Fani
hizo ni sayansi za tiba na afya, ualimu wa sayansi na hisabati,
uhandisi wa viwanda, kilimo, mifugo, mafuta, gesi asilia, sayansi
asilia, mabadiliko ya tabia nchi, sayansi za ardhi, usanifu majengo na
miundombinu.
Serikali
inachukua uamuzi huo, baada ya kubaini kuwapo wanafunzi wanaosomea fani
hizo ili kupata mikopo, lakini baada ya kumaliza hukimbilia kufanya
kazi nyingine au nje ya nchi na hivyo kuendelea kuwepo upungufu wa
wataalamu waliowakusudia kubaki.
Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na mafunzo ya ufundi, Stella
Manyanya aliyasema hayo hivi karibuni, alipozungumzia utoaji wa mikopo
kwa wanafunzi wa elimu ya juu. Alieleza kuwa serikali inafikiria kuwe na
utaratibu kwa wanaonufaika na mikopo ya kipaumbele kuingia makubaliano
na serikali.
Alisema
suala hilo halitakuwa jipya kwani hapo nyuma walikuwa wakibanwa kuwa
lazima kufanya kazi angalau kwa miaka mitano serikalini na baadaye ni
ruhusa kwenda popote, lakini kwa sasa hawawezi kuwabana wote, lakini
lazima kufanya hivyo kwa hao wa kipaumbele.
Aidha Manyanya alizungumzia ulipaji mikopo hiyo na kudai wanaboresha sheria ya kukusanya madeni kwa kushirikiana na waajiri.
“Serikali
itakusanya madeni hata kwa wakopaji ambao wamejiajiri kwa sababu wengi
wakimaliza masomo hawafikirii kulipa,” alisema.”Sasa lazima walipe,
wakopaji watambue fedha hizo ni mikopo na lazima kulipa.”
Alisema
kwa wakopaji watakaoajiriwa, wizara inataka mkopo huo kuwa wa kwanza
kukatwa kabla ya mingine ili kuepuka kuingiliana na sheria za kazi,
zinazotaka mkopaji kuachiwa fedha fulani katika mshahara wake.
0 Comments
on