Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Salvador Antonio Valdes Mesa amewasili jana jioni katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kupokelewa na Mwenyeji wake Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Salvador Antonio Valdes Mesa atafanya ziara ya kikazi ya siku Tatu hapa nchini na lengo la ziara hiyo ni kuendeleza na kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Cuba katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu,afya, utamaduni,michezo,kilimo, nishati, teknolojia na kuangalia maeneo mapya ya uwekezaji.

 Tarehe 3/09/2016 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba atakutana na kufanya mazungumzo ya faragha na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli ikulu jijini Dar es salaam.

Makamu wa Rais huyo wa Jamhuri ya Cuba Salvador Antonio Valdes Mesa pia atakutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ikulu na baada ya mazungumzo hayo ya faradha viongozi hao watafanya mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili

Nchi nyingine ambazo Makamu wa Rais huyo wa Jamhuri ya Cuba anazitembelea ni Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo- DRC-,Botwana na Zimbabwe.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Salvador Antonio Valdes Mesa akiangalia ngoma za asili mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Saalaam ambapo atakuwa na ziara ya kikazi ya siku tatu hapa nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Salvador Antonio Valdes Mesa akiangalia moja ya kikundi kilichokuwa kinatumbuiza kwa matarumbeta mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Saalaam ambapo atakuwa na ziara ya kikazi ya siku tatu hapa nchini.