Header Ads Widget

SORRY MADAM -Sehemu ya 68 & 69 (Destination of my enemies)


MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWAILIPOISHIA
ILIPOISHIA



Macho ya Eddy, Sa Yoo, Shamsa na Madam Mery wakawashuhudia Phidaya na Rahab wakiingia kwenye moja ya gari la kifahari huku nyuma yao akiwepo dokta Ranjiti.
“RANJITIIIIIIIIIIIIIIIIIII…………………….”
Eddy aliita kwa sauti kubwa na kumfanya dokta Ranjiti kutazama sehemu sauti hiyo inapo tokea, kwa haraka aliweza kuotambua sauti hiyo ni ya Eddy, ila sura ni tofauti kabisa, ila macho yake yalipo muona Madam Mery akiwa nyuma ya mtu huyo akagundua kwamba kila kitu kimeharibika. Kwa kiwewe dokta Ranjiti akajikuta akifyatua risasi kadhaa kuelekea anapotokea Eddy na kusababisha watu kuanza kukimbia kimbia ovyo kuyaokoa maisha yao.

ENDELEA
Dokta Ranjiti hakuhitaji kupoteza muda au kuangalia risasi zake zimemdhuru nani kwa haraka akaingia ndani ya gari na kumuamuru dereva wake waondoke kwa kasi katika eneo hilo. Risasi alizo zifyatua dokta Ranjiti kwa muda mchache ulio pita kwa bahati mbaya ziliwapata raia wawili ambao walikuwa wakikatiza mbele ya Eddy. Eddy akajairibu kulifukuzia gari hilo kwa miguu ila mbio zake hazikuweza kusaidia chochote mbele ya mwendo kasi wa gari hilo. Madam Mery, Sa Yoon a Shamsa wakafika sehemu alipo simama Eddy anaye hema kwa hasira.
“Sasa inakuwaje?”
Sa Yoo aliuliza huku macho yakiwa yamemtoka asijue ni nini afanye kwa wakati huo. Kila mmoja wao hakujua afanye nini ubaya ni kwamba wote ni wageni katika nchi ya Misri.
                                                                                                    ***
“Ranjiti kwa nini unatufanyia hivi lakini?”
Phidaya alizungumza huku machozi yakimwagika.
“Nyamaza wewe, unahisi  unaweza kunikimbia mimi, pumbavu sana wewe”
Muda wote huo, Rahab alikaa kimya asizungumze kitu chochote akilini mwake akipanga ni kitu gani anacho weza kukifanya kuyaokoa maisha yao. Hakuhitaji kuonyesha uwezo wake kwa wakati huo, alihitaji waweze kufika katika eneo ambalo dokta Ranjiti alikusudia kuweza kufika ili aweze kufanya atakacho weza kukifanya kwa wakati huo.
Safari yao ikachukua takribani dakika arobaini, wakafanikiwa kufika kwenye moja ya gorofa refu kwenda juu, ambalo kwa haraka haraka linaonekana ni gorofa kuu kuu(limechakaa). Wakaingia kwenye ndani, dokta Ranjiti akapolewa na kikundi cha vijana wenye silaha mikononi mwao, huku sura zao zikiwa zimefunikwa na vitambaa vyeusi huku ni sehemu ya macho yao tu ndio inayo onekana. Wakamtoa Phidaya kwenye gari pamoja na Rahab, kila mmoja akapelekwa upande wake jambo ambalo lilimchanganya sana Rahab. 
Rahab akaingizwa kwenye chumba kimoja chenye kiti kimoja cha chuma pamoja na meza moja iliyo tengenezwa kwa chuma. Akakalishwa kwa nguvu kwenye kiti hicho, akafungwa miguu na mikono yake kwenye kiti hicho. Lugha ya kiarabu wanayo zungumza vijana hao wawili walio muingiza ndani ya chumba hicho, ikazidi kumtatiza Rahab, hata wazo la kujiokoa likapotea kichwani mwake. 
Vija hao wakatoka ndani ya chumba hicho chenye mlango wa chumba, na kuufunga kwa nje. Vijana wawili wakabaki nje ya mlango huo kwa ajili ya kuimarisha ulinzi.
    Phidaya akaingizwa kwenye moja ya chumba, ambacho kinakitanda kikubwa. Akarushwa kitandani na vijana walio muingiza humo ndani wakatoka na kumuacha dokta Ranjiti peke yake ndani ya chumba hicho.
“Hivi wewe ni mjanja kuliko mimi, si ndio……?”
Dokta Ranjiti alizungumza huku bastola yake akiwa ameishika mkononi, Phidaya hakujibu kitu chochote zaidi ya kutetemeka mwili mzima na kumwagikwa na machozi mengi.
