Mwana FA amedai kuwa video ya wimbo wake mpya ‘Dume Suruali’ aliomshirikisha Vanessa Mdee ilifanyika mara mbili baada ya ile ya kwanza kutowaridhisha.
14693779_1810973885816195_1155827793011933184_n
Rapper huyo amekiambia kipindi cha Clouds E cha Clouds TV kuwa sababu iliyowafanya kuikataa video hiyo si ubora wa picha bali tafsiri ya video hiyo haikuendana na ile waliyokubaliana mwanzo.
“Mara ya kwanza ilikuja lakini sisi hatukuwa tumeridhika na viwango ambavyo ilikuwa nayo kulinganisha na vile ambavyo sisi tulikuwa tunavihitaji,” amesema.
“Si viwango vya picha au nini lakini ni tafsiri ambayo sisi tulikuwa tunaipata kutoka kwenye wimbo haikuwa tafsiri yenye kutosha kuwakilishwa na video ambayo tulikuwa nayo mara ya kwanza. Kwahiyo ikabidi nisafiri tena kwaajili ya kushoot video nyingine,” amesema FA.
Mpaka sasa video ya wimbo huo bado haijawekwa kwenye mtandao wa Youtube