Katibu wa chama cha wananchi CUF, Maalim Seif amelishutumu jeshi la polisi kwa kile alichodai kuvuruga mikutano inayoandaliwa na wafuasi wa chama hicho wanaomuunga mkono katibu mkuu huyo.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, amedai kushangazwa na nguvu kubwa inayotumiwa na polisi katika kuzuia mikutano ya ndani inayoandaliwa na wafuasi wa chama hicho wanaomuunga mkono huku wakiruhusu inayoandaliwa na mwenyekiti wa chama hicho Profesa Ibrahim Lipumba.
“Mpaka muda ninavyoongea na nyinyi waandishi wa habari gari iliyokuwa kituoni kama kielelezo au sahihi limeondolewa kituoni hapo na watuhumiwa wote wameachiwa huru na wapo mitaani huku wakitamba wanalindwa na jeshi la polisi. Wamekuwa wakitisha katika mitandao ya kijamii na katika mazingira ambapo wapo wanachama wa CUF bila ya hofu kwani wanaamini na kusema waziwazi kwamba jeshi la polisi ni sehemu yao na haliwafanyi lolote,” alisema Seif.
Aidha Maalif Seif alisema kuwa suala la kuachiwa huru watuhumiwa wa utekaji nyara wa viongozi na wanachama wa CUF ni ukiukaji wa haki na kumtaka waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Nchemba kuingilia kati