Header Ads Widget

RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 35 & 36

Mwandishi: EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA   
“Asante sana Fred”
Wakiwa juu angani, wakaendelea kupata vinywaji mbalimbali, huku wakitazama baadhi ya chanel, za tv ndogo iliyopo kwenye kila meza ya safa lililopo ndani ya ndege hiyo ya kifahari. Gafla Rahab akaanza kujihisi vaibaya vibaya, huku mara kadhaa, akawa anajikaza ili Praygod asijue ni kitu gani kinacho endelea, ila gafla akajikuita akianza kutapika na kulichafua gauni lake alilo livaa

ENDELEA   
Furaha ikabadilika na kuwa mshike mshike ndani ya ndege kwani kadri muda ulivyo zidi kwenda hali ya Rahab ikaanza kubadilika na kujikuta mwili mzima ukianza kumtetemeka, na kutoa mapuvu mdomoni mwake. Frednando akawaamuru marubani wairudishe ndege haraka kwenye kiwanja cha nyumba kwake ili kumuwahisha Rahab, aweze kuonana na madktari. 

Macho ya Rahab yakabadilika na mboni zake nyeusi zikapotea na kubaki weupe kwenye macho yake jambo lililozidi kumchanganya raisi Praygod pamoja na Frednando ambaye hakujua ni ugonjwa gani ambao bibi harusi ameweza kuupata.
Haikuchukua muda mwingi, matairi ya ndege yakawa yanaserereka kwenye ardhi ya uwanja wa nyumbani kwa Frednando, ambapo Alisha waeleza madaktari wake wawe tayari kwa kumpokea mgonjwa.
Kwa kushirikia na Frednando, wakambeba Rahab na kumtoa nje ya ndege na kumuingiza kwenye gari maalumu la wagonjwa lililokuwa likiwasubiri. Moja kwa moja Rahab akakimbizwa kwenye jingo linalo tumiwa na Fredando kama hospitali inayo mtibu yeye na familia yake pale wanapo patwa, na hali yoyote ya kuumwa. Uzuri wa eneo lilipo jumba la Frednando, aliweza kuwekeza pesa nyingi kujijengea vitu muhimu kwa mahitaji yake, ikiwemo jengo la hospitali, lenye madaktari bingwa ambao Fredinando anawaamini sana
“Kaka hivi mke wangu atapona kweli?”
Raisi Praygod alizungumza huku machozi yakimlenga lenga, akamshuhudia mke wake akipakizwa kwenye kitanda cha matairi baada ya kushushwa ndani ya gari, na moja kwa moja akaingizwa kwenye chumba kilicho jaa vifaa muhimu kwa kumuhudumia mgonjwa mahututi
“Atapona tu, usijali rafiki yangu”
Fredinando alimfariji raisi Praygod, lakini yeye mwenye amechanganyikiwa kwani hakuamini kama siku kama hiyo kutajitokeza jambo kama hilo la kuhuzunisha. Wakiwa wamesimama kwenye nje ya mlango wenye kioo kikubwa, wakawashuhudia madaktari wakitumia mashine za kustulia mapigo ya moyo wakiziweka kwenye kifua cha rahabu ambaye amezima kabisa mapigo yake ya moyo.
Machozi taratibu yakaanza kumtoka raisi Praygod, hakuamini uzuri wote wa Rahab, unaweza kupotea muda wowote kuanzia sasa.
“Kaka jikaze”