“Umeisumbua akili yangu, umeusumbua moyo wangu. Nashindwa kufanya vitu vya maana kwa ajili yako wewe”
Dokta Ranjiti alizungumza kwa hasira huku macho yake yakimtazama Phidaya aliye zidi kutetemeka na kulia kwa woga.
“Nimelimisi sana penzi lako”
Dokta Ranjiti alizungumza huku akianza kuvua nguo zake moja baada ya nyingine. Alipo bakiwa na nguo ya ndani akapanda kitandani na kuanza kumsogelea Phidaya taratibu huku bastola yake akiwa nayo mkononi mwake.
                                                                                                         ***
   Eddy na wezake wakajikuta wakirudi kwenye chumba anacho lala Shamsa na Sa Yoo, kila mmoja alijikuta akiwa mwingi wa mawazo, hususani Eddy, alijihisi kichwa kitampasuka kwa kuwaza. Simu ya mezani ikawatoa wote kwenye dibwi la mawazo. Kila mmoja akaitazama simu hiyo inavyo ita. Kwa haraka Sa Yoo akasimama na kwenda kuipokea simu hiyo.
“Haloo”
Sauti ya kiume ilisikika upande wa pili wa simu, Sa Yoo akajikuta akipata kigugumizi kuijibu sauti hiyo. Eddy kwa akili ya haraka akagundua kigugumizi cha Sa Yoo kina jambo fulani ambalo Sa Yoo anashindwa kulijibu. Eddy akanyanyuka kwa haraka na kumpokonya simu Sa Yoo na kuzungumza na aliye piga simu hiyo.
“Nani?”
Eddy aliuliza kwa sauti yenye msisitizo mkubwa. Mpiga simu wa upande wa pili akajikuta akikaa kimya kwa muda asijubu kitu cha aina yoyote. 
“Halooo”
Eddy alizungumza tena kwa msisitizo.
“Samahani nahisi nimekosea namba”
Mtu huyo mwenye sauti ya kiume alizungumza na kukata simu. Eddy taratibu akaurudisha mkonga wa simu kwenye sehemu husika kisha akarudi kwenye sofa alilo kuwa amekaa.
  Hadi inatimu majira ya saa tatu kasoro usiku hapakuwa na jibu  lolote walilo weza kulipata juu ya kutekwa kwa Phidaya. Hata polisi ambao walianza upelelezi wao hawakuweza kumpata mualifu wala hawakujua ni wapi muhalifu huyo alipo.
“Kukiwa na chochote, mutanifahamisha, naeleka chumbani kwangu”
Eddy alizungumza kwa sauti ya unyonge huku taratibu akinyanyuka na kutoka katika chumba walipo Shamsa, Madam Mery na Sa Yoo. Kila mmoja alimtazama Eddy akitoka katika chumba hicho.
“Mutakula nini?”
Madam Mery alizungumza huku akiwaangali Shamsa na Sa Yoo.
“Mimi sijisikii njaa”
Shamsa alizungumza huku akinyanyuka na kueleka katika chumba cha Eddy na kuwaacha Sa Yoo, na madam Mery alio amua kushuka chini kabisa ya gorofa la hoteli hiyo kwenye mgahawa mkubwa kwa ajili ya wageni walio fika kwenye hoteli hiyo.
Shamsa akagonga kwenye chumba cha Eddy mara kadhaa, baada ya kuona mlango haufunguliwi, kaingia ndani na kumkuta Eddy akiwa amejilaza kwenye sofa pasipo kuwasha taa.
“Eddy”
“Mmmmmmm”
“Usiwaze sana”
Shamsa alizungumza kwa sauti ya unyonge huku taratibu akikaa sofa la pembeni ya sofa alilo lala Eddy.
“Ni lazima niwaze, sifahamu ni kitu gani kinacho endelea kwenye hii dunia”
“Kivipi?”
“Kila kitu ninacho kikusudia kukifanya kwenye maisha yangu naona kinakwenda kinyume na jinsi nilivyo taraji kiende”
Eddy alizungumza kwa sauti iliyo jaa huzuni na unyonge ndani yake huku machozi yakimlenga lenga.
“Eddy, tambua kwamba kila jambo hutokea kwa wakati wake. Kuna wakati wa kulia na kunawakati wa kucheka”
“Sawa Shamsa ila mimi naona ninalia kuliko huko kucheka. Tazama Junio mwangangu amefariki, mbaya ameuawa na dada yangu Manka. Mama amefariki, ameuliwa na baba yangu tena mzazi. Mke wangu ambaye nilikuwa ninajua amefariki leo hii namuaona yupo hai, basi nimchukue. Anatokea mtu anamteka ni nini nitafanya hapa duniani ili nitulie”
