Lady Jaydee amefunga ndoa kimya kimya? Hilo ni swali ambalo kila mmoja anajiuliza lakini majibu yapo tofauti.
Ukurasa wake wa Instagram, unaonesha dalili hizo na wengi wameendelea kumpongeza wakiwemo watu wake wa karibu. Lakini ukweli ndio huo?
Wiki iliyopita nilimuuliza meneja wake, Seven kama kweli muimbaji huyo wa ‘Sawa Na Wao’ amerudi ndoani lakini alinieleza kuwa Jide atatoa taarifa rasmi kuhusu hilo mwezi ujao.
Kabla ya kuanza kuchekesha ‘theory’ kadhaa zinazoweza kutupa jibu la kama kweli ndoa hiyo ipo, tumfahamu kwanza shemela wetu ni nani. Anaitwa Spicy, ni mwanamuziki mahiri wa Nigeria aliye chini ya label ya Flavour, 2nite Enter10ment Music Group.
Si msanii aliyekuwa anafahamika na wengi hapa Tanzania lakini inaonesha kuwa ni msanii mkubwa nchini humo na uwezo wake si haba.
Yeye mwenyewe kwenye post kadhaa za Instagram amedhihirisha pendo lake kwa Jaydee.
Kwenye post moja akiwa naye, Spicy ameandika: Can’t really explain it… So into you.” Kwenye nyingine ameandika: Don’t get it twisted, love is a beautiful feeling.” Siku kadhaa zilizopita, Jide alipost picha ya Spicy na kuandika: Wanna follow my bae???I permit you Follow him now @spicymuzik.”
Post zao zinazidi kuipa nguvu imani ya wengi kuwa huenda ikawa kweli Jaydee ameanguka kwenye penzi la staa wa Nigeria.
Lakini hebu tukeche akili kidogo. Kwanza, si kila unachokiona kwenye Instagram au mitandao mingine ya kijamii ni kweli – tena inapomhusu mwanamuziki! Vipi kama ikiwa ni video ya muziki? Mheshimiwa Temba (ana mke tayari), Linex, Akothee na wasanii wengine wamewahi kutuaminisha kuwa wamefunga ndoa lakini baadaye ikaja kuwa ni video ya muziki.
Kingine, tangu nimeanza kumfahamu Lady Jaydee, sijawahi kumtambua kama mtu anayeweka hadharani mambo yake binafsi. Hiyo ni ‘rule’ kubwa aliyojijengea kwa muda wote wa career yake – ana usiri wa hali ya juu katika mambo ya uhusiano. Na ndio maana hata wakati akiwa mke wa Gardiner G Habash, maswali ya ndoa yake alikuwa hayapi nafasi. Iweje leo Jide amekuwa mtu wa kuweka sana mahusiano yake mtandaoni? Umelifikiria hilo?
La mwisho, wiki moja iliyopita ambayo Jide na Spicy walikuwa visiwani Zanzibar, ndio wiki ambayo muongozaji wa video wa Afrika Kusini, Justin Campos na mke wake Candice, walikuwa huko.
Walikuwa wanashoot video ya nani? Kumbuka, ni Campos ndiye aliyeongoza video ya Ndindindi ya Lady Jaydee!
Kwakuwa hizo bado ni theory tu, wacha tusubiri mwezi ujao tamko rasmi litakapotoka.
0 Comments
on