Frednando alizungumza huku, naye machozi yakiwa yanamtiririka, uchungu anao upata rafiki yake, nao unaugusa moyo wake, kwani ni dakika chacha tu wametoka kucheka na kufurahi na shemeji yake ambaye muda mwingi anapenda kumtania kwa jina la ‘AFRICAN QUEEN’. Mashine zakupulia zinazo soma mapigo ya moyo jinsi yanavyo kwenda yakazidi kuwachanganya madaktari hawa wane, kwani ni mstari mmoja ulio nyooka ndio unakatiza kwenye mashine hiyo, huku kukisomeka sifuri mbili za rangi nyekundu zikiashiria kwamba Rahab mapigi ya moyo hayafanyi kazi, moja inawezekana amesha fariki au moyo wake upepata mstuko mkubwa
                                                                                           ***
Si Fetty wala mwenzake yoyote aliye weza kujinyanyua kutoka kwenye sakafu walipo kaa, kila mmoja macho yake yaliyo jaa machozi, wakawa wanaitazama sura ya kipande cha mwanaume, aliye fura kwa hasira na si mwingine bali ni bwana Rusev, aliye simama huku bastola yake ikiwa mkononi mwake. Kila mmoja akatamani kujitetea, ila nguvu hakuwa nazo za kutosha kusema anaweza kupambana na bwana Rusev, anaye onekana kuchukia baada ya mapiganaji yake matatu kuuliwa kinyama
“Hatuna tulicho kibakisha tena duniani, tumekuwa ni watu waovu. Hatuna pa kwenda zaidi ya kaburini. Tuue sisi yupo tayari”
Anna alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake, huku mikono yake yenye kufungwa pingu akiendelea kumshika Halima, aliye kwenye hali ngumu sana.
“Ehee Mungu zipokee roho zetu, na utusamee makosa yetu tuliyo yafanya. Amen”
Anna alizungumza kwa sauti ya unyonge iliyo wafanya wezake kuendelea kulia kwa uchungu, kwani hakuna aliye tarajia kwamba maisha yake yatakuwa hivyo. Maneno ya Anna, yakamfanya bwana Rusev, kumwagikwa na chozi lililo washangaza askari wake waliopo nje wakiwatazama.
Bwana Rusev akawamrisha askari wake kuingia ndani na kuwechukua Fetty na wezake, ambapo akawaamrisha wavalinye vipande vya vigunia vyuesi kwenye vichwa vyao wasijue ni wapi wanapelekwa.
Wakatolewa ndani ya chumba hicho huku wakiwa wamebebwa, kwenye mabega ya askari walio jazia miili yao kwa mazoezi magumu wanayo yafanya kila kukicha. Moja kwa moja wakawatoa nje ya jumba hilo na kuwaingiza kwenye helcoptar ambapo bwana Rusev naye akaingia ndani ya helcoptar hiyo. Mtiani mkubwa kwa Fetty na wezake ni kujua ni wapi wanapo kwenda, kutokana hawakuwa na jinsi yakufanya huku mikono yao ikiwa imefungwa pingu na miguu yao ikiwa imefungwa minyororo mirefe.
Mwendo wa lisaa zima wakawa wapo angani, ambapo moja kwa moja wakafika katikati ya kina cha bahari, ambapo helcoptar hiyo taratibu ikaanza kushuka chini. Kutokana haoni chochote ikawa ni ngumu kujua ni kitu gani kinacho fwata mbeleni. Jinsi helecoptar hiyo, ilivyo zidi kushuka chini ndivyo sehemu hiyo kubwa ya maji ilivyo anza kujigawa. Maji ya sehemu kubwa yakatawanyika na  mfuniko mkubwa wa chuma ukafunguka na kuiruhusu helcoptar hiyo kuingia ndani, ambapo ndipo kuna kambi kubwa ya silaha ya bwana Rusev, ambayo si rahisi kwa mtu kuweza kugundua swala hilo. 

