Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Projest Kahyoza amejitoa kusikiliza shauri linalowakabili
wakurugenzi wa kampuni ya Tiptop Connections ya jijini Dar es Salaam,
Hamis Shaaban maarufu Babu Tale na ndugu yake, Idd Shaaban.
Kahyoza alifikia uamuzi huo juzi, siku aliyopanga kutoa maelekezo
maalumu kwa wadaiwa hao. Hata hivyo, mlalamikaji Sheikh Hashim Mbonde
alimuomba ajitoe kwa madai kuwa hana imani naye.
Katika shauri hilo, Babu Tale na nduguye wanatakiwa kujieleza ni kwa
nini wasifungwe jela kwa kushindwa kutekeleza amri ya Mahakama hiyo.
Mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam ilimtaka Babu Tale amlipe Shekh
Hamis Mbonde, shilingi milioni 250 kwa kudaiwa kuvunja mkataba kati yake
na Sheikh Mbonde wa kuuza na kusambaza nakala za mawaidha (DVDs) bila
ridhaa ya sheikh huyo.
Source:Mwananchi
0 Comments
on