Kama hujawahi sikia kuhusu App ya Prisma, Unaweza Kuwa hujaijua vizuri sayansi na teknologia ya App inavyoendelea.
Prisma
ni photo editing application ambayo inafanya maajabu makubwa hasa
inapokuja issue ya photo editing kikubwa ni kutokana na Effect zake za
kipekee saaana,Lakini tatizo ni moja kwamba App ya Prisma haipatikani kwa watumiaji wa Android hii ipo special kwa watumiaji wa iOS PEKEE.
Lakini usijali wakati Prisma ikiwa ni kwaajili ya watumiaji wa iOS pekee nikisema iOS nAamaansha simu kama iPhone, Lakini kuna uhakika wa kupata effect kama hizo pia kwa watumiaji wa simu za Android.
Hizi hapa nimekuletea App 4 zenye uwezo mkubwa kama wa Prisma Ambazo wewe kama mtumiaji wa Android unaweza furahia kwa uwezo wake mkubwa:
1. PicsArt
Ukishaidownload fungua sehemu ya Effects katika App ya PicsArt Na utaona baadhi ya effect na baadhi ya filters kama vile pop art, paper and colours,
Ni kama vile ukiwa unatumia Prisma's ambako kuna poster, motion, shear, pastel, comic na gouache.
PicsArt
Pia ina vifaa vingnine vya kueditia ambavyo hujumuisha artistic
brushes, overlays, collage maker, drawing na painting tools
wakati huo huo ikikupa uwezo wa kutengeneza picha katika mfumo wa GIFs
videos.
2. SuperPhoto
SuperPhoto
ni application nyingine kwa watumiaji wa Android ambayo hukupa zaidi ya
effect 200 katika toleo la bure. Na vipi kama ukiamua kulipia app hii?
Vizuri, Utajipatia zaidi ya effect 1500 pamoja na mitandao miiingi ya
kijamii (social
community) kushare oicha zako, Lakini pamoja na hilo SuperPhoto huchukua
muda kidogo ili kukamilisha kuedit picha ako lakin picha hutoka katika
ubora wake.
3.Photo Lab
Unachotakiwa kufanya baada ya kudownload Photo Lab,
ni kwenda katika faili lake la Artistic Effects ili kuigeuza picha yako
katika pieces of art. App hii ina baadhi ya features nzuri saana.
Lakini wakati ukiapply filters, hakikisha picha ipo katika ubora wa juu
la sivyo matokeo hayatakupendeza.
4. Pikazo
Pikazo
ni application nyingine nzuri saana ambayo inaweza kutumika kubadili
picha kuwa katika mfumo wa Artwork au mwonekano wa katuni.
Chakufanya ni rahisi saana baada ya kuidownload, Chagua mwonekano wowote
utakaokupendeza na upload picha ako ili kuipata katika mwonekano
unaopenda. Iko haraka na rahisi sana kuitumia, Pikazo ni ni app nzuri
saana inafaa uijaribu.
Umeionaje hii Tunategemea comment ako baada ya kuijaribu!
0 Comments
on