Kutona na utaalamu mkubwa waliweza kujenga ngome kubwa chini ya bahari ambapo, ipo ndani ya miamba. Ambapo wameweza kutengeneza hewa ya oksijeni, wanayo weza kuitumi ndani ya miamba hiyo mikubwa huku taa kubwa za umeme zikiwa zinawaka masaa 24. 

Wanajeshi wote wanao ishi kwenye ngome hiyo ni makomandoo na niwatu wenye vipaji maalimu, ambao bwana Rusev aliweza kuwachukua sehemu mbalimbali dunia, na kuwaweka pamoja na kuanza kutengeneza silaha ambazo ni adimu sana duniani. Huku siku hadi siku wakitengeneza mabomu ya nyuklia, ambayo ni hatari pale yanapo tumiwa kwenye kushambulia sehemu yoyote kwenye kiumbe, hai nilazima kitaatjirika vibaya.
Fetty na wezake wakapokelewa na wanajeshi, wakapelekwa kwenye wodi, kabla hawajatolewa vipande vya magunia kwenye vichwa vyao, wakachomwa sindano za usingizi, ambazo zikawafanya wapoteze fahamu na kulala fofofo. Wakaanza kuhudimiwa kwenye majeraha yao yote pasipo wao kujigundua.
“Mkuu hawa ni kina nani?”
Daktari mmoja aliuliza kwa lugha ya kirusi.
“Hawa mabinti wananifaa sana kwenye kazi yangu, hakikisheni afya zoa zinatengemaa na kuwa katika hali nzuri sawa”
“Sawa mkuu”
Bwana Rusev akatoka kwenye wodi walipo lazwa Fetty na wezake kisha na kwenda kufwatilia utendaji wa kazi wa vijana wake ndani ya ngome yake hiyo.
                                                                                                  ***
Taratibu vimistari vya mashine, iliyopo pembei mwa kitanda alicho lazwa Rahab, ikaanza kuonekana vikiwa vimepinda pinda, ikiashiria kwamba ameanza kupumua hii ni baada ya madaktari kuendelea kuustua moyo wake kwa kutumia mashine maalumu za kuweza kustulia mapigo ya moyo. Ikawapa nafasi madakari kuweza kufanya uchunguzi wa kina juu ya tatizo lililo mkumbwa Rahab. 
Raisi Praygod akazidi kumuomba Mungu, huku macho yake akiwa ameyatoa kwenye mashine iliyo endelea kuonyesha vimistari vidogo vya kijani ikiashiria kwamba mke wake ameanza kupumua. Baada ya kusimama kwa muda mrefu, Fredando akamchukua raisi Praygod hadi kwenye moja chumba cha mapumziko, ambacho mara nyingi hukitumia pale anapokuwa anazungumza na madaktari wake.
Matokeo ya majibu ya vipimo, ikawa ni jambo la kustaajabisha kwa madaktari ambao wakaanza kujiuliza ni nani ambaye amehusika na ugonjwa wa rahabu
“Wewe umezoeana na baso, peleka majibu”
Mmoja wa madaktari alipendekeza daktari Canter, mwanamama mpole na mchishi kuweza kupelea majibu hayo
“Hivi jamani, ni kweli haya majibu yapo sahihi”
“Jamani si sote hapa tumepima na majibu kuwa hivyo, na tukarudia kwa kipomo kingine majibi yamekuja hay ohayo”
“Wewe peleka sisi huku tuendeleaa kumugudumia mgonjwa”
Bi canter akatoka kwenye chumba alipo lazwa Rahab, moja kwa moja akaelekea kwenye chumba mara nyingu hukitumia kuzungumza na bosi wao. Baada ya kuingia ndani ya chumba hicho raisi Praygod, akanyanyuka kwenye kiti alicho kaa, na kumpokea daktati huyo kwa macho makali yaliyo jaa wasiwasi. Frednando akamuomba daktari kukaa kwenye kiti cha pembeni
“Mke wangu anatatizo gani dokta?”
“Kaa chini kaka”
Frednando alizungumza huku akimshika mkono raisi Praygod na kumkalisha kwenye kiti alichokua amekikalia
“Tumeweza kumfanyia mgonjwa uchunguzi wa kina, na tumeweza kugundua kwamba……”
Baada ya kfika sehemu ya tatizo linalo msumbu Rahab, dokta Canter akanyamaza na kuwatazama matajiri wake hao, ambao wote wamemtumbulia mimacho
“Mke wako muheshimiwa, tumemkuta na….. na sumu nyingi”
“SUMUU…..!!!”
Raisi Praygod alizungumza huku akiwa anashangaa swala hilo
“Ndio sumu ambayo inaoenekana iliwekwa kwenye kinywaji alicho kunywa dakika chache kabla ya kuanza kufanya kazi mwilini mwake”
                                                                                
SHE IS MY WIFE(36)

