Header Ads Widget

Jihan aeleza atafanya nini endapo atapata nafasi ya kuwa video queen kwenye video ya staa wa Bongo


Miss Universe 2016 na mshindi wa tatu wa Miss Tanzania 2014, Jihan Dimach amesema akipata nafasi ya kuwa video queen kwenye video yoyote ya msanii wa Bongo ataonyesha kitu tofauti na sio kucheza cheza kama video queens wengine wanavyofanya.
Mrembo huyo ambaye anajipanga kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya dunia ya Miss Universe, amesema anapokea ofa nyingi kutoka kwa wasanii lakini kuna vitu wanashindwana.
“Mimi nataka nikionekana kwenye video niwe tofauti na wale video queen wa kucheza cheza tu,” alisema Jihan. “Yaani urembo wangu pamoja na vitendo ambavyo nitafanya vionyeshe huyo kweli ni video queen. Kwa hiyo niseme tu kuna mambo mazuri yanakuja kwenye upande huo tena kuwa wasanii wengi wamekuwa wakinicheki nadhani tukifikia makubaliano mtaniona,” alisema Jihan.
Pia mrembo huyo amewataka video queens kutumia nafasi wanazopata katika video mbalimbali za mastaa ili waende hata kimataifa.



Jiunge na DJADAM64.COM sasa

Post a Comment

0 Comments