Header Ads Widget

VIDEO | DIAMOND AWASILI KWENYE MJENGO WAKE WA SA, AWAPA MADONGO WALIOSEMA SI WAKE

Afrika Kusini sasa imekuwa nyumbani kwingine kwa Diamond baada ya kununua nyumba ya kifahari iliyopo jijini Pretoria.

Baada ya kutangaza kununua nyumba hiyo iliyomgharimu zaidi ya shilingi milioni 400, maneno mengi yalisemwa yakiwemo ya wale waliohisi amepiga changa la macho. Na sasa muimbaji huyo amethibitisha kuwa mjengo huo ni mali yake baada ya kuwasili rasmi Jumanne hii.
Akiwa na timu yake ya WCB, Diamond ameikagua nyumba kwa mara ya kwanza na kuwasogeza karibu nayo mashabiki wake kwa video alizoweka Instagram.

“Meet my neighbors ðŸ˜Š…mnh ujirani huu hata siku Ukiwa na shida ya chumvi sjui unaingiaje kujichekesha upewe!…. #MyNewCribInSouthAfrica,” ameandika kwenye video moja.
Kwenye nyingine ameandika, “Wow! If you don’t know yet today was my first time seeing my house physically since I bought it a month ago….and honestly I went crazy when I saw it coz I was so excited to… so proud of my baby @zarithebosslady for being a good leader in our love and life..”
Ya mwisho ilikuwa na ujumbe mkali zaidi uliowalenga wale waliodai si nyumba yake.
“Asa k*nya nak*nya mie makalio yanawauma wengine, eti inahuu..,” ameandika.
“Wambie wasininunie mie, wakazane….halaf hii clip naomba wanangu mnisaidie kuwatag wote waliokuwa busy kupost na kuzungumza Kuwa nyumba hii si yangu….waambie hizi ndio kwanza rasharasha clip hata kupost sijaanza bado..”
“Soon naamia ndani😂😂…halaf nlisahau, wakikwambia mie mswahili wambie Mswahili haswaaa👌… halaf uswahili wangu najua kuutumia na umefanya leo niwe na kibanda south asa wao Uzungu wao Umewapa nini?”

Post a Comment

0 Comments