Mahakama ya nchini Malawi imemuhukumu kifungo cha miaka miwili na kufanya kazi ngumu kijana anayefahamika kwa jina la Eric Aniva aliyekuwa akiwabikiri wasichana na kulipwa kiasi cha dola 7.
Kesi hiyo imedumu kwa miezi mitatu mpaka sasa tangu iliporipotiwa kwa mara ya kwanza na kituo cha habari cha BBC.
Kijana huyo alikamatwa mwezi Julai mwaka huu kwa amri ya Rais wa nchi hiyo Peter Mutharika kutokana na kitendo hicho kilichokatazwa huku akidaiwa kuwa tayari ameshawafanyia kitendo hicho zaidi ya wasichana 104 ilhali akiwa ni muathirika wa virusi vya ukimwi.
Hata hivyo hukumu hiyo imeonekana kutoridhiwa na baadhi wasichana waliowahi kufanyiwa kitendo hicho akiwemo Maria Nthepheya.
0 Comments
on