BABA
mmoja mkazi wa Kijiji cha Maji ya Moto, Wilaya ya Arumeru mkoani hapa,
Wilfred Kivuyo amemuua mtoto wake baada ya kumchoma kisu tumboni, kwa
kosa la kufungulia redio kwa sauti ya juu.
Kabla
ya tukio hilo inadaiwa yalitokea mabishano ya kugombea kupunguza sauti
ya redio kati ya baba na mtoto, ambapo baba aliamua kumchoma kisu
tumboni mtoto wake na utumbo kutoka nje.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alisema, tukio hilo lilitokea
Oktoba 23, mwaka huu saa tatu usiku katika Kijiji cha Maji Moto na
kumtaja marehemu kuwa ni Abraham Wilfred (22), ambaye kabla ya mauti
alikuwa nyumbani akiendelea na shughuli zake huku akiwa amefungulia
redio.
Alisema
siku ya tukio mtuhumiwa huyo alifika nyumbani akiwa amelewa na kumkuta
mtoto wake amefungulia redio kwa sauti ya juu, ambapo alimtaka kupunguza
sauti hiyo lakini mtoto huyo aligoma.
“Baada
ya hapo mabishano na kutoelewana kulijitokeza baina yao wakaanza
kupigana, baba alipozidiwa nguvu na mtoto wake alichomoa kisu cha
kukunja kwenye mfuko wa suruali kisha akamchoma tumboni na kumsababisha
utumbo kutoka nje.
“Mara
baada ya tukio hilo mtoto huyo alichukuliwa na kukimbizwa katika
Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru kwa ajili ya matibabu, lakini hata hivyo
alifariki wakati madaktari wakiendelea kuokoa maisha yake,” alisema Kamanda Mkumbo.
Kamanda
Mkumbo alisema Jeshi la Polisi linaendelea kumsaka mtuhumiwa huyo
ambaye baada ya tukio alikimbia ili hatua zaidi za kisheria
zisichukuliwe dhidi yake
0 Comments
on