Muongozaji wa video za muziki nchini Tanzania, Director Khalfan amefunguka kwa kusema kuwa ushindani kwa madirector wa video nchini upo katika kufanya kazi nyingi na sio kufanya kazi bora.
Akiongea na djadam64 Jumamosi hii, Khalfan amesema kuwa madirector wengi wanashindana kwenye kufanya video nyingi huku chache kati ya hizo ndio bora.
“Mimi mwenyewe kazi nyingi za madirector wa Tanzania hazinipi challenge, ni madirector wachache sana ambao tunafanya nao kazi na wananipa challenge tena kwa video chache kwa sababu video moja anaweza akatoa nzuri nyingine kawaida,” alisema Khalfan.
Aliongeza, “Sasa hivi mimi naona madirector wengi wanashindana kufanya video nyingi na sio video kali. Kwa hiyo mimi binafsi naona tunasafari ndefu sana ya kushindana na madirector wakubwa wa nje,”
Muongozaji huyo hivi karibuni amefanya video ya wimbo ‘Raha Jipe Mwenyewe’ ya Linah Sanga.
0 Comments
on