Kuna sababu nyingi sana zinazofanya WiFi unayorusha kutoka katika kifaa chako cha android kuwa slow sana. Moja ya sababu hizo ni uwezekano wa kifaa au mtu mmoja usiyemfahamu anatumia WiFi yako bila ya wewe kujua na akawa anakula data ya kutosha. Sasa leo tutaangalia jinsi ya kumkamata mwizi wa yako na kumfungia kabisa.
Nani anatumia WiFi yangu?
Kujua nani anatumia WiFi yako kitu cha kwanza ni kuhakikisha umejiunga katika WiFi husika. Kisha download app inayoitwa Fing kutoka katika Playstore au link hii hapa.Baada ya kuipakua na kuifungua utaona jina la network yako pamoja na kitufe cha refresh, bonyeza kitufe cha refresh ili uweze kupata majina ya vifaa vilivyoungwa katika mtandao wako.
Baada ya muda, refresh itamaliza na hapo utaona orodha ya vifaa vyote vilivyoungwa katika mtandao huo pamoja na icon ya kuonyesha kama ni PC au ni Simu.
Bonyeza moja ya vifaa hivyo ili kupata menu ya jinsi ya kukimudu kifaa husika, kama PING au Wake On LAN signals na pia unaweza ukaset muda gani vifaa hivyo vijiunge katika WiFi yako na muda gani visijiunge.
Jinsi ya Kublock?
Kama utaona kifaa kigeni katik orodha yako unaweza ukakiblock moja kwa moja kutumia mtandao wako. Fing itakuonyesha MAC Address ya kila kifaa kilichoungwa katika mtandao wako.Njia mbadala
Unaweza ukaend katika settings=>mobile networks=>tethering and portable hotspot na hapo utachagua WiFi Hotspot, orodha ya vifaa vilivyoungwa katika wifi yako vitaonekana hapo.Kisha bonyeza kwenye kifaa husika kisha chagua Forget na hicho kifaa kitaondoka katika orodha yako.
Njia nyingine rahisi ni kuhakikisha unabadili passwords za WiFi yako mara kwa mara ili kupunguza uwezekano wa watu kutumia WiFi yako bila ya wewe kufahamu.
0 Comments
on