Maneno haya Eddy aliyazungumza huku machozi yakimwagika, taratibu Shamsa akanyanyuka kwenye sofa alilo kaa, akakinanyua kichwa cha Eddy na kukaa kwenye sofa hilo kisha akakaa na kukiweka kichwa cha Eddy kwenye mapaja yake yaliyo jazia kiasi.
“Eddy, jinsi unavyo umia wewe ndivyo name pina ndivyo ninavyo umia”
“Shamsa, hupaswi kuumia tena. Maisha yangu kwa sasa ninaona hayana thamani yoyote. Nitafanya chochote nitakacho agizwa ili kumuokoa mke wangu”
“Bado unathamani kubwa moyoni mwangu Eddy.”
Shamsa alizungumza huku mkono wake wa kulia akiupitisha pitisha kwenye kifua cha Eddy. Eddy hakuliweekea maanani jambo hilo, akili yake na mawazo yake yote yapo kwa mke wake ambaye hadi sasa hatambui ni wapi alipo. Shamsa akajikuta akizidi kuipeleka mikono yake yote miwili kwenye mwili wa Eddy, hadi akaifikisha kiuno cha Eddy na taratibu akaanza kufungua mkanda wa suruali.
                                                                                                                   ***
Dokta Ranjiti akaendelea na shuhuli ya kumuingilia Phidaya, pasipo ridhaa yake japo ni mke wake, aliye kuwa akiishi naye, ila kwa wakati huo Phidaya kumbukumbu zake hazikuwepo. Muda wote dokta Ranjiti anavyo muingilia Phidaya, aliendelea kulia hadi dokta Ranjiti alipo maliza.
“Aghaaaaaaaa”
Dokta Ranjiti alishusha pumzi huku akitoa miguno ya kumaliza mpambano wa ulazima alio ufanya kwa Phidaya. Kama kawaida yake dokta Ranjiti akajilaza pembani huku akihema kana kwamba amekimbia umbali wa mbio nyingi.
“Utamu wako mke wangu bado haujaondoka, bado tunda lako lina joto kali kama nilivyo liacha”
Dokta Ranjiti alizungumza maneno ambayo yalizidi kumchoma moyo Phidaya, na kuzidi kuipandisha hasira ya Phidaya iliyo jijenga mara baada ya kumbukumbu zake kumrejea”
“Hivi niambie mke wangu ni wapi ulipo kuwa?”
Phidaya hakujibu kitu chochote zaidi ya kukaa kimya.
“Ukikaa kimya sio swala muhimu, kwako. Ila nimetambua kwamba kamume kako ka zamani bado kapo hai. Kitu nitakacho kwenda kukifanya utasikia”
Dokta Ranjiti alizungumza huku akishuka kitandani na kuanza kuvaa nguo zake. Alipo maliza kuvaa akakaa tena kitandani kwa dharau.
“Huto toka hapa hadi nihakikishe Eddy ANAKUFA”
Phidaya alipo sikia kauli ya dokta Ranjiti, mapigo yake ya moyo yakaanza kumuenda mbio, woga ukazidi kumtawala maradufu na ilivyo kuwa wali.
“Tafadhali Ranjiti ninakuomba usimuue Eddy, kwa maana hajafanya kosa lolote baya kwako”
“Nikumuacha hai atafanya kosa ambalo litakuwa baya kwangu. Wewe ni wangu na hakuna ambaye atakutoa wewe mikononi mwangu”
Dokta Ranjiti baada ya kuyazungumza maneno hayo akanyanyuka kutoka kitandani na kutoka ndani ya chumba hicho na kumuacha Phidaya akiendelea kulia.
Dokta Ranjiti baada ya kutoka kwenye chumba alipo Phidaya moja kwa moja akaeleka kwenye chumba alipo shikiliwa Rahab.
“Mumempatia chakula?”
Dokta Ranjiti aliwauliza vijana wake kwa luhga ya kiarabu, alio wakuta nje ya chumba walipo muhifadhi Rahab.
“Ndio mkuu, ila anaonekana amekata chakula”
“Nifungulieni”
Dokta Ranjiti akafunguliwa mlango na kuingia ndani akamkuta Rahab hajakula chochote na wala hajafunguliwa jinsi alivyo kuwa amefungwa tangu mwanzoni, alipo ingizwa katika chumba hicho. Dokta Ranjiti akamtazama vizuri Rahab na kujikuta akistuka na kumsogelea vizuri usoni mwake. Kumbukumbu zake kwa haraka zikampelaka siku ya msiba wa Phidaya nchini Tanzania. Aliweza kumshudia akiletwa na msafara mkubwa na kuheshimiwa.
“Wewe si mke wa raisi Praygod”
Dokta Ranjiti alizungumza huku macho yakimtoka na kumuangalia vizuri Rahab, akaanza kumgeuza geuza Rahab sura yake. Jibu alilo kuwa nalo kichwani mwake ni sahihi kwani Rahab kweli ni mke wa raisi Praygod. 

