kwa kujitolea kwenu!Nawapenda SANA!"
0 Comments
on