Tanzania ni moja kati ya nchi zenye amani na uhuru mkubwa kwa kuruhusu raia wake kufanya vitu vingi lakini leo March 31 2017 naomba nikusogezee sheria sita za nchi ya Korea Kaskazini ambapo kama zikiletwa Tanzania itakuwa ngumu watu kuzitekeleza kutokana na utaratibu ambao tumezoea.
1: Style ya kunyoa nywele inachaguliwa na serikali
Hiki kinaweza kuwa ni kitu cha kushangaza sana lakini ni kweli mwaka 2013 serikali ya Korea Kaskazini ilianzisha sheria ambayo inaipa mamlaka ya kuchagulia raia wake Style za nywele ambapo 18 kwa wanawake na 10 kwa wanaume cha kushangaza zaidi style ya nywele ya Rais wa nchi hiyo Kim Jung Un haipo kwenye list iliyotolewa.
2: Serikali huchagua watu maalum wa kuishi ndani ya mji Mkuu.
Korea Kaskazini ni watu maalum waliochaguliwa na serikali ndio wanaruhusiwa kuishi ndani ya mji mkuu wa nchi hiyo, ni kosa kisheria kwa mtu kuingia mjini Pyongyang bila kibali maalum cha kuingia katika mji huo.Watu wenye mafanikio na wenye utii kwa serikali ndo huruhusiwa kuishi katika mji mkuu.
3: Ni lazima watu kupiga kura.
Kwa kawaida kupiga kura ni jambo la hiari nchi zote duniani lakini ukiwa Korea Kaskazini ni lazima upige kura, nchi hiyo hufanya uchaguzi kila baada ya miaka mitano lakini cha kushangaza hakuna mgombea aliyewahi kujitokeza kushindana na Kim kwenye uchaguzi mkuu.
4: Ni lazima kuangalia TV ya Taifa.
Wananchi wa Korea Kaskazini huruhusiwa kuangalia channel tatu pekee ni kosa la kisheria kuangalia program za Tv kutoka nchi zingine hasa Marekani na ni lazima wananchi kuangalia Televisheni ya Taifa kujua kinachoendelea nchini mwao.
5: Wananchi hawaruhusiwi kumiliki bibilia.
Ukiwa Korea Kaskazini ni kosa kisheria kumiliki bibilia au kuamini katika ukristo, serikali ya nchi hiyo inaamini kwamba ukristo ni dini ya nchi za magharibi hivyo serikali ndio taasisi inayotakiwa kuabudiwa na wananchi wa nchi hiyo.
6: Ukitoroka jela wanaoadhibiwa ni familia yako.
Ukitoroka jela Korea Kaskazini wanaoadhibiwa ni familia yako mpaka kizazi cha tatu yaani kuanzia wewe,watoto utakaowazaa na wajukuu zako, sheria hii iliwekwa ili kuzuia watu kutoroka jela licha ya kuwa ilipingwa vikali na umoja wa kimataifa (UN).
0 Comments
on