Dokta Ranjiti akakaa kimya kwa muda kisha akatoka kwenye chumba hicho akiwa na wasiwasi mkubwa moyoni mwake japo ni jasiri ila kosa ambalo anahisi litayagharimu maisha yake ni kitendo cha kuweza kumteka  mke wa raisi. Japo kuwa haelewi ni kitu gani kinacho endelea ndani ya Tanzania.
“Nahitaji mumuachie huyu msichana”
“Kwa nini mkuu?”
“Huyu sina kazi naye. Hakikisheni kwamba munamuachia hapa na kumtelekeza huko mtaani”
Hapakuwa na kijana aliye weza kuipinga amri hiyo ya bosi wao dokta Rajiti, vijana hao wakaingia ndani ya chumba walipo Rahab. Wakamvunga macho yake kwa kitambaa cheusi kisha wakambeba juu juu na moja kwa moja wakempeka kwenye gari lao jeusi aina ya Toyota Land Cruser V8. Safari ikaaza kumpeleka kwenye mtaa mmoja ambao hauna watu wengi. 

Bila ya kupoteza muda wakafungua mlango wa gari  lao na kumsukumia Rahab pembezoni mwa barabara na akaangukia kwenye nyasi nyingi kisha wakaondoka kwa mwendo wa kasi pasipo kumfungua kamba na kitambaa walicho mfunga usoni  mwake. Rahab akaanza kujitahidi kujifungua kamba hizo kwa bahati nzuri akapita kijana wa kiume aliye amua kumsaidia Rahab na kumfungua kamba hizo pamoja na kitambaa alicho fungwa usoni mwake.
“Asante”
Rahab alizungumza huku akijipangusa pangusa majani yaliyoshikamana na nguo zake. Kutokana na kijana huyo kuzungumza kiarabu na Rahab haifahamu lugha hiyo ikamlazimu Rahab kumshukuru kwa vitendo kijana huyo ambaye naye pia alijibu kwa vitendo. Kwa bahati nzuri katika eneo hilo ambalo Rahab alitelekezwa, aliweza kulifahamu kwani ni moja ya maeneo ambayo hupita asubuhi anapo kimbia akichukua mazoezi ya viungo.
                                                                                               ***
Wasiwasi ukaanza kumtawala Raisi Praygod ambaye kila alipo itazama simu yake hapakuwa na simu yoyote ambayo imeingia kutoka kwa mke wake, ambaye walikubaliana baada ya kufika hotelini na kukutana na Eddy wawasiliane. Akaanza kuipiga namba ya simu ya mke wake Rahab, kwa bahati mbaya ikawa haipatikani jambo lililo zidi kukiumiza kichwa cheke. 

Masaa yakazidi kukatika pasipo Rahab kurudi nyumbani. Kwa haraka akakumbuka kwamba kuna namba ambayo mke wake aliweza kuwasiliana na watu ambao wanakwenda kuonana nao. Kwa haraka akaitazama kwenye simu yake na kuipiga, kwani Rahab alimpatia namba hiyo kipindi alipokuwa anaondoka eneo hilo.
Namba ya simu hiyo kwa bahati nzuri inaita, baada ya muda ikapokelewa, ila mtu aliye ipokea hakuzungumza chochote hata pale alipo jaribu kuzungumza neon Hallo
Sauti nzito ya kiume ilimuuliza kwa lugha ya Kiswahili kwamba yeye ni nani. Ikamlazimu dokta Ranjiti kuomba msamaha kwamba amekosea namba. Raisi Praygod alizungumza hivyo baada ya kumuona Rahab akiingia ndani, huku jasho likimwagika. Kwa haraka akakata simu na kwenda kumlaki mke wake.
“Phidaya ametekwa”
Rahab alizungumza huku akihema, akiwa amemkumbatia mume wake, kipenzi.
“Ametekwa………..?”
“Ndio ametekwa na mwanaume mmoja ambaye sina kumbukumbu naye. Ila alipo niona mimi akanikumbuka na kujikuta akiniachia mimi huru”
Rahab alizungumza huku akihema, hii ni kutokna na kukimbia kwa umbali mrefu.
“Huyo mtu ana asili gani?”
“Kivipi?”
“Namaanisha kwamba ni muafrika, mzungu au?”
“Ni muarabu”
Raisi Praygod alijikuta akibaki na mshangao mkubwa kwani hakujua ni nani aliye tekeleza agizo la Phidaya kutekwa.
“Au labda ndio huyo mume wake ambaye alitueleza?”
“Ndio sasa nimepata picha, itabidi tuhakikishe tunamuokoa Phidaya”
“Sasa unapakumbua sehemu alipo kuwa amewapeleka?”
“Hapana ila nitahakikisha kwamba tunamkomboa”
                                                                                                 ***
“Shamsa stop”
Eddy alisimama na kutoka mikononi mwa Shamsa ambaye alisha fanikiwa kuufungua mkanda wa suruali pamoja na kifungo cha suruali. 
“Kumbuka kwamba mimi ni baba yako”
“Hapana Eddy wewe si baba yangu. Mimi nimesha kuwa na nina hisia za kupenda kama wanawake wengine na siwezi kuendelea kuzidanganya hisia zangu kwamba wewe ni baba yangu wakati tayari nimesha weza kuonja mate yako.”
Shamsa alizungumza kwa kujiamini na kumfanya Eddy abaki akiwa ameduwaa asijue amjibu nini Shamsa.
                                                                                                                                                            SORRY MADAM (69) (Destination of my enemies)