Raisi Praygod akamgeukia rafiki yake kipenzi Frednando, na kumtazama kwa macho makali ambayo alianza kumtilia mashaka rafiki yake huyo, ila Frednando naye alionekana kuwa hatambui lolote lililo jitokeza katika hili swala kwani muda mwingi walikuwa pamoja.
“Ila tunaendelea kuitoa sumu iliyo ingia mwilini mwake”
“Sawa”
Frednando alimjibu dokta Canter na kumfanya dokta huyo kuomba kunyanyuka na kuondoka ndani ya chumba hicho huku akiwaacha Raisi Praygod na Frednando wakiwa na maswali mengi juu ya nani ni aliye weka sumu kwenye kinywaji cha Rahab.
 **(MASAA MACHACHE KABLA)**
    Kila alipo yatupa macho yake usoni mwa raisi Ptagod Makuya na mke wake Rahab, roho ikazidi kumuuma Mercy, binti mrembo, ila ni mfanyakazi hodari wa kupika katika jumba hili la tajiri Frednando, tangu siku ya kwanza kumuona Praygod kuingia katika jumba hili moyo wake ulipata shinikizo kubwa la maumivu yaliyo changanyikana na upendo mkubwa. Japo asili yake ni mmexco halisi, ila alijikuta akimpenda mwanaume mwenye ngozi nyeusi kama Praygod.
Halikuwa ni jambo rahisi kuweza kulitamka swala la kumpenda Praygod kwa mtu yoyote ndani ya jumba hili kwani alihisi kwamba itakuw ni hatari kubwa sana kwake, kwani akilini mwake alisha anza kufikiria jambo ambalo lingemfanya akiuke maadili ya kazi yake pamoja na sheria za nchi yake. Ila hakuwa na jinsi zaidi ya kupanga mipango mizito kichwani mwake ya kumuondoa duniani Rahab, ili we rahisi kwake kujiweka karibu na Raisi Praygod, anaye onekana kudatishwa na penzi la Rahab.
Macho ya Mercy, yaliendelea kuwashuhudia Rahab na Praygod jinsi wanavyo endelea kufurahi wakiwa katika mavazi yakuependeza, ikiashiria kwamba kwa sasa ni mke na mume.
Japo ni wafanyakazi wengi wakiume waliendelea kumtamani Mercy ila hapakuwa na aliye ambulia hata kupewa matumaini ya kuoenyeshwa kwamba amependwa na binti huyo. Kila mmoja alijikuuta akijibiwa mbona na binti huyo mrefu, mwenye nywele ndefu zinazo fika mgongoni, huku akiwa na umbo fulani jembamba la kimisi, ila lenye mvuto kwani liliweza kuchukua vazi lolote litakalo mpendeza.
Macho ya Mercy hayakucheza mbali na Rahab, aliye shika kinywaji chake mkononi, huku pembeni yake kukiwa na mumewe aliye endelea kuachia tabasamu pana lililo mfanya azidi kuwa mzuri na kumchanganya Mercy.
“Oooh Mungu wangu nisaidie mimi”
Mercy alizungumza huku mkoni mwake akiwa ameshika kitambaa alicho saga, kidonge komoja cha sumu, kali sana inayo tumika katika kunyunyizia katika mimea ya matunda aina ya apple, ambalo ni zao kubwa sana linalo patikana katika nchi ya Mexco. Mercy akaanza kutafuta uwezekana na kuweza kumuwekea unga huo Rahab kwenye kinywaji alicho kishika kwenye mkono wake. Wakati wa kuwasalimia maharushi na kuwapa mikono ikawa ndio nafasi ya pekee kwa Mercy kuweza kutimiza adhima yake kwa Rahab.

Wakatu wakaanza kupita walio maharusi, huku wengine wakiwakumbatia maharusi kwa ishara ya kuwapongeza. Mercy akaanza kumkumbatia raisi Praygod huku kwenye vidole vyake akiwa ameshika chenhachenga kidogo za unga wa sumu, alipo mfikia Rahab, akamkumbatia na kupata nafasi ya kunyunyiza unga wa sumu kwenye kinywaji cha Rahab pasipo mtu yoyote kuweza kushuhudia tukio hilo, akampiga mabusu kadhaa Rahab ya mashavuni, huku moyoni mwake akiwa akiwa na furaha kwani Rahab kwa muda wowote anaweza kuja na kuwa marehemu mtarajiwa.
Kitu kilicho anza kumshangaza Mercy ni jinsi Rahab alivyo anza kupata ugumu wa kunywa kinywaji hicho, kwa mara kadhaa Rahab alikipeleka kinywaji hicho hadi mdomoni mwake ila akakirudisha na kujikuta akizungumza au akitabasamu na memewe aliye onekena kujawa na furaha sana.
“Foolish”(Pumbavu)
Mercy alizungumza baada ya kusikia kwamba bosi wao amewakabidhi ndege ya kifahari Raisi Praygod pamoja na Rahab. Akawashuhudia Rahab, Praygod na Frednando wakielekea kwenye ndege na kuingia. Mercy akaondoka kwa hasira eneo la sherehe na kuelekea chumbani kwake, akajifungia na kujirusha kitandani mwake na kuanza kupiga piga mto wake kwa ngumi, kwani ni maumivu mazito ya mapenzi yaliuchoma mayo wake hadi jasho jembamba likaanza kumwagika.
Ndani ya nusu  saa akaanza kusikia ving’ora vya gari la wagonjwa, kwa haraka akakimbilia dirishani na kufungua kutazama nje, kutokana na chumba chake kuwa gorofa ya nne kwenda juu, aliweza kushuhudia jinsi madaktari wao wakifanya juhudi za kumpa huduma ya kwanza Rahab, mara baada ya kumshusha kwenye ndege.
“I win”(Nimeshinda)
Alizungumza huku tabasamu akiendelea kuliachia, sasa akilini mwake akatambua kwamba kinacho fwata hapa ni yeye kuanza kujiweka karibu na Praygod kwani amefanikiwa kumuondoa adui yake namba moja, japo Rahab hakuwahi  kumfanyia jambo lolote ambalo alipaswa kumlipizia kisasi kwa kumsababishia kifo.
                                                                                            ***
   Frednando akamuaga Rais Praygod, akatoka nje ya jengo la hospitali huku moyoni mwake akiwa amefadhahika sana kwa kile kilicho tokea kwa mke wa rafiki yake kipenzi Praygod. 

