Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa amesema serikali itazingatia utawala na kanuni za utawala bora ili kuhakikisha kuwa haki za wafanyakazi wa nchi zinalindwa ipasavyo.
Ametoa agizo hilo wakati akifungua mkutano mkuu wa sita wa shirikishi wa vyama vya wafanyakazi nchini mjini Dodoma ambapo amesema sheria ya ajira inatoa sheria mbalimbali zinazoumika kuajiri na waajiri wanapaswa kufuata sheria hiyo kwani ndiyo ufunguo wa mahusiano mema utulivu na tija sehemu za kazi.
“Hii ni hoja ya kuhusu wafanyakazi kunyanyaswa, kushushwa vyeo na kusimamishwa kazi na wanasiasa, serikali hii makini chini ya uongozi wa Dkt John Pombe Magufuli itaendelea kuzingatia utawala na kanuni za utawala bora ili kuhakikisha kuwa haki za wafanyakazi wa nchi zinalindwa ipasavyo,”alisema Majaliwa.
“Kimsingi watumishi wa umma wanasimamiwa na mamlaka mbalimbali za nidhamu kulingana na masharti ya ajira watumishi husika kama kifungu cha 6 kwa kifungu kidogo cha 1 cha sheria ya utumishi wa umma sura 298 kikisomwa kwa pamoja na kanuni ya 35 ya kanuni za utumishi wa umma za mwaka 2003 zinazoelekeza mamlaka hizi ndizo zinazochukua mamlaka stahiki za kinidhamu hata pale ambapo maelekezo ya hatua hizo yanaweza kutolewa mamlaka,” aliongeza.
Kauli ya Waziri Mkuu imekuja katika wakati ambao baadhi ya wafanyakazi wamelalamika kuonewa na viongozi wa juu.
BY: EMMY MWAIPOPO
BY: EMMY MWAIPOPO
0 Comments
on