Eddy hakuhitaji kuzungumza chochote zaidi ya kufunga kifungo cha suruali yake kisha akamalizia na mkanda, kisha akakaa kitandani huku akimtazama Shamsa kwa macho makali. Ukimya ukatawala kwa dakika kadhaa, hapakuwa na mtu aliye weza kuzungumza kitu chochote.
   Shamsa akashusha pumzi nyingi kisha akatoka ndani ya chumba cha Eddy moja kwa moja akaeleka kwenye baa iliyomo ndani ya hoteli hiyo. Akaagiza mzinga wa pombe kali na kuanza kuunywa kwa fujo japo hiyo ndio mara yake ya kwanza kuweza kunywa kilevi, ila amefanya hivyo ili mradi kupoteza mawazo ya kumuwazia Eddy.
‘Eddy ni lazima awe wako’
Shamsa aliisikia sauti ikimshauri kwa msisitizo kichwani mwake.
‘Una sifa za kuwa na Eddy, hakikisha kwamba anakuwa wakwako’
Sauti hiyo iliendelea kuzungumza jambo lililo zidi kumpa munkari Shamsa ya kunywa kwa fujo pombe hiyo hadi muudumu aliye muhudumi kwenye kaunta hiyo  ya kinywaji akabaki amemkodolea macho ya mshangao kwani kwa kipindi cha miaka minne tangu aanze kuifanya kazi hiyo hajawahi kumshuhudia mtu akiinywa pombe hiyo kali kwa fujo kama anavyo fanya binti huyo.
“Samahani dada”
Muhudumu huyo alizungumza huku akimtazama Shamsa usoni, Shamsa akamtazama muhudumu huyo kwa macho yaliyo jaa ulevi mwingi.
“Samahani ninaomba niuchukue huu mzinga, kwa maana pombe unayo itumia ni kali sana”
“Nimekulipa au sijakulipa?”
“Natambua hilo ila kwa jinsi unavyo zidi kuinywa hiyo pombe ni hatari kwa afya yako”
“Hembu niachi….e uu….puuzi wako”
Shamsa alizungumza huku akijaribu kuushusha mguu wake mmoja chini, kutoka kwenye kiti kirefu alicho kikalia, kila alivyo jaribu kuushusha mguu wake, ndivyo jinsi alivyo jikuta akishikwa na kizunguzungu kikali kilicho mpeleka chini na kumuangusha chini kama mzigo. Kishindo cha Shamsa kuanguuka kikawastusha hadi wateja wengine.
Sa Yoo naye macho yake aliweza kuyapeleka sehemu ilipo tokea kishindo hicho, katika kuangalia vizuri akamuona ni Shamsa akijikaza kaza kunyanyuka kutoka sehemu alipo anguka. Kwa haraka Sa Yoo akanyanyuka kutoka katika kiti alicho kaa na kwenda alipo Shamsa.
“Shamsa vipi?”
Sa Yoo alijikuta akimshangaa Shamsa kwa jinsi alivyo lewa, kwa msaada wa muhudumu mmoja wa kike wakasaidiana kumnyanyua Shamsa, na kuanza kumpeleka sehemu kulipo na lifti. Wakaingia wote watatu na kuelekea katika gorofani kilipo chumba cha Shamsa na Sa Yoo.
“Asante”
Sa Yoo alimshukuru muhudumu  huyo mara baada ya kumlaza Shamsa kitandani, huku akikoroma koroma tu pasipo kujitambua. Baada ya muhudumu huyo kutoka ndani ya chumba chao Sa Yoo kwa unyonge akaka pembeni ya kitanda, alicho lala Shamsa.
“EDDY NAKUPENDAAA..AA.AAAA”
Shamsa alizungumza maneno hayo huku akikoroma, kitendo kilicho mshangaza Sa Yoo, akajaribu kumtingisha Shamsa ila hakuitika kwa lolote. Simu ya mezani ikaita na kumfanya Sa Yoo, kusitisha zoezi la kumuamsha Shamsa akasimama na kwenda kuipokea simu hiyo, japo ni majira ya usiku ila aliamini kwamba simu hiyo inaweza kuwa na umuhimu mkubwa kwao.
                                                                                                                ***
“Basi itabidi kuweza kujaribu kuwasiliana na huyo binti ambaye alikuja kumuona bosi wake”
Raisi Praygod alizungumza huku akimtazama Rahab usoni. Rahab akajipapasa mifukoni mwake na kujikuta akiwa hana simu yake. 
“Vipi?”
“Simu yangu siioni”
“Chukua hii ya kwangu, na muda fulani niliipiga ile namba uliyo nipatia ila sikuweza kuzungumza alipokea mwanaume tofauti na ulivyo niambia kwamba mtu sahihi ni mwanamke”
“Hmebu naomba nijaribu kuipiga tena hiyo namba”
Rahab akaichukua simu ya mumewe na kuipiga namba, ambayo anazungumza na Sa Yoo. Kwa bahati nzuri namba hiyo ikaanza kuita na baada ya muda ikapokelewa.
“Haloo”
Rahab aluzungumza huku akiwa na shauku ya kuishikia sauti ya kike, ambayo ni sauti ya Sa Yoo.
“Haloo madam nilikuwa ninaishubiria simu yako kwa hamu kubwa”
Sa Yoo alizungumza huku akionekana kuwa na furaha kubwa moyoni mwake, japo hajawahi kuonana na Rahab
“Ohhoooo asante Mungu. Sasa sib ado upo hapo hotelini?”
“Ndio bado nipo”
“Basi asubuhi na mapema nitakuwepo hapo, hakikisha kwamba humuelezi mtu yoyote juu ya ujio wangu”
“Sawa, ila samahani bado sijakufahamu jina lako kwa maana tunazungumza tu?”
“Mimi ninaitwa Rahab”
“Rahab asante kwa kukufahamu”
“Haya usiku mwema”
Rahab akakata simu na kumkabidhi mume wake. Kwa mapenzi makubwa raisi Praygod akamsindikiza Rahab bafuni na kumuogesha, akamuandalia chakula cha kizuri ambacho mara nyingi Rahab ukipenda chakula hicho.
                                                                                                                ***
    Wanannchi wengi nchini Tanzania, walizidi kujikuta wakiingia katika hali ngumu ya maisha, ukiachilia mbali kupanda kwa uchumi na maisha kuwa magumu, bali hata matumizi mabovu ya madaraka yalizidi kuwaumiza. 