Akaingia kwenye gari lake na kumuamrisha dereva aendeshe kwa kasi gari hilo hadi nyumbani kwake, huku akipiga simu kwa msimamizi mkuu wa jumba lake aweze kuandaa kikao kikubwa na wafanyakazi wote walio hudhuria kwenye sherehe ya harusi muda mchache ulio pita. 

Ndani ya dakika kumi akawa amefika kwenye jumba analo ishi, kuingia sebleni akawakuta wafanyakazi wake wote wakiwa kwenye mkao wa kumsubiria bosi wao huyo, ambaye huwa mara nyingi hapendi ujinga na swala la kumuondoa mtu duniani kwa kumtandika risasi ni dogo sana kwake, endapo mtu huyo ataonekana kuenenda kinyume na taratibu zake alizo ziweka kwa wafanyakazi wake hao.
Frednando akapita katikati yao huku akioenekana kukasirika hadi rangi ya ngozi yake kubadilika na kutawaliwa na uwekundu fulani. Akawatazama wafanyakazi wake karibia wote kutokana na wingi wao, hakuweza kuzitazama sura zote.
“Esto es ridiculo”(Huu ni ujinga)
Frednando alizungumza kwa lugha ya kispain, huku akiwfoka kwa sauti ya juu, na kuzidi kuwaogopesha wafanya kazi wake hao, ambao wengi humuogopa sana bosi wao.
“Quien habĺa puesto veneno en ;a bebida de Rahab”(Ni nani aliye weka sumu kwenye kinywaji cha Rahab?)
Ukali was suati ya Frednando, ikapenya masikioni mwa Mercy aliyekuwa akishuka ngazi kuja chini sebleni kusikiliza kikao walicho itiwa na bosi wao huyo. Ikambidi asimame kuchungulia chini na kuona wezake wakiwa wamesimama kwenye kundi kubwa hku kila mmoja akionekana kuwa makini na kumsikiliza bosi wao
“Jefe habria sido mejoe si vemos los videos gue se graban en toda la boda sel acontencimento”(Bosi itakuwa ni vizuri tukitazama viseo zilizo rekodiwakwenye tukio zima la arusi)
Mshauri wa Frednando alitoa wazo ambalo kila mmoja alionekana akingong’ona akiamini hiyo itakuwa ni njia mafaka kwa wao kuweza kumjua ni nani muhusika. Wazo hilo likamfanya Mercy kuanza kutetemeka mwili mzima na kushindwa kushuka chini zaidi ya kujibanza kwewye sehemu alipo simama na kuendelea kutazama ni nini kitakacho fwata. 

Mafundi mitambo walio husika na swala zima la kurekodi matukio yaliyo tokea kwenye harusi, wakaunganisha picha za matukio yote kwenye mkanda mmoja kisha na kuuweka kwenye kifaa maalumu cha kuwezesha mkanda huo kuonyesha katika tambaa kubwa lililopo sebleni, taa zote zikazima na kubakiwa na mwanga wa mkali wa kifaa kilicho kuwa kinamulika kwenye tambaa hilo na kuonyesha matukio yoyote.
Mercy naye hakuwa mbali katika kutupia macho yake kwenye video hiyo inayo onekana na wezake wote pamoja kwenye seble hiyo kubwa. Ikafika wakati wakiwapa mikono maharusi kwa ishara ya kuwapongeza. Mercy akajiona akipita kwa Raisi Praygod kisha akafika kwa Rahab na kumkumbatia huku akipimpiga mabusu.
“Detener inmediatemente”(Simamisha hapo hapo)
Frednando alizungumza kwa sauti ya juu na kumfanya muongozaji wa video hiyo kusimamisha sehemu inayo muoenyesha Mercy akimkumbatia Rahab kwa furaha. Mercy akajikuta akiitumbualia macho sehemu hiyo iliyo simamishwa huku mapigo ya moyo yakimuenda kasi sana.

==> ITAENDELEA

Post a Comment

0 Comments