Kijana huyo ambaye tayari ameshaonekana mara kadhaa katika baadhi ya video za mastaa wa muziki nchini, amemmwagia sifa malkia huyo wa filamu huku akishindwa kuweka wazi kama ni kweli anatoka naye kimapenzi au la!.
“Wema is a beautiful girl, sexy and every man’s dream, na mimi pia ni mvulana mzuri ambaye mwanamke yeyote angependa kuwa na mimi, akiwemo Wema mwenyewe,” Calisah alikiambia kipindi cha Enewz cha EATV. “Siwezi kusema moja kwa moja kwamba sisi ni wapenzi, lakini lakizima ujue kuwa Wema ni mzuri na mimi mzuri,”
Pia kijana huyo alidai kuwa hamtambui Idris Sultan na hakumbuki kama Tanzania imewahi kuwakilishwa na mtu anayeitwa Idriss katika mashindano ya Big Brother Afrika.
“Who? Idriss, kwani amewahi kuwa Big Brother? Which year?,” aliuliza kijana huyo.
Malkia huyo wa filamu toka aachane na mshindi huyo wa Big Brother Afrika 2014, hajaweka wazi mahusiano yake mapy
0 Comments
on