Header Ads Widget

RIWAYA: Mwanafunzi Mchawi - (A Wizard Student) - Sehemu ya 27





MTUNZI: ENEA FAIDY
...... MR ALOYCE alibaki kimya akiwa ametulia kimya kama vile amegandishwa na gundi ngumu. Haja ndogo ilipita taratibu katikati ya mapaja yake na kushuka chini ardhini. 

Alitamani ardhi ipasuke ili walau akajifiche chini ya ardhi kuliko kuendelea kushuhudia tukio lililokuwa linaendelea kwa wakati ule. 

Akili ilisimama, mwili ulinyong'onyea kwani hakuwa na lolote la kuweza kufikikiria kwa wakati ule. "Nimekamatika kwenye mtego" ndilo wazo pekee lililomjia akilini mwake.

Chatu yule aliendelea kujiviringisha kwa madaha na mbwembwe nyingi mwilini mwa Mr Aloyce na kumfanya mwanaume yule ajihisi mfu aliyebakisha roho yake tu kabla ya mazishi. 

"Nisaidie Mungu wangu" Mr Aloyce alisali kimoyo moyo akiamini kwamba huenda Mungu atasikia maombi yake na kumkumkumbuka katika Mateso yake. Machozi hayakumtoka hata chembe kwani hofu ilimzidia mpaka chozi lilimkauka.

Akiwa katika hali hiyo ngumu isiyoelezeka Mr Alloyce hakuona mtu yeyote wala dalili ya kiumbe chochote katika eneo lile. Ghafla upepo mkali ukapuliza eneo lile, ulikuwa kama kimbunga kinachoweza kuleta maafa kwa makazi ya watu.

Mr Aloyce alijishangaa sana kuona mwili wake ukiwa mwepesi sana tena umejiachia kupita kiasi. Moyo wake ukafurahi na akatumia nafasi hiyo kujitazama mwilini mwake, akagundua yule chatu hayupo tena mwilini mwake Bali amesogea pembeni kidogo na kujituliza kama gogo.

Macho yalimtoka kama njugu akimtazama yule Chatu, ghafla akapigwa na mshangao wa ajabu baada yule chatu kubadilika umbile na kuwa na umbo la mtu. Mr Alloyce akamkazia macho MTU yule aliyetokana na chatu.

 Hakuamini macho yake pale alipogundua mtu yule alikuwa mkewe, Aloyce alitetemeka sana. Ndipo mwanamke yule alipoachia kicheko kikali sana huku akimsogelea Mr Aloyce. "Nilikukumbuka sana mume wangu.. Ila nasikitika unaniogopa" alisema mwanamke yule mwenye sura na umbile la mama Eddy. Mr Aloyce alitetemeka sana, akapiga hatua za kinyumenyume kumkwepa mwanamke yule.
 
"Mume wangu! Mbona unaniogopa?" Alisema mwanamke yule.

Post a Comment

0 Comments