Kauli ya raisi Godwin ya wananchi wote kupiga kura ya Ndio ya kubadilisha mfuo wa kiserikali, kutoka katika mfumo wa raisi hadi kwenye mfumo ufalma. Kauli hiyo ilizidi kuzua mijadala kwenye sehemu nyingi ndani na nje ya Tanzania. Nchi kubwa zenye ngumu duniani, hususani na Marekani, ikaanza kutangaza vikwazo kwa raisi wa Tanzania Mzee Godwin, kwamba endapo mfumo wa kimadaraka utabadilika basi wanasitisha urafiki kati ya nchi hizi mbili.
    Swala hilo halikuweza kumtisha wa kumteteresha raisi Praygod. Alicho kiamini ni kwamba anahitaji kujitengenezea serikali yenye nguvu na yakuogopwa ndani na nje ya bara la Afrika. Siku iliyo pangwa kwa wananchi kuweza kupiga kura ya kubadilisha mfumo wa kiserikali. Hapakuwa na wananchi walio jitokeza kuweza kufanya hivyo, hata wale ambao walikuwa wakimuunga mkono raisi Godwin katika kipindi cha kampeni.
“Muheshimiwa kwa taarifa tulizo nazo, hakuna hata mwananchi mmoja aliye jitokeza kupiga kura”
Mshauri wa Mzee Godwin alimuambia, mara baada ya kupata taarifa hizo kutoka kwa mawakala walio weza kuwatuma katika vituo vya kupigia kura nchi nzima.
“Nini….??”
“Ndio hivyo mku”
Raisi Godwin alizungumza huku akinaynyuka kwenye kiti chake cha ufalme ambacho tayari kilisha endaliwa.
“Ndio hivyo muheshimiwa”
“Tuma vikosi vya polisi kuwatoa watu majumbani mwao na hakikisheni wananchi wote wanakwenda kupiga kura”
“Sawa mkuu, je endapo watakataa?”
“Watakao kataa wakamatwe na wawekwe rumande”
“Sawa mkuu”
Amri ikatolewa mara moja kwa makamanda wakuu wa polisi(RPC) wa mikoa yote juu ya amri ambayo raisi Godwin. Japo ni amri ya udikteka, ila polisi ikawadi kuweza kufanya walicho agizwa. Polisi wote wakaanza kupita nyumba moja baada ya nyingine kuwachukua wananchi kinguvu na kuwapeleka katika vituo vya kupigia kura. Kama kawaida wapo wananchi ambao waliweza kupingana na polisi, ila cha mtemakuni walikiona, wengine baada ya kipigo wao wenyewe waliweza kukubali kwenda na wengine walio kataa kabisa waliweza kupelekwa rumande kama agizo la riaisi Godwin lilivyo sema. 
Vituo vya televishion na redio ndani na nje ya Tanzania viliweza kurusha matangazo juu ya tukio hilo la kusikitisha, viongozi wa nchi jirani zinazo pakana na Tanzania walijikuta wakilaani kitendo hicho na kushangazwa sana, kwani wengi kati yao walihisi swala hilo lisinge fikia katika hatua ya wananchi kuweza kulazimishwa kwa nguvu.
                                                                                                                          ***
    Taarifa ya ukatili unao endelea ndani ya Tanzania, iliweza kumfikia Eddy majira ya asubu alipo weza kufungulia televishion, huku akilini mwake akiwa na lindi la mawazo kichwani mwake. Kwa jinsi wananchi walivyo kuwa wakipatia kipigo na polisi, kitu hicho kiliweza kumuumiza sana moyo wake. Akazidi kumchukia baba yake Mzee Godwin ambaye kwa sasa ndio anashikilia madaraka ya nchi ya Tanzania. Eddy akajikuta akimwagikwa na machozi, taratibu akanyanyua rimoti ya tv na kuizima, hakuhitaji kuendelea kuiangalia taarifa hiyo ambayo ilizidi kumachanganya.
Tangu nguo alizi zivaa jana hakuweza kuzibadilisha kutokana na kuwa katika hali ya msongamano wa mawazo. Akajizoa zoa kwenye sofa alilo kalia na kunyanyuka, kwa lengo la kwenda bafuni, kabla hajaufikia mlango wa kuingilia bafuni, mlango ukagongwa. Taratibu akauendelea mlango huo na kuufungua. Akamkuta Sa Yoo akiwa amesimama, huku sura yake ikiwa na tabasamu.
“Za asubuhi Eddy”
“Salama vipi?”
“Kuna yule mwanamke ambaye nilikuwa ninazungumza naye kwenye simu aliye tufahamisha kuwa yupo na madam Phidaya amekuja”
“Kweli?”
“Ndio”
“Yupo wapi?”
“Nifwate”
Eddy hata swala la kuoga likamuondoka kichwani mwake kwa haraka akaanza kumfwata Sa Yoo kwa nyuma, wakaingia kwenye lifti na kushuka hadi gorofa ya chini kabisa, wakaanza kutembea kueleka kwenye sehemu yenye maegesho ya magari. Wakalifikia gari ambalo amekuja nalo Rahab, ambaye alipo muona Sa Yoo, akija na mwanaume huyo, akafungua kioo cha gari.
“Munaweza kuingia ndani ya gari”
Kitendo cha Eddy kumuona Rahab, akahisi miguu yake ikikosa nguvu kabisa, kwa maana anamtambua vizuri Rahab.  
“Kaka unaweza kuingia tu ndani ya gari”
Rahab alizungumza hivyo pasipo kugundua kwamba mtu anaye zungumza naye ni Eddy hii ni kutoka na Eddy kuibadilisha sura yake. Eddy pasipo kuwa na ubishi akaingia ndani ya gari mara baada ya Sa Yoo kuingia ndani ya gari hilo.
“Itakuwa ni vizuri kama tunaweza kwenda kuzungumza mazungumzo hayo nyumbani kwangu”
Rahab alizungumza huku akimtazama Eddy aliye kaa siti ya nyuma. Eddy akatingisha kichwa chake, hakuhitaji kuzungumza chochote kohofia sauti yake kuweza kutambulika. 
“Sa Yoo mwenzako anaonekana kuwa yupo serious eheee?”
Rahab alimuuliza Sa Yoo huku akigeuza gari lake na kuanza kutoka katika eneo hilo la hoteli.
“Anamawazo tu ya mk…..madam kutekwa”
Ilibi akili ya Shamsa kuweza kufanya kazi kwa haraka, kwa maana anaelewa ni hali gani ambayo anayo Eddy kwa wakati huu, na hata angesema kwamba huyu ndio mume wa Phidaya ingemshangaza hata Rahab kwa maana anavyo dai anamfahamu Eddy vizuri.
     Safari yao haikuchukua dakika nyingi wakawa wamefanikiwa kuweza kufika katika nyumba anayo ishi Shamsa na mume wake ambaye ni Raisi Praygod. Kwa pamoja wakashuka kwenye gari na kingia ndani. Eddy alipo muona raisi Praygod akiwa amekaa kwenye sofa, akiitazama taarifa inayo husiana na Tanzania.
“Honey tumerejea”
Raisi Praygod alipo waona akanyanyuka na kuwakaribisha Sa Yoo na Eddy pasipo kuweza kumtambua mara mojo kwa maana sura ambayo Eddy ametengenezewa ni sura ambayo si rahisi kwa mtu kuweza kuifahamu kwamba ni sura bandia.
“Kama nilivyo weza kukueleza Sa Yoo. Phidaya bado anashikiliwa na mume wake na inavyo onekana wanaweza kuondoka ndani ya nchi hii muda wowote na sinto fahamu ni wapi watakapo elekea”
Eddy akataka kuzungumza kitu ila akanyamaza kidogo, kitu kingine ambacho kinaweza kumsaidia Eddy kuto kujilikana kirahisi ni jinsi mwili wake ulivyo weza kujengeka kimazoezi. Watu walio weza kumuona kipindi ni waziri wa ulinzi ni ngumu kuweza kumgundua kwa haraka na ndivyo ilivyo kwa Rahab na mumewe dokta Ranjiti.
“Sasa unapafahamu hiyo sehemu gani ambayo waliweza kuwapeleka?”
“Kwa haraka haraka siwezi kupafahamu, ila nakumbua jengo hilo kwa maana tulivyo ingia niliweza kulitazama vizuri ila tulivyo toka sikuweza kuliona kutokana nilifunikwa sura”
“Huyo atakuwa ni dokta Ranjiti ndio aliye mteka madam Phidaya”
Sa Yoo alizungumza huku akiwa ameyatoa macho yake makubwa kiasi kabla mtu yoyote hajazungumza,
simu ya raisi Praygod ilita na kuwafanya watu wote kukaa kimya Raisi Praygod akainyanyua simu yake aliyo kuwa ameiweka mezani na kuitazama namba ambayo inapiga, namba hiyo ni namba ngeni kwenye simu yake na ni namba ya simu ya mkononi. Taratibu dokta Ranjiti akaminya kitufe cha kupokela na kuiweka simu yake kwenye sikio la upande wa kulia, kuisikilizia simu hiyo.
                                                                                                         ***
Kipindi Rahab alipo kuwa anahatolewa katika jengo la himaya ya dokta Ranjiti, kijana wake mmoja aliweza kumchomolea simu Rahab pasipo yeye mwenye kutambua. Walipo kamilisha zoezi la kumtupa Rahab katika sehemu waliyo ona kwao inafaa kumtupa wakarejea katika ngome yao. Akaanza kuipekua semu ya Rahab kuanzia kwenye majina yaliyo wekwa ndani ya simu hiyo hadi picha. 

Aliweza kuona picha nyingi za Phidaya akiwa amepiga na Rahab pamoja na mwanaume mmoja ambaye hakuweza kumfahamu. Kutoka usiku huo bosi wake aliendelea kuburudika na mke wake aliye kuwa akimtafuta kwa muda mrefu, kijana huyo ajulikanaye kwa jila la Adrus, aliweza kusubiria hadi kulipo pambazuka na kwenda moja kwa moja kwenye ofisi ndogo ya dokta Ranjiti, iliyomo ndani ya jengo hilo. Kwa bahati nzuri akamkuta akiwa yupo ndani ya ofisi hiyo, wakasalimiana kwa kiarabu kisha akakaribisha na kukaa kwenye kiti kilichopo mbele ya meza ya dokta Ranjiti.
“Bosi kuna hii simu niliweza kumchomolea yule binti tuliye muachi huru jana”
Adrus aluzingumza huku akimkabidhi dokta Ranjiti simu hiyo, ambayo taratibu akaanza kuipekua kama alivyo fanya Adrus, swali la kujiuliza kwamba Rahab alikuwa ni mke wa raisi Praygod, liliweza kupata uhakika baada ya kuona picha za raisi Praygod akiwa amepiga na Rahab pamoja na Phidaya. Katika kuchunguza chunguza akakuta namba iliyo andikwa(Husband)
“Hii ni namba ya mume wake ambaye ni raisi wa nchi ya Tanzania”
Dokta Ranjiti alizungumza huku akimuonyesha Adrus namba hiyo
“Bosi unaonaje ukamtumia mke wako kuweza kujivunia pesa?”
“Kivipi?”
“Unaweza kumuambia kwamba ili kumpata rafiki yao, basi watoe kiasi cha pesa ambacho utakihitaji kisha tunawachezea pata potea”
“Hivi unahisi kwamba mpango wako unaweza kuzaa matunda katika hilo?”
“Kama mtu ni raisi ninaamini kwamba kila kitu kitakwenda salama na tutajipatia pesa nyingi za kupunguza machongu ya kuweza kumtafuta mke wako kwa kipindi chote hicho”
Dokta Ranjiti akafikiria kwa dakika kadhaa, mpango alio shauriwa na kijana wake. Akaona kidogo ni mpango wenye nguvu. Taratibu akaanza kuinakili namba ya raisi Praygod kwenye simu yake, alipo maliza, akaitazama kwa sekunde kadhaa kisha akaipiga. Simu hiyo ikaanza kuita kwa muda kisha ikapokelewa.
“Halooo, ninaamini kwamba wewe ni raisi Praygod?”
“Ndio ni mimi”
Sauti hiyo ilisikika kutokea upande wa pili wa simu
“Unazungumza na Ranjiti, ninaamini kwamba munamtafuta Phidaya, ambaye yupo mikononi mwangu”
“Ndi………”
Mikwaruzano ikasikia upande wa pili wa simu na kumfanya dokta Ranjiti kusikilizia vizuri
                                                                                                                ***
Eddy alipo isikia sauti ya Ranjiti kwenye simu ya raisi Praygod, akasimama kwa haraka kwenye sofa alilo kaa, kisha akaikwapua simu kutoa mkononi mwa raisi Praygod na wafanya watu wote wamshangae.
“RANJITI, SIKU NIKUKITIA MIKONONI MWANGU NITAHAKIKISHA KWAMBA KICHWA CHAKO KINAKUWA MALI YANGU”
“Wee…..weee si Eddy”
Dokta Ranjiti alizungumza kwa wasiwasi mkubwa
“NDIO MIMI NI EDDY, MUME HALALI WA PHIDAYA”
Eddy alizungumza kwa sauti yanye msisitizo na kuwafanya Rahab na raisi Praygod wote kushtuka na kujikuta wakinyanyuka kwenye sofa na kumshangaa, kwani kati yao hakuna aliye weza kumgundua kwamba kijana huyo ni Eddy, ambaye alikuwa ni waziri wa ulinzi katika serikali yao na ni adui wa mapenzi wa raisi Praygoda, kwani aliweza kugundua Eddy alishirikia tendo la ndoa na mke wake kipenzi Rahab.

              ==>ITAENDELEA...

Jiunge na djadam64.com sasa



Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter's  na Instagram  ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka djadam64.com

Post a Comment

0 Comments