Mkali wa muziki anayefanya vizuri na wimbo ‘Salome’ Diamond Platnumz
Alhamisi hii siku moja kabla ya birthday ya mama watoto wake Zari,
ameonyesha nyumba ya familia aliyonunua Afrika Kusini.
Muimbaji huyo ambaye ni mmoja kati ya wasanii wachache wenye
mafanikio makubwa hapa nchini, hakuweka wazi nyumba hiyo imegharimu
kiasi gani kuinunua.
“Wanakazana kujisifu matajiri ilhali watoto zao wanaishi kwenye
Nyumba zakupanga. Halafu leo yule yule wanaemtukana kutwa kwenye
mitandao kuwa masikini, kajawa na shida, Kanunua nyumba kulekule kwao
ili watoto wao waishi maisha bora kama wanayoyatamani. Heri ya siku ya
Kuzaliwa Mama tee wangu. Nakupenda sana na unalifahamu hilo, natumai
umeipenda nyumba yetu hii mpya South Africa. Nasubiria kwa hamu
kusheherekea nawe siku yako hii kubwa kesho (leo) Zanzibar,” Diamond
aliandika instagram.
Muimbaji huo amevunja zile tetesi za kwamba huwenda hayupo sawa na
mama Tiffah baada ya mrembo huyo siku chache zilizopita kudai amekuta
hereni za mwanamke mwingine chumbani kwake.
0 Comments
on