Kufuatia shinikizo kubwa kutoka kwa wawekezaji waliovurugwa, Samsung imepanga kutangaza mabadiliko Jumanne hii.
Wawekezaji wengine wanataka pia kutengenishwa kampuni hiyo kuzalisha mawili, kwa mujibu wa Reuters. Samsung imekabiliwa na matatizo chungu mzima mwaka huu yakiwemo kusitishwa uzalishaji wa simu za Samsung Galaxy Note 7 na zingine mamilioni kuondolewa sokoni. Pia kuna zile mashine za kufulia nguo milioni 2.8 zilizorudishwa kiwandani.
Kashfa za kisiasa zilisababisha pia ofisi za kampuni hiyo mjini Seoul kuvamiwa katika matukio mawili tofauti. Wawekezaji wameanza kulalamika kuhusiana na jinsi kampuni hiyo inavyoendeshwa.
Bado Samsung haijathibitisha kama inafikiria ushauri wa kujigawa mara mbili.
Faida ya kampuni hiyo imeshuka kwa asilimia 30. Kampuni hiyo imedai kuwa kasoro za Galaxy Note 7 zinaweza kuigharimu dola bilioni 5.
Faida ya kampuni hiyo imeshuka kwa asilimia 30. Kampuni hiyo imedai kuwa kasoro za Galaxy Note 7 zinaweza kuigharimu dola bilioni 5.
0